MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) imesema
inayatambua malalamiko ya fidia ya wakazi wa Kurasini wilayani Temeke,
wanaopaswa kuhama kupisha mradi mkubwa wa mtambo wa kuchakata maji taka
na unayafanyia kazi.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Sais Kyejo, alisema suala hilo linafahamika, na mamlaka hiyo itashirikiana na walalamikaji kutafuta ufumbuzi wake, ikiwa ni pamoja na kufanya uhakiki upya.
Kyejo alisema eneo hilo, lina mabwawa makubwa mawili, na kwamba wapo watu waliolipwa tangu mwaka 2004, wengine walihakikiwa 2009 na wakarudiwa kuhakikiwa mwaka 2015 na kulipwa.
“Eneo kubwa ni mtambo mkubwa wa kuchakata maji taka na eneo hilo lina mlolongo mrefu maana Dawasa ilishalipa mara kadhaa. Tutapitia upya malalamiko yao kuona msingi wake na namna ya kuyatatua kabla mradi kuanza,” alisema Kyejo bila kueleza kazi hiyo itaanza lini.
Mwishoni mwa wiki, wakazi wa eneo hilo wapatao 70 kupitia Mwenyekiti wao Dismas Chilongo na Katibu, Boniface Chacha, walifika katika ofisi za gazeti hili, kulalamika kuwa Dawasa inawataka wahame katika maeneo yao bila kuwalipa fidia wapishe mradi huo.
Chilongo alisema wamekuwa njia panda, wasijue cha kufanya kwa miaka zaidi ya 10 baada ya Dawasa kukaa kimya na hawajui hatima yao pamoja na kwamba wamekuwa tayari walipwe wapishe mradi huo. Walimuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kuingilia kati suala hilo.
Naye Chacha alisema wao wapo tayari kuondoka kwani wanatambua juhudi za serikali katika kuleta maendeleo, lakini kwa kuwa walijaza fomu namba 69 ya fidia, Dawasa inapaswa iwalipe ili waondoke.
Kwa mujibu wa wananchi hao, mwaka 2003 wakiwa 116 walijaza fomu namba 69 ya kudai fidia ya makazi wa ardhi kama Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 inavyoelekeza na badala ya kulipwa fidia, Dawasa iliwalipa kifuta jasho mwaka 2004.
Hata hivyo alisema wenzao 46 walilipwa na tayari wameondoka. Aidha, barua ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliyotolewa kwa niaba yake na Mthamini Mkuu, Mei 23 mwaka 2006 iliitaka Dawasa kufafanua upana wa ukanda wa ardhi inayozunguka mradi wa maji machafu kutokana na kubadilika ukubwa na pia kuwataka wawalipe fidia wahusika.
“Wananchi waliolipwa kifuta jasho ni wale tu waliokuwa na mimea ya mazao, nyumba zote zilizokuwa ndani ya ukanda, hazikulipwa fidia, hivyo, iwapo Dawasa inaona ni vyema nyumba hizo zibomolewe ili kuacha ukanda wazi kisheria, wananchi hao wanastahili kulipwa fidia,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.

0 comments:
Post a Comment