MKUU wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewaasa warembo wanaoshiriki shindano la Mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania-2016),
kutambua wana jukumu zito mbele yao la kuzisaidia jamii zao katika majukumu mbali mbali ya kijamii.
Mongella alitoa kauli hiyo muda mfupi mara baada ya warembo 30 wanaoshiriki shindano hilo kumtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha.
Mongella aliwataka warembo hao kufanyakazi kwa bidii na kujituma kwani ndio njia pekee itakayowawezesha kuondokana na umasikini.
“Jijengeeni tabia yakufanyakazi kwa bidii na maarifa tena bila kuchoka, hii awamu ya tano ni awamu ya hapa kazi tuu, hivyo kama warembo mnalo jukumu zito la kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais katika kufanya kazi na hasa katika kazi za kijamii, lakini haya yote yatawezekana mkiwa wadilifu na wachapa kazi, sasa hivi mpo kwenye U miss wewe pambana na jenga tabia yakufanya kazi masuala ya nani atakuwa mshindi waachie majaji, alisema Mongella.
Katika hatua nyingine Mongella amewashauri warembo hao kuto ionea haya Lugha ya Taifa ya Kiswahili, k wakuwa fikra sahihi huja kwa lugha sahihi, amewataka kuinze Lugha hiyo wakati wa mashindano hasa pale wanapotakiwa kujieleza ili kuweza kufikisha ujumbe kwa jamii kwa wepesi.
Akizungumza kabla yakumkaribisha mkuu wa mkoa wa Mwanza, mmoja wa waratibu wa Mashindano hayo Bibi Pamella Irengo, amesema, wamefurahi sana kama mkoa wa Mwanza kuyapokea mashindano hayo, kwani hii ni mara ya kwanza mashindano hayo yatafanyika nje ya mkoa wa Dar es salaam.
“Mhe. Mkuu wa Mkoa mashindano haya kwa miaka 21, yamekuwa yakifanyika Mkoa wa Dar es salaam, hivyo kuyaleta Mwanza sisi kwetu ni fursa ya kipekee katika kuutangaza mkoa wetu lakini tunashukuru sana uongozi wa mkoa kwakutuunga mkono nakutupokea kwa moyo mkunjufu.
Mashindano ya kumsaka Mrembo wa Tanzania yatafanyika Oktoba, 29, 2016 katika Ukumbi wa Rock City Mall, ambapo warembo wapatao thelasini (30), watachuana kumsaka mrembo mmoja atakaye peperusha Bendera ya Taifa katika mashindano ya Dunia na Kauli mbiu ya mashindano hayo kwa Mwaka huu ni
“Mrembo na Mazingira safi”.

0 comments:
Post a Comment