Ajali
za Barabarani zimekuwa zikipoteza maisha ya wananchi wengi kila siku
huku wengine kupata ulemavu wa kudumu. Leo October 25, 2016 Serikali
kupitia kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Eng. Hamad Masaudi imetoa
mkakati ili kupunguza ajali hizo.
Naibu
Waziri Eng. Hamad Masauni amesema kuwa mkakati huo utahusikana na
kuchukua hatua kali kwa askari ambao watahusika na masuala ya ukaguzi
wa vyombo vya usafiri, madereva pamoja na wamiliki wa magari
yatakayohusika kwenye ajali.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri Masauni amezitaja wilaya za Ilala na Kinondoni kuwa zinaongoza kwa ajali nchi Tanzania.
Ayo TV
inakuletea taarifa kamili ya Naibu Waziri Hamad Masauni wakati
akizungumzia mikakati ya Serikali juu ya ajali za Barabarani.
0 comments:
Post a Comment