Thursday 3 November 2016

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA NNE, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu Waombaji wote walioomba kudahiliwa katika kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) na Umma kwa ujumla kuwa dirisha la maombi lilifungwa mnamo tarehe 15 Oktoba 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya nne kwa waombaji wa kozi hizo.

Uteuzi wa awamu ya nne kwa waombaji wa Astashahada na Stashahada unatarajiwa kutangazwa mnamo tarehe 2 Novemba 2016, hivyo basi waombaji wanaombwa kuwa na subira ili kutoa muda kwa Baraza kukamilisha taratibu za uteuzi huo.

Maombi mapya ya Udahili:

Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) utafunguliwa tena tarehe 2 Novemba 2016 hadi tarehe 6 Novemba 2016 ilikujaza nafasi za udahili zilizobaki wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya nne. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuweza kuomba hapo awali.

Maombi ya Uhamisho:

Mwombaji aliyechaguliwa ataweza kuomba uhamisho kutoka chuo ama kozi moja kwenda nyingine kupitia kwenye ukurasa wake binafsi (profile) tu. Uhamisho huu utategemea nafasi zilizopo, ushindani na alama za chini za kujiunga na kozi (cut-off). Orodha ya Vyuo na Programu zenye nafasi inapatikana hapa

Hatua za kuomba uhamisho:

1. Ingia kwenye ukurasa wako binafsi (profile) kwa kutumia jina la mtumiaji (Username) na neno la siri (Password) ulivyopewa wakati wa usajili
2. Bofya kitufe kilichoandikwa “Transfer Request/Kuomba Uhamisho”, na punde ukurasa utafunguka
3. Utafunguka ukurasa unaokuonesha chuo na kozi uliyochaguliwa awali
4. Chagua kada unayohitaji kuhamia
5. Chagua chuo unachohitaji kuhamia
6. Chagua kozi unayohitaji kuhamia
7. Mfumo utatathmini kama una sifa za kujiunga na kozi uliyochagua. Iwapo una sifa za kujiunga na kozi hiyo mfumo utakuomba ulipie Sh. 30,000/- kama ada ya maombi ya uhamisho. Kiasi hiki hakitarudishwa (non-refundable)
8. Bofya kitufe kilichoandikwa “Confirm Transfer Request/Kamilisha Maombi”.
9. Utapewa muhtasari wa maombi yako ya uhamisho pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye namba ya simu ya mkononi uliyoweka wakati wa usajili na barua pepe kukujulisha kwamba umekamilisha maombi.

Jinsi ya kulipia (Malipo ya tafanywa kwa M - pesa tu):

1. Piga *150*00#
2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa
3. Chagua 4. Weka namba ya kampuni
4. Tafadhali weka namba ya kampuni (No. 607070)
5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (No. 1234)
6. Weka kiasi (e.g. 30,000/=)
7. Weka namba ya siri
8. Bonyeza 1 kuthibitisha.

Angalizo (Disclaimer):

1. Kuhama chuo na kozi si lazima.
2. Uhamisho utafanyika kwa kozi zile tu zenye nafasi na kwa vyuo ambavyo bado havijafunguliwa na kuanza masomo.
3. Uhamisho ni kwa wale waombaji waliokwisha kuchaguliwa kupitia mfumo wa pamoja wa udahili tu.
4. Maombi ya uhamisho yanaweza kufanyika MARA MOJA na kwa kozi moja
5. Iwapo umefanikiwa kupata uhamisho, majibu yataonekana kwenye ukurasa wako binafsi (Profile). Majibu haya pia yatatumwa kwenye namba yako ya simu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupitia barua pepe baada ya tarehe ya mwisho ya maombi (6 Novemba 2016).
6. Uhamisho utategemea ufaulu wa waombaji na nafasi zilizopo. Hii inamaanisha kwamba wenye ufaulu wa juu ndio wenye uwezo mkubwa wa kukubaliwa kuhama.
7. Maombi yatakayotumwa kwa barua au barua pepe hayatoshughulikiwa.
8. Waombaji waliomba uhamisho na kukosa awamu iliyopita wataruhusiwa kuomba tena bila malipo mapya.

Imetolewana
Ofisiya Katibu Mtendaji
Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Tarehe: 1 Novemba, 2016
Share:

Wednesday 2 November 2016

Mke wa Lema aunganishwa kesi ya kumtusi RC Arusha

MKE wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, Neema Lema (33) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kuunganishwa katika kesi ya mume wake ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuwa ni shoga.
Akimsomea mashitaka hayo kwa mara ya kwanza, Wakili wa Serikali, Blandina Msawa mbele ya Hakimu Augustino Rwezile, alidai kuwa kati ya Agosti 20, mwaka huu ndani ya Arusha, Neema ambaye ni mkazi wa Njiro alimtumia ujumbe wa simu ya kiganjani mkuu huyo wa mkoa wenye lugha ya matusi, huku akijua ni kosa kisheria.
Alidai mtuhumiwa huyo alituma ujumbe kutoka namba 0764 150 747 na 0756 551 918 kwenda namba 0766 757 575 uliokuwa ukidai, “Karibu, tutakudhibiti kama Uarabuni wanavyodhibiti mashoga.”
Mshitakiwa alikana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana hadi Novemba 15, mwaka huu itakapotajwa tena kesi hiyo.
Share:

DC ataka Mwalimu Mkuu Mwananyamala kushushwa cheo

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Aron Kagurumjuli kumshusha cheo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwananyamala B, Emmanuel Temba kwa makosa mbalimbali, ikiwemo kufanya biashara shuleni.
Akitoa agizo hilo katika ziara ya kutembelea kata za manispaa hiyo jana, Hapi alisema ametoa adhabu hiyo kwa kosa la kufanya biashara ya vibanda shuleni hapo wakati agizo la serikali lililotolewa mwaka 2006, haliruhusu biashara shuleni.
‘’Huyu mwalimu mkuu wa shule hii, hatufai haiwezekani afanye biashara ya vibanda shuleni wakati serikali ilishakataza huku akiwaruhusu wafanyabiashara kutumia vyoo vya watoto wetu wanaosoma hapa, na kuagiza mkurugenzi mvue cheo huyu mwalimu,” alisema Hapi.
Aidha, Hapi alisema kosa lingine linalomkabili Temba ni kuruhusu wafanyabiashara wa vibanda hivyo kutumia vyoo vya wanafunzi vilivyopo shuleni hapo, ikiwa ni pamoja kuweka kituo cha kuuza mafuta ya taa katika eneo la shule. Hapi alitoa agizo hilo huku mwalimu mkuu huyo akiwa hayupo shuleni hapo, na taarifa zilidai alienda kwenye msiba wa kaka yake.
Mkuu huyo wa wilaya alitembelea pia Soko la Mwananyamala Kisiwani ambako aliagiza ujenzi wa soko hilo uliosimama kwa muda mrefu uanze.
“Hili soko haiwezekani fedha zimeshatolewa na Halmashauri, lakini ujenzi mpaka leo haujaisha, nawapa wiki mbili ujenzi uanze mara moja,” alisema.
Share:

Watumishi changamkieni ununuzi wa nyumba-RC

WATUMISHI wa umma wameshauriwa kuchangamkia fursa ya kununua nyumba zilizojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) kabla ya muda wa kustaafu ili kujitengenezea maisha mazuri baada ya kustaafu.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati alipotembelea nyumba za watumishi zilizojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) zilizopo eneo la Bunju na nyumba za wananchi Magomeni Kota.
Makonda alisema watumishi wengi amekuwa wakiishi maisha ya tabu baada ya kustaafu kutokana na kutojipanga kabla ya kustaafu