MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) itavifuata vikundi 87 vya
ujasiriamali katika maeneo yao, kuwapa elimu ya namna ya kusajili bidhaa
zao na kufanya ziwe na ubora na ziweze kupata masoko ya ndani na nje.
Akizungumza kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini ya Ngongo,
Lindi, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa TFDA, Gaudensia
Semwanza alisema kupitia maonesho hayo yaliyofika tamati jana, TFDA
imevifikia vikundi 87 vya wajasiriamali na kujua taarifa zao.
“Katika maonesho haya tumefikia vikundi 87 vya wajasiriamali na hivi
tutavifuatilia maeneo yao katika mwaka huu wa fedha, lengo likiwa ni
kuwapa elimu ya namna ya kusajili bidhaa zao na kufanya usindikaji bora
wa bidhaa ili ziwe na ubora,” alisema.
Aidha, Semwanza alisema TFDA imetoa elimu ya kuepuka matumizi ya
vipodozi vyenye madhara na vya kuongeza makalio kwa wanafunzi wa vyuo,
sekondari na shule za msingi wapatao 41,000 katika mikoa 10.
0 comments:
Post a Comment