WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
amewataka wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania
kusimamia mapato kwa kukusanya fedha kinyume cha hapo atachomoa mmoja
mmoja na kuweka wengine kwa nusu saa tu.
Aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo, alisema kwa kuwa serikali inahitaji fedha, kama waziri hahitaji kuambiwa maneno mengi, kwani tofauti na hapo ataendelea kuwachomoa wajumbe hao mpaka apate kile anachokihitaji.
“Nahitaji pesa kwenye shirika. Ukiniambia maneno mengi mimi sijali, mimi nataka pesa, serikali inataka pesa, sitaki kitu kingine. Ni lazima msimamie mapato mkishindwa nachomoa mmoja mmoja. Naweza kufanya hivyo nusu saa tu. Nitaendelea kufanya hivyo mpaka nihakikishe Napata kile ninachokihitaji,” alisema Profesa Mbarawa.

0 comments:
Post a Comment