WAKATI serikali ya awamu ya tano ikiendelea na hekaheka za kuhamishia
makao makuu yake mkoani Dodoma, baadhi ya wakazi wa mkoa huo wamelaani
hatua hiyo ya serikali na kusema inawasababishia matatizo makubwa,
“Sisi tunafahamu kuwa eneo hili halijapimwa na watu tuliopo hapa ni wazawa hivyo tunashangazwa na watu kuja na kudai wana hatimiliki za maeneo haya.
“Tunajutia uamuzi wa Rais Magufuli kuhamishia rasmi makao makuu ya nchi Dodoma, tumeanza kupata matatizo makubwa, watu wenye hati wanadai kuwa wameuziwa maeneo yetu,” amesema Nicholaus Lupimo, Mkazi wa Ndachi.
Ameongeza kuwa, wamekuwa wakipigwa na askari walioagizwa kuondoa wazawa, ambao wanaitwa wavamizi katika eneo hilo licha ya kuishi hapo kwa zaidi ya miaka hamsini sasa.
John Masala, aliyezaliwa mwaka 1954 katika eneo la Ndachi amesema Babu na Baba yake wamekuwa wakazi wa eneo hilo tangu mwaka 1915 na kwamba hata yeye alizaliwa katika eneo hilo ambalo ameishi mpaka sasa.
“Sisi hatujatoka Rwanda wala Burundi, kama wanatuona sisi ni wakimbizi au wavamizi basi waturudishe tulipotoka,” amesema.
Kwa upande wake Jackson Mpilimi, ameeleza kuwa alizaliwa katika eneo hilo mwaka 1968, na hawajawahi kuhama wala kuona maeneo hayo yanapimwa katika kipindi chote hicho.
“Baada ya tangazo la Serikali kuhamia rasmi Dodoma, watu wameingia katika eneo hili wakiwa na hati tunazoamini kuwa ni ‘feki’ wanadai kuwa walishauziwa maeneo haya. Tunafukuzwa na polisi na kupigwa mabomu,” amesema.
Wananchi hao waliamua kuitisha mkutano wa hadhara baina yao na Godwine Kunambi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma siku ya leo ambapo alifika katika eneo hilo ili kusikiliza madai yao.
Amewaomba wananchi hao kumpa siku saba ili aweze kufuatilia kwa kina na kujua kama eneo hilo kama lipo chini CDA au manispaa.
“Nawaomba muwe watulivu nitashughulikia jambo hili ndani ya siku saba na kuwapatia majibu ya kina. Hakuna haki ya mtu yeyote itakayopotea, kama kuna watendaji au mamlaka imehusika katika kupoteza haki za wananchi basi tutatoa taarifa sehemu husika na hatua zitachukuliwa,” amesema.
Wakizungumza na mtandao huu, wakazi wa Ndachi kata ya Miyuji, Manispaa ya Dodoma, wamesema baada ya serikali kutangaza kuhamishia makao makuu yake Dodoma, tayari wameanza kuporwa ardhi yao.Wameenda mbali zaidi na kutishia kuwakata kwa mapanga na kuwajeruhi kwa mishale watu wanaovamia maeneo yao kwa madai kuwa wana hatimiliki kutoka Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) pamoja na halmashauri.
“Sisi tunafahamu kuwa eneo hili halijapimwa na watu tuliopo hapa ni wazawa hivyo tunashangazwa na watu kuja na kudai wana hatimiliki za maeneo haya.
“Tunajutia uamuzi wa Rais Magufuli kuhamishia rasmi makao makuu ya nchi Dodoma, tumeanza kupata matatizo makubwa, watu wenye hati wanadai kuwa wameuziwa maeneo yetu,” amesema Nicholaus Lupimo, Mkazi wa Ndachi.
Ameongeza kuwa, wamekuwa wakipigwa na askari walioagizwa kuondoa wazawa, ambao wanaitwa wavamizi katika eneo hilo licha ya kuishi hapo kwa zaidi ya miaka hamsini sasa.
John Masala, aliyezaliwa mwaka 1954 katika eneo la Ndachi amesema Babu na Baba yake wamekuwa wakazi wa eneo hilo tangu mwaka 1915 na kwamba hata yeye alizaliwa katika eneo hilo ambalo ameishi mpaka sasa.
“Sisi hatujatoka Rwanda wala Burundi, kama wanatuona sisi ni wakimbizi au wavamizi basi waturudishe tulipotoka,” amesema.
Kwa upande wake Jackson Mpilimi, ameeleza kuwa alizaliwa katika eneo hilo mwaka 1968, na hawajawahi kuhama wala kuona maeneo hayo yanapimwa katika kipindi chote hicho.
“Baada ya tangazo la Serikali kuhamia rasmi Dodoma, watu wameingia katika eneo hili wakiwa na hati tunazoamini kuwa ni ‘feki’ wanadai kuwa walishauziwa maeneo haya. Tunafukuzwa na polisi na kupigwa mabomu,” amesema.
Wananchi hao waliamua kuitisha mkutano wa hadhara baina yao na Godwine Kunambi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma siku ya leo ambapo alifika katika eneo hilo ili kusikiliza madai yao.
Amewaomba wananchi hao kumpa siku saba ili aweze kufuatilia kwa kina na kujua kama eneo hilo kama lipo chini CDA au manispaa.
“Nawaomba muwe watulivu nitashughulikia jambo hili ndani ya siku saba na kuwapatia majibu ya kina. Hakuna haki ya mtu yeyote itakayopotea, kama kuna watendaji au mamlaka imehusika katika kupoteza haki za wananchi basi tutatoa taarifa sehemu husika na hatua zitachukuliwa,” amesema.
0 comments:
Post a Comment