UKARABATI wa miundombinu iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi mkoani
Kagera umeanza, na tayari Sh milioni 800 zimetumika kati ya Sh bilioni
tano zilizotolewa na wadau mbalimbali katika kuwachangia waathirika wa
tetemeko hilo lililotokea Sept 10, mwaka huu na kusababisha vifo,
uharibifu wa majengo na miundombinu mbalimbali.
Aidha, imeelezwa kuwa, inahitaji miaka miwili au mitatu kwa mkoa huo kurejea katika hali ya kawaida kutokana na maeneo mengi kuathirika vibaya.
Hayo yalibainishwa mjini Dodoma jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohammed Mchengerwa alipokuwa anazungumzia taarifa ya serikali ya maafa ya tetemeko yaliyotokea mkoani Kagera.
Taarifa hiyo iliwasilishwa mbele ya kamati hiyo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. Alisisitiza kuwa, serikali imeihakikishia kamati hiyo kuwa inaendelea na jitihada za kusaidia waathirika hao.
Aidha, alisema kwa mujibu wa taarifa ya waziri huyo kwa sasa wanafunzi wa shule ya sekondari Ihungo wamehamishwa kupelekwa shule ya Mwani ili kuendelea na masomo.
“Hadi sasa wagonjwa 440 waliokuwa hospitali wameendelea kupatiwa matibabu na kati ya wagonjwa hao sita wamefariki dunia,” alisema Mchengerwa.
Alisema kutokana na taarifa hiyo, kwa sasa idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko hilo imeongezeka kutoka watu 17 na kufikia 23.
Alisema taarifa hiyo pia imebainisha kuwa wananchi walioathirika na janga hilo, kwa sasa wanaendelea kupata huduma mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa miundombinu yao ambapo askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) takribani 96 wapo mkoani humo wakiendelea kulinda na kusaidia masuala ya usalama.
Akizungumzia mapendekezo ya kamati hiyo kwa serikali, Mchengerwa alisema imeitaka serikali kusimamia masuala ya afya na usalama kwa wananchi waliopatwa na tetemeko.
Aidha, alisema kamati hiyo imeishauri serikali iendelee kuratibu kwa kushirikiana na wahisani na kuhakikisha wanawatumia wataalamu wa ndani katika kufanya utafiti katika maeneo yenye bonde la ufa kabla ya maafa kutokea.
Pia kamati imeiomba serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya tetemeko na kujenga nyumba imara zinazostahimili mtikisiko, kuboresha kitengo cha maafa na kuanzisha vituo vya kitaifa vyenye vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majanga.
Akizungumzia serikali kuhamia Dodoma, alisema kamati hiyo imeishauri itungwe sheria maalumu itakayosisitizia jambo hilo na kuongeza nguvu katika kuisimamia Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) inayolalamikiwa kwa kuwa na urasimu mkubwa katika upangishaji wa ardhi.

0 comments:
Post a Comment