KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) imesema imejipanga kujiendesha
kwa faida, ikiwa ni pamoja na kubadilisha mtambo wa uchapishaji ili
kuleta ushindani kwenye soko. Mhariri Mtendaji wa TSN, Dk Jim Yonazi
alisema hayo jana wakati akihojiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Uwekezaji na Mitaji mjini Dodoma.
“Kimsingi, sisi ni wafanyabiashara, tunajipanga katika kuhakikisha tunafanya biashara kiufanisi zaidi,” alisema Dk Yonazi na kuongeza kuwa, mwenendo wa kampuni kimapato umekuwa ukitegemea matangazo.
Soko kuu la TSN linategemea wizara, mashirika ya umma na kumekuwa na ushindani mkubwa. Alisema ushindani huo wa kibiashara, umechangia kubuni na kuanzishwa Kitengo cha Habari za Mtandao ili kuhakikisha wasomaji wanapata habari kila zinapotokea.
Alisema japo kumekuwepo na changamoto nyingi, wataendelea kujitahidi ili kufikia malengo waliyojiwekea kwa kushirikiana na wasambazaji na wauzaji ili magazeti hayo yafike sokoni kwa wakati na kuongeza mauzo.
Akizungumzia changamoto zinazoikabili kampuni hiyo, alisema kumekuwa wadaiwa sugu, ambao wanawapitia kuona ni namna gani madeni hayo yatalipwa.
“Wadaiwa wakubwa ni serikali na taasisi zake, tumekuwa tukifuatilia, baadhi ya taasisi zimeonesha kuwa zinapitia changamoto ya kifedha na tumekwenda hadi hazina, lengo likiwa ni kuhakikisha madeni yanalipwa,” alisema na kuongeza kuwa, walikwenda hadi Zanzibar na wameahidiwa kuwa kuanzia mwezi ujao, wataanza kulipa.
Aidha, alisema kampuni hiyo inamiliki majengo mawili; moja lipo Mtaa wa Samora na Tazara jijini Dar es Salaam, na sasa wanakusudia kufanya uwekezaji mkubwa mkoani Dodoma, ambapo watajenga jengo la kisasa litakalokuwa na ofisi kwa ajili ya kupangisha.
Pia alisema wanakusudia kuingia katika soko la Afrika Mashariki na Kati na wameshaingia makubaliano na Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) ili wauze Kiswahili nchi zinazoizunguka Tanzania. Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Albert Obama wakati umefika kampuni hiyo kufanya mabadiliko ili ijiendeshe kwa faida.
“Punguzeni watu ili uwe na menejimenti ambayo unaimudu,” alisema Obama.
Katika michango yao, wabunge walihoji kwa nini waandishi wa mikoani hawaajiriwi, namna gani kampuni imejipanga kutoa taarifa kupitia mtandao na ina wafanyakazi wangapi, kwa sababu imekuwa ikilalamika kwamba ina ukosefu wa fedha wakati ina mlolongo wa mameneja wapatao 10 wanaongozwa na Mhariri Mtendaji.
“Mlolongo huo wa mameneja ni lazima uwe tatizo kubwa kwenye matumizi, kwani kila kitengo kinakuwa kinajitegemea. Nahitaji bajeti ionekane, mnajiendesha kwa mfumo wa kiserikali na si wa kibiashara,” alihoji Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu (CCM).
Awali katika taarifa yake, ilielezwa kwamba kampuni hiyo kwa asilimia 99 inamilikiwa na serikali kupitia kwa Msajili wa Hazina na Mkurugenzi Mtendaji anamiliki asilimia moja. Kampuni hiyo inachapisha magazeti ya Daily News, Sunday News, HabariLeo na SpotiLeo, pia inamiliki kiwanda cha uchapishaji.

0 comments:
Post a Comment