SERIKALI imezindua mpango maalumu kitaifa wa kuboresha afya
ujulikanao kama Mkoba wa siku 1,000 utakaotumika kutekeleza afua
mbalimbali za lishe nchini kwa lengo la kupunguza udumavu kwa watoto na
upungufu wa damu kwa wajawazito na wanyonyeshao.
Mkoba wa siku 1,000 ni nyenzo ya uwezeshaji unaotumia njia mbalimbali za mawasiliano yenye lengo la kushawishi mabadiliko ya tabia na mitazamo kuhusu lishe katika jamii, ukihamasisha wajibu wa kijinsia wa wazazi na walezi walio ndani ya siku 1,000 za mwanzo wa maisha ya mwanadamu ambazo zinahesabiwa tangu mimba inapokuwa imetungwa hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili.
Akizindua mpango huo jana jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk Zainab Chaula alisema Mkoba wa siku 1,000 utaasiliwa na serikali kama Mkoba Maalumu wa Kitaifa.
Alisema mpango uliotengenezwa na mradi wa lishe wa Mwanzo Bora kwa kushirikiana na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) ulifanya kazi katika mikoa sita nchini ambao umesaidia pia kupunguza tatizo la udumavu.
Kuhusu udumavu, Dk Chaula alisema ni jambo lililopo lisiloonekana ingawaje ni hatari likiwa tishio kijamii, kiuchumi na likihitaji kufanyiwa kazi na kupatikana kwa suluhu.
Alisema serikali imejipanga kuratibu juhudi zilizofanywa na wadau katika kupambana na aina yoyote ya udumavu nchini.
Alisema Mkoba wa siku 1,000 utatumiwa na wadau mbalimbali kama maofisa lishe wa wilaya na mikoa, wahudumu wa afya katika jamii ili kuchochea tabia chanya zinazolenga kupunguza tatizo la upungufu wa damu kwa wajawazito na wanaonyonyesha na udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka miwili.
Alisema msisitizo umewekwa katika kuboresha matendo na majukumu katika jamii ambayo ni muhimu sana katika kupunguza matatizo ya lishe kwa akina mama na watoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dk Joyceline Kaganda alisema Mkoba wa siku 1,000 una vyumba sita kila kimoja kikiwa na alama maalumu ya utambulisho, kila chumba kimehifadhiwa machapisho mbalimbali yenye jumbe zinazohamasisha matendo na tabia chanya za lishe katika kila hatua ya maendeleo ya ukuaji wa mtoto.

2 comments:
habari, nahitaji kupata huu mkoba wa siku 1000, nitaupataje? Jane kutoka singida
INGIA KWENYE WIZARA YA AFYA
Post a Comment