MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Bosco Ndunguru, kulipa malimbikizo
yote ya mishahara ya miezi 22 yanayofikia Sh 660,000 ya mlinzi wa Shule
ya Msingi Ndevelwa, Agustino Paul (58), badala ya kuendelea kumpiga
danadana.
Mwanri alitoa agizo hilo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Ndevelwa iliyopo katika manispaa hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kuhutubia wananchi na kutoa nafasi ya kuuliza maswali au kueleza kero zao.
Baada ya mlinzi huyo kutoa malalamiko yake, Mwanri alimwita Mtendaji wa kata hiyo Hamis Kasonta ili kutoa ufafanuzi wa madai hayo, ambapo alikiri mlinzi huyo kutolipwa mishahara yake na uongozi wa shule hiyo ya serikali kwa miezi 22.
Diwani wa kata hiyo, Seleman Maganga, alieleza kuwa awali mlinzi huyo alikuwa anapata mshahara wake kama kawaida, lakini baadaye wakaacha kumlipa kwa kisingizio cha serikali ya kijiji kutopokea fedha yoyote ya uwezeshwaji kutoka halmashauri ya manispaa.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Chatta Lukela, alisema suala hilo lipo chini ya uongozi wa shule na serikali ya kijiji ndio inayopaswa kumlipa mishahara yake yote mlinzi huyo.
Baada ya maelezo hayo, Mwanri alisema kwa kuwa serikali ya kijiji haijapata mgao wa fedha za uwezeshwaji kutoka halmashauri ya manispaa, deni hilo lilipwe moja kwa moja kutoka ofisi ya mkurugenzi wa manispaa na utaratibu wa malipo uanze mara moja hata kama ni kidogo kidogo.
Ili kuhakikisha deni hilo linalipwa, Mwanri alimwagiza mkuu wa wilaya ya Tabora, Queen Mlozi kulisimamia na kumpa mrejesho wa kufanyika kwa malipo hayo.
Akizungumza mlinzi huyo, alisema alianza kazi hiyo mwaka 2014 kwa makubaliano ya kulipwa Sh 30,000 kwa mwezi na alilipwa miezi kadhaa lakini baada ya hapo hakulipwa tena ila aliambiwa avumilie fedha zikipatikana atalipwa.
"Baada ya kukaa miezi kumi bila kulipwa niliamua kuacha kazi lakini baadaye wakanirudisha tena huku wakiahidi kunilipa kidogo kidogo mpaka deni liishe, ahadi hiyo haijatekelezwa hadi leo na bado niko kazini," alisema.

0 comments:
Post a Comment