FUNGU HAPA KUPATA MATOK...
Thursday, 27 October 2016
UTOAJI WA MIKOPO KWA WANAFUNZI MWAKA 2016/2017
Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183
wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika
mwongozo wa utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na
kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni
pamoja na:
I. Vipaumbele vya kitaifa vinavyoendana na Mpango wa Maendeleo wa
Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mafunzo...
Majibu ya Meya Kinondoni kwa wanaohoji uwepo wa Dk. Tulia na Ndalichako

October 23 2016 baraza la halmashauri ya manispaa ya Kinondoni, Dar es salaam lilitangaza ushindi wa nafasi ya umeya kwa Benjamin Sitta ambaye alipigiwa kura na baadhi ya wajumbe.
Lakini moja ya headline zilizochukua
nafasi kubwa kuanzia kwanye mitandao ya kijamii hadi magazetini ni
uhalali wa uchaguzi huo kuwa haukuwa wa haki baada ya kuonekana ushiriki
wa Naibu spika Dk. Tulia pamoja na Waziri Ndalichako.
meya huyo ambaye anashare...
Baada ya Mchungaji Lwakatare kuwatoa wafungwa DSM, sasa ni zamu ya Dodoma

Ikiwa
siku kadhaa zimepita tangu Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto
Mikocheni B, Dk. Getrude Lwakatare kutoa milioni 25 kwa ajili ya
kuwalipia wafungwa 78 ambao walikosa fedha za kulipia faini na kufungwa
jela mkoa wa Dar es salaam. Sasa amejitolea kuwalipia faini wafungwa
50 walioko kwenye magereza mkoani DODOMA, wakiwemo wanaonyonyesha, wazee
na watoto.
Akizungumza na Ayo Tv na millardayo.com, Lwakatare amesema...
Mabadiliko ya Yanga na Simba yapigwa stop na serikali

Serikali imezipiga stop klabu za Yanga na Simba kuendelea na
michakato yao ya kubadili umiliki wake hadi pale yatakapofanyika
marekebisho ya katiba zao.
Hayo yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la
Taifa (BMT), Mohamed Kiganja alipozungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam.
Hivi karibuni klabu hizo kongwe ziliazimia kuingia kwenye mabadiliko,
Yanga ikikodishwa na mwenyekiti wake Yusuf Manji na Simba ikitaka...
Model anayedaiwa kutoka kimapenzi na Wema na kudai hamjui Idris Sultan anyoosha maelezo

Wiki moja iliyopita kupitia kipindi kimoja cha runinga, model huyo alisema hamjui Idris Sultan.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Calisah alisema ni kweli kwamba
hamjui Idris Sultan na wala hakuongea kwa nia mbaya au kutafuta kiki.
“Mimi nashangaa kwanini watu wamepanic kisa kusema simjui Idris
Sultan, kwani yeye ni nani kila mtu amjue?,” aliuliza Model huyo. “Wewe
kuna wanamichezo wangapi wameshachukua tuzo kubwa duniani hawajui?.
Kwahiyo mimi...
Dayna Nyange: Lebo yoyote itakayokubali masharti yangu nitafanya nayo kazi

Hitmaker huyo wa ‘Komela’ amemuambia mtangazaji wa Maisha FM ya
Dodoma, Silver Touchez “Kikubwa nachoangalia ni sababu, kabla sijajiunga
na lebo yoyote lazima niwe na vitu vyangu ambavyo navitaka na wao
wanavitu vyao wanavyotaka.”
“Record label ni studio tu ambao watu watakuwa wanasimamia kazi zangu
ni kitu ambacho mimi mwenyewe ninaweza nikaenda sehemu yoyote nikafanya
kazi zangu. Kuna vitu vingi sana kabla hujaingia kwenye lebo yoyote
kama...
Man Utd kukutana na West Ham robo fainali EFL Cup

Mechi za robo fainali EFL Cup ratiba imetoka baada ya kumuondoa Guardiola, Mourinho sasa atacheza na Bilic.
Mechi hizi zitachezwa katika wiki inayoanza Tarehe 28,Novemba.
Hii ndo ratiba kamili ya Michuano ya EFL Cup.
...
‘Magufuli ameletea msiba Dodoma’

