TANZANIA imepiga marufuku uingizaji migomba na mazao yake kutoka
Msumbiji kwa kuwa nchi hiyo imekumbwa na ugonjwa unaoshambulia zao hilo
ambao kitaalamu unajulikana kwa jina la Panama Disease.
Haya yalisemwa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa wataalamu wa afya ya mimea kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) iliyosomwa na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia afya ya mimea katika wizara hiyo, Cornelius Mkondo.
Dk Turuka alisema katika kuhakikisha mazao ya migomba hayaingii nchini kutoka Msumbiji, Tanzania imeweka wataalamu wake wa mimea katika mipaka na nchi hiyo, viwanja vya ndege na maeneo yote muhimu ili kuimarisha ukaguzi.
Alisema ugonjwa huo haujaingia nchini, lakini tayari wamechukua tahadhari kwa kuzuia uingizwaji wa mazao ya migomba kutoka Msumbiji kwa kuwa ugonjwa huo ni hatari.
Mbali na ugonjwa huo, pia Tanzania kwa sasa haiwezi kusafirisha matunda kwenda Afrika Kusini kutokana na kuwepo mdudu hatari wa matunda.
Dk Turuka amewaambia washiriki wa mkutano huo unaoshirikisha nchi 15 za SADC na COMESA kuwa mkutano huo ni muhimu katika kupanga mikakati ya pamoja kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya mimea katika ukanda wa Afrika kwani magonjwa hayo katika sekta ya kilimo yanaathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji na uchumi wa nchi na wananchi wake na kusababisha kukosekana kwa uhakika wa usalama wa chakula na mazao.
Ugonjwa wa migomba huathiri uzalishaji kwa asilimia 70 katika nchi za SADC na husababisha hasara ya tani 1.52 za ndizi katika nchi hizo.
Pia alisema ugonjwa wa mahindi uliozikumba nchi za Afrika Mashariki ulitokea kuwa ugonjwa hatari na kuathiri zaidi uzalishaji wa mahindi na kutishia usalama wa chakula kwa kaya nyingi.

0 comments:
Post a Comment