“NIKIWA mwanamke nimeguswa na kundi la akina mama, kwani naamini
sehemu yoyote mwanamke ndiye anayezalisha mali, iwe sekta za viwandani
au kilimo. Sisemi kuwa wanaume hawazalishi hapana ila kuna utofauti
kwenye namna ya kuzalisha mali.
“Bado naweza kusema kuwa mwanamke ndiye anaweza kukomboa familia hasa kwa kuwa anaweza kufanya kazi yoyote ile na kwa muda wowote,” hiyo ni kauli ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe.
“Hebu tumuangalie mwanamke anaamka mapema katika nyumba na kuelekea kwenye kilimo, wakati huo atatumia nafasi hiyo pia kuchanja kuni na baadaye kuteka maji hivyo nalazimika kusema bado tunaweza kutamka ni nguvu kazi ya taifa na familia," anasema.
Munde ananukuu maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyewahi kusema kwamba eneo lolote ama taifa lenye maendeleo basi mwanamke aliwezeshwa na anamiliki uchumi. Tambwe anasema kauli hiyo ya Mwalimu Nyerere ndiyo iliyomsukuma, akaamua kuanza kuwapa mafunzo ya semina akina mama wajasiriamali wa jimbo la Tabora Mjini.
Anasema licha ya kuanza kuwasaidia nakina mama kwa mafunzo ya semina Tabora Mjini, amekuwa akiwawezesha akina mama wajasiriamali na vijana mkoa mzima tangu mwaka 2010.
Anasema amekuwa akifanya hivyo kwa kuungana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo mkoani Tabora (SIDO) kwa kujali zaidi wajasiriamali wadogo wadogo, kwani hali hiyo itakomboa kundi hili kwa kasi kikubwa.
Anasema tangu mwaka 2010 vipo vikundi ambavyo alivipa mafunzo na mitaji na sasa vikundi hivyo vimesimama imara na vina mitaji mikubwa na vingine ambavyo havikuzingatia maelekezo na mafunzo vilikufa. Anasema anaendesha semina ya mafunzo katika kata zote 29 za jimbo la Tabora Mjini na kila kata alikuwa akichukua takribani wajasiriamali 250 hadi 300.
Anafafanua kwamba alikuwa akitafuta walimu wenye ujuzi ili kufundisha vijana na akina mama wajasiriamali lakini kwa sasa ameamua kwanza kuanza na kina mama.
Munde anaeleza kipato kidogo cha akina mama na vijana ndiyo sababu hasa ilimsukuma ili mafunzo atakayowapatia anaamini atawavusha kutoka walipo na kuondokana na umasikini.
Aidha anasema anaamini makundi haya ndiyo nguvu kazi ya taifa na kwamba wakiwezeshwa kwenye mafunzo na kupatiwa mitaji watafika mbali kimaisha na kutoa mchango wa kiuchumi kwa taifa.
Anasema akina mama wengi kiuchumi ni wanyonge na hivyo anaungana na Rais John Magufuli kutetea wanyonge kwa vitendo kwa kuwawezesha ili waweze kuchangia uchumi wa taifa na kukuza mitaji na kusaidia familia zao kufikia mkakati wa Tanzania ya viwanda.
Anasema mafunzo aliyoendesha katika kata 29 yalilenga kuwapatia ujuzi akina mama ambapo jumla ya waliopewa mafunzo hayo ni 8,700 kwa mujibu wa mahudhurio na kwamba yalimgharimu Sh milioni 23. Munde anabainisha aina ya mafunzo kwa vitendo waliyopata akina mama hao ni utengenezaji wa batiki, utengenezaji mishumaaa, utengenezaji sabuni ngumu na za maji, utengenezaji shampoo, usindikaji mazao na utengenezaji mafuta.
Mafunzo mengine waliyopata ni ufumaji mashuka, ufumaji vitambaa, utengenezaji achali, tomato sauce (nyana za mezani), chili (pilipili), vitafunwa vitokanavyo na zao la muhogo, utunzaji wa vitabu vya hesabu, namna ya kusajili vikundi na namna ya kuweka na kukopa.
Kuhusu kundi la vijana anasema kwa kuwa wameshapatiwa mafunzo sasa anakuja kuwawezesha kifedha ili waweze kutunisha mitaji ama kazi za uzalishaji watakazoanzisha.
Ili kutekeleza azma yake, mbunge huyo alikabidhi fedha taslimu kwa wajasiliamali akina mama kwa kata zote 29 sh milioni 14.5 ambapo kila kikundi kilipokea sh 500,000 taslimu kama mtaji watakaoanzia.
Tambwe anasema pamoja na msaada huo bado anajipanga kwa kuanza mchakato wa kuunganisha vikundi anavyoviwezesha hatkmaye viweze kuunganishwa na Baraza la Taifa la Uwekezaji nchini kuelekea Tanzania ya viwanda.
Anasema baraza hilo litasaidia vikundi hivi kusaidiwa kwenye maeneo kadhaa ili viweze kuyafikia malengo yao na kujikwamua kiuchumi na kwamba ana imani vikundi vitaleta mageuzi ya kweli.
Anatoa mwito kwa vikundi vote vilivyopata mafunzo na mitaji kutumia mafunzo na mitaji hiyo ili kufikia malengo waliyojiwekea hususani kujikwamua kiuchumi.
Zinduna Abdallah, mkazi wa Tambuka Reli anasema yeye ni mmoja wa wanufaika na hivyo anatoa wito kwa wajasiriamali mkoani Tabora kuweka nia ya dhati ya kujiendeleza kiuchumi kwa fedha hizo na mafunzo waliopata. Aziza Bakari Said wa kata ya Ikomwa anasema kikundi chao cha Tupendane walipokea Sh 500,000 kama mtaji na wamejipanga kuzitumia ipasavyo ili kuondokana na umasikini.

0 comments:
Post a Comment