Katika
milima ya jimbo la Sichuan kusini magharibi mwa China, kundi la watoto
ambalo lilikuwa likishuka mita 800 kwenye mlima ili kufika shule huku
wakitumia njia za asili ambazo ni ngazi za miti ambayo ni hatari sasa
wanajengewa ngazi za chuma.
Ngazi
hiyo ya chuma inayojengwa na wanakijiji itakuwa na mabomba 1,500 ya
chuma na inatarajiwa kukamilika mwezi November mwaka huu, ujenzi wa
ngazi hizo zenye gharama ya dola za marekani 150,000 ambazo ni karibu
Tsh za kitanzania milioni 327, ilianza kujengwa na wanakijiji mwezi
August mwaka huu.
Ngazi
hiyo inatarajiwa kuwa na muundo imara zaidi pia inatarajiwa itakuwa
yenye usalama zaidi kwa hata wanakijiji wa kijiji hicho ambao watakuwa
wanaitumia kupanda na kushuka kila wiki kununua bidhaa mbalimbali na
kufanya biashara zao katika soko ambalo liko mbali na wanakoishi. Siku za nyuma wanakijiji walikuwa wakitumia miti ya mizabibu ambayo ilikuwa mibovu.
0 comments:
Post a Comment