Wednesday, 26 October 2016

al Hussein:chuki za makabila ni hatari Sudan Kusini

Kamishina wa juu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa Prince Zeid Ra'ad al Hussein ameonya kuwa kuzuka kwa kauli za chuki na uchochezi wa ghasia za kikabila nchini Sudan kunaweza kusababisha mauaji ya halaiki.
Hofu baina ya makabila makubwa Dinka, na yale ya kutoka ukanda wa ikweta imeongezeka kwa kasi katika wiki za hivi karibuni, baada ya shambulio la basi huko Dinka na kusababisha vifo vya watu kadhaa waliokuwa wakisafiri.
Umoja wa mataifa unasema kuwa una wasiwasi juu ya mashambulio hayo na kuhusu barua za kuogofya watu kutoka ukanda wa Ikweta inaonekana kuwa ni kulipiza kisasi.
Pia amesema kuwa ametilia maanani kauli iliyotolewa na Rais wa nchi hiyo Salva Kiir ambayo imetafsiriwa na wengi kama ina msukumo wa kikabila. Rais Kiir alisema yeye mwenyewe ataendesha operasheni ya kijeshi dhidi ya makundi ya waasi kuwajibika kwa mauaji katika eneo hilo.
Share:

0 comments:

nunua vitabu vya watoto kuanzia chekechekea mpaka darasa la saba

nunua vitabu vya watoto kuanzia chekechekea mpaka darasa la saba

Arquivo do blog