KAMATI ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC), imeshindwa kupitia
hesabu za Mfuko wa Pensheni wa PSPF na kulazimika kuahirisha kikao
chake, baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James
kushindwa kuhudhuria kikao cha kamati hiyo bila kutoa taarifa.
Katibu Mkuu huyo ndiye alipaswa kwenda mbele ya kamati hiyo na viongozi wa mfuko huo kwa kuwa PSPF haina bodi na kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, zinataka shirika ambalo halina bodi, Katibu Mkuu anayewakilisha serikali kufika mbele yake.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka, alisema kamati imesikitishwa na kitendo cha Katibu Mkuu huyo na kubainisha kuwa wajumbe, wamekitafsiri kama ni dharau kwa kamati hiyo na Bunge.
"PAC haitaki dharau na kuburuzwa kwa sababu inajulikana wazi kuwa katibu huyo alipewa taarifa ya kuhudhuria kikao hicho na kuthibitisha kuwa atahudhuria, lakini hakufika bila kutoa taarifa yoyote,” alisema Kaboyoka.
“Tunajua hili si kosa lenu, ila Katibu Mkuu amewaponza. Naagiza Katibu Mkuu huyu afike mara moja kesho afike kwenye kamati bila kutuma mwakilishi,” alisisitiza.
Alisema hali ya mfuko huo hairidhishi kwani dalili zinaonesha kuwa, unakaribia kufa kutokana na kuelemewa na madeni ambayo mengi kati yake unaidai serikali.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilaly alisema mahudhurio ya katibu huyo katika kamati hiyo ni muhimu kwani anapaswa kujibu namna serikali itakavyouokoa mfuko huo kutokana na kuendelea kuwa katika hali mbaya ya kifedha.

0 comments:
Post a Comment