Biashara ya Simu za kisasa maarufu kama
Smartphone au Simu Janja imeendelea kukua na kuongeza ushindani wa
makampuni ya utengenezaji wa bidhaa hizo duniani kote. Leo October 26,
2016 mtu wangu nimeipata hii kuhusu nchi iliyofanya vizuri kwenye
biashara ya Smartphone duniani.
Ripoti
iliyotolewa na kampuni ya GFK ya Ujerumani inaonesha kuwa, mpaka kufikia
robo ya tatu ya mwaka huu, China imeongoza katika soko la simu za
smartphone na kuendelea kukua zaidi, huku ikiongeza msukumo mkubwa wa
ukuaji wa soko la simu hizo duniani.
Ripoti hiyo inasema simu milioni 353 aina
ya smartphone zimeshauzwa katika robo ya tatu ya mwaka huu duniani kote,
na idadi hiyo imetajwa kuongezeka kwa asilimia 7.5 kuliko mwaka 2015
kwa wakati kama huo, huku simu milioni 113 kati ya hizo zikiuzwa katika
soko la China pekee.
0 comments:
Post a Comment