WAKATI serikali ya awamu ya tano ikiendelea na hekaheka za kuhamishia
makao makuu yake mkoani Dodoma, baadhi ya wakazi wa mkoa huo wamelaani
hatua hiyo ya serikali na kusema inawasababishia matatizo makubwa,
Wakizungumza na mtandao huu, wakazi wa Ndachi
kata ya Miyuji, Manispaa ya Dodoma, wamesema baada ya serikali kutangaza
kuhamishia makao makuu yake Dodoma, tayari wameanza kuporwa ardhi yao.
Wameenda mbali zaidi na kutishia kuwakata...
RC MWANZA APOKEA UJUMBE WA WAWEKEZAJI KUTOKA KOREA.
Awaahidi ushirikiano.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amepokea ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini,
wenye niya yakuwekeza katika mkoa wa Mwanza ukiwa na ujumbe wa watu kumi na watano nakufanya nao mazungumzo mapema
katika Ofisi yake kabla yakuendelea na ziara yao katika Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
Katika mazungumzo yao yaliyodumu saa 1:33, Mkuu wa Mkoa amewahakikishia utayari
wa mkoa wa Mwanza kuwapokea wawekezaji kutoka nchini humo
lakini pia kuwabainishia maeneo mbali mbali katika sekta ya...
RC MWANZA ATOA SOMO KWA WAREMBO MISS TANZANIA. 2016
MKUU wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewaasa warembo wanaoshiriki shindano la Mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania-2016),
kutambua wana jukumu zito mbele yao la kuzisaidia jamii zao katika majukumu mbali mbali ya kijamii.
Mongella alitoa kauli hiyo muda mfupi mara baada ya warembo 30 wanaoshiriki shindano
hilo kumtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha.
Mongella aliwataka warembo hao kufanyakazi kwa bidii na kujituma kwani
ndio njia pekee itakayowawezesha kuondokana na umasikini.
“Jijengeeni tabia...
Ofisa usalama feki atupwa jela miaka 2
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemhukumu Seleman Manoti, kifungo cha
miaka miwili jela kwa kupatikana na hatia ya kujifanya usalama wa Taifa.
Hata hivyo, mahakama imetoa hukumu hiyo bila mshitakiwa kuwepo
mahakamani kutokana na kuruka dhamana kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa.
Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Flora Haule alisema kuwa
upande wa mashitaka, ulileta mashahidi wanne kwa ajili ya kuthibitisha
tuhuma hizo.
Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa, mahakama imeridhishwa na
ushahidi huo na kwamba mahakama inamtia hatiani mshitakiwa...
TFS yanasa lori lenye shehena ya mbao

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wamekamata lori lililokuwa
likisafirisha mbao zilizovunwa kinyume cha sheria baada ya kupata
taarifa kutoka kwa wasamaria.
Lori hilo lenye namba za usajili T 676ANQ aina ya Scania lililokuwa
likitoka Kigoma kwenda jijini Dar es Salaam, lilikutwa limetelekezwa
katika maegesho ya mkazi wa Dar es Salaam, eneo la Amana katika Manispaa
ya Ilala na dereva wa lori hilo kutokomea kusikojulikana.
Hata hivyo,...
Kiini cha nauli juu Dar-Zanzibar chaelezwa

TATIZO la uhaba wa vyombo vya usafiri kati ya Zanzibar na Tanzania
Bara ikiwemo boti zinazokwenda kwa kasi, kwa kiasi kikubwa kumechangia
kuwepo kwa tatizo la ulanguzi wa tiketi kwa abiria na kusababisha
usumbufu mkubwa.
Ulanguzi wa tiketi hizo umeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Ujenzi na Uchukuzi, Mohammed Ahmada wakati alipofanya ziara katika eneo
la bandari ya Malindi.
Tiketi moja ya boti zinazokwenda kwa kasi zinazomilikiwa...
Serikali yazindua mpango maalumu kuboresha afya
SERIKALI imezindua mpango maalumu kitaifa wa kuboresha afya
ujulikanao kama Mkoba wa siku 1,000 utakaotumika kutekeleza afua
mbalimbali za lishe nchini kwa lengo la kupunguza udumavu kwa watoto na
upungufu wa damu kwa wajawazito na wanyonyeshao.
Mkoba wa siku 1,000 ni nyenzo ya uwezeshaji unaotumia njia mbalimbali
za mawasiliano yenye lengo la kushawishi mabadiliko ya tabia na
mitazamo kuhusu lishe katika jamii, ukihamasisha wajibu wa kijinsia wa
wazazi na walezi walio ndani ya siku 1,000 za mwanzo wa maisha ya
mwanadamu ambazo zinahesabiwa...
Wanaosomea fani za kipaumbele wapewe mikataba
TAARIFA kwamba serikali inakusudia kuweka utaratibu wa kuwabana
wanafunzi wanaopewa mikopo katika fani za kipaumbele, kutumikia utumishi
wa umma kwa muda fulani, haina budi kuungwa mkono na kila mpenda
maendeleo ya kweli.
Fani ambazo serikali kwa makusudi imezipa kipaumbele kwa lengo la
kupata wataalamu wa kutosha katika maeneo husika, ambayo kwa sasa yana
wataalamu wachache ni pamoja na fani za sayansi ya tiba na afya, ualimu
wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta,
gesi asilia, sayansi asilia, mabadiliko...
Polisi yawashikilia wanne mtandao wizi wa magari

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu wanne kwa
tuhuma za wizi wa magari kwa kununua nyaraka za magari yaliyopata ajali
na kulipwa na bima.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi, Simon Sirro
alisema jana Dar es Salaam kuwa askari waliwakamata watuhumiwa hao baada
ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
“Watuhumiwa hawa wanajihusisha na wizi wa magari kwa mbinu ya kununua
nyaraka za magari yaliyopata ajali...
Pluijm aziita timu zinazomtaka

KOCHA Hans van Pluijm amesema milango iko wazi kwa timu yoyote inayomhitaji.
Kocha huyo Mholanzi alitangaza kujiuzulu juzi baada ya waajiri wake
Yanga kuingia mkataba na kocha wa Zesco ya Zambia, George Lwandamina
bila kumshirikisha.
Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm alikiri timu kadhaa kumwania
lakini akasema ni mapema kuzitaja na kusisitiza amefungua milango kwa
yeyote inayomtaka kumfuata kwa mazungumzo.
“Muhimu siwezi kukaa bila...
Serikali yazipiga stop Yanga, Simba

SERIKALI imezipiga stop klabu za Yanga na Simba kuendelea na
michakato yao ya kubadili umiliki wake hadi pale yatakapofanyika
marekebisho ya katiba zao.
Hayo yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la
Taifa (BMT), Mohamed Kiganja alipozungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam.
Hivi karibuni klabu hizo kongwe ziliazimia kuingia kwenye mabadiliko,
Yanga ikikodishwa na mwenyekiti wake Yusuf Manji na Simba ikitaka...
Mbarawa awataka Posta kukusanya mapato

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
amewataka wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania
kusimamia mapato kwa kukusanya fedha kinyume cha hapo atachomoa mmoja
mmoja na kuweka wengine kwa nusu saa tu.
Aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo, alisema kwa kuwa serikali inahitaji fedha, kama
waziri hahitaji kuambiwa maneno...
Historia MOI upasuaji kwa wenye kibiongo
KIBIONGO ni tatizo la kupinda kwa mgongo upande moja hasa wa kulia,
hali inayomfanya mtu aliye na hali hiyo kutembea akiwa ama ameinama au
kujikunja. Tatizo hilo mtu huweza kuzaliwa nalo au kutokea baadaye mtoto
anapokuwa amefikisha umri wa miaka mitatu na kuendelea.
Kwa kuwa hapa nchini kulikuwa hakuna upasuaji kwa tatizo hilo, watu
waliokuwa na shida hiyo walikuwa wakikua nalo hivyo hivyo isipokuwa
wenye uwezo wa kifedha na kuwa na taarifa sahihi walipelekwa nje ya nchi
kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji. Hivi sasa ufumbuzi umepatikana...
Mfumo wa PReM utakavyodhibiti wanafunzi hewa

TANGU serikali iliporuhusu mazingira ya soko huria katika sekta ya
elimu, kumekuwapo na shule binafsi nyingi. Katika shule hizo binafsi,
suala la kuhamisha wanafunzi limekuwa halizingatiwi kama ilivyokuwa
miaka ya nyumba ambapo ilikuwa ni lazima taarifa za mwanafunzi za kuhama
zipate baraka na mamlaka za elimu katika ngazi za kata, wilaya na mkoa
na taarifa kubaki katika ngazi hizo.
Kukatika kwa mnyororo huo ulifanywa uhamishaji na taarifa...
Yanga siku 5 bao kumi

ANGA siku tano bao 10! ndivyo ilivyotokea jana baada ya mabingwa hao
watetezi wa Ligi Kuu kushinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu na hivyo kuwa
na mabao 10 ndani ya siku tano baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 6-2
Jumamosi iliyopita.
Ushindi huo uliopatikana kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam
umeifanya Yanga kuendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na
pointi 24, tofauti ya pointi tano na vinara wa ligi hiyo, Simba. Katika
...
Kagera yatumia mil. 800/- ukarabati miundombinu

UKARABATI wa miundombinu iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi mkoani
Kagera umeanza, na tayari Sh milioni 800 zimetumika kati ya Sh bilioni
tano zilizotolewa na wadau mbalimbali katika kuwachangia waathirika wa
tetemeko hilo lililotokea Sept 10, mwaka huu na kusababisha vifo,
uharibifu wa majengo na miundombinu mbalimbali.
Aidha, imeelezwa kuwa, inahitaji miaka miwili au mitatu kwa mkoa huo
kurejea katika hali ya kawaida kutokana na maeneo...
Wa-Baha’i kufanya sherehe kubwa
JUMUIYA wa Baha’i ya jijini Dar es Salaam itaungana na Wa-Baha’i
wengine duniani, kuadhimisha kuzaliwa kwa waanzilishi wa imani yao ya
Baha’i, Bab na Baha’u’llah, Novemba mosi na 2, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwakilishi wa Mawasiliano
wa Baraza la Kiroho la Baha’i Dar es Salaam, Qudsiyeh Roy, maadhimisho
ya kuzaliwa Bab ambaye ni Mtume Mtangulizi wa imani ya Baha’i,
yatafanyika Novemba mosi na sherehe ya kuzaliwa kwa Baha’u’llah ambaye
ni Mtume Mwanzilishi wa imani hiyo itafanyika Novemba 2.
Maadhimisho hayo...
Wachina mbaroni kwa kumteka mwenzao

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia raia wawili wa
China kwa tuhuma za kumteka nyara Mchina mwenzao, Liu Hong (48) ambaye
ni mfanyakazi wa Le Grande Cassino, wakidai kulipwa Dola za Marekani
19,000 (zaidi ya Sh milioni 38).
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda
wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi, Simon Sirro alisema walipokea
taarifa kwamba raia huyo wa China alitekwa nyara na watu wasiofahamika.
Alisema...
Wednesday, 26 October 2016
Vyuo vikuu waanza kupata mikopo

AKAUNTI za wanafunzi wa vikuu nchini zitakuwa zimeanza kunona baada
ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kusema kuanzia
jana imeanza kuingiza fedha za wanafunzi wote wa elimu ya juu ambao
wamekidhi vigezo vya kupatiwa mikopo.
Wanafunzi 20,183 kati ya wanafunzi 58,010 ambao wamedahiliwa na Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ndio ambao wamepangiwa kupata mikopo na
bodi hiyo baada ya kutimiza vigezo vyote vilivyowekwa.
“Napenda...
NSSF hatarini ‘kulizwa’ bil 270/-
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekiri mbele ya Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa linaweza kupoteza kiasi cha Sh
bilioni 270, zilizoingizwa kwenye mradi wa ubia baina yake na Kampuni
ya Azimio Housing Estates (AHEL), kama shirika hilo lisipokuwa makini.
Pamoja na hayo, kamati hiyo baada ya kubaini madudu kadhaa katika
hesabu za shirika hilo, imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), kufanya...
U HEARD: Alichoongea H Baba kuhusu nyumba walizopost Alikiba na Diamond

Jana
October 25, 2016 kwenye mtandao wa Instagram kulikuwa na majibizano ya
mashabiki wa mastaa wakubwa wa muziki wa Bongo Flava Tanzania
nawazungumzia Diamond Platinumz na Alikiba hukua akiwepo mtu wa kati H
Baba ambaye pia aliwahi kutofautiana na Diamond Platinumz siku za nyuma
na sababu ikitajwa na kuwa waliibiana nyimbo studio.
Kupitia
account ya Instagram ya Diamond Platinumz jana alipost picha akiwa
kwenye nyumba yake anayodai kuwa...
Kiwango cha Pesa utatakiwa kulipa Ili upate Collabo na msanii Akothee

Kama
ilivyo ahadi yangu kwako, ni kuhakikisha haipitwi na story yoyote mtu
wangu na leo nimeipata hii kutoka kwa msanii wa muziki kutoka
Kenya, Akothee. Inawezekana wengi wetu tunafahamu tu kwamba ni msanii na
labda kwasababu ana historia ya kuwa na pesa nyingi basi hata muziki
anaufanya tu kama starehe.
Kwa mujibu
wa Citizen, taarifa hii ikufikie kama ni msanii na unahitaji kufanya
collabo na Akothee basi unatakiwa kuandaa mfuko...
China imeshikilia rekodi hii ya dunia kwenye biashara ya Smartphone!!

Biashara ya Simu za kisasa maarufu kama
Smartphone au Simu Janja imeendelea kukua na kuongeza ushindani wa
makampuni ya utengenezaji wa bidhaa hizo duniani kote. Leo October 26,
2016 mtu wangu nimeipata hii kuhusu nchi iliyofanya vizuri kwenye
biashara ya Smartphone duniani.
Ripoti
iliyotolewa na kampuni ya GFK ya Ujerumani inaonesha kuwa, mpaka kufikia
robo ya tatu ya mwaka huu, China imeongoza katika soko la simu za
smartphone na kuendelea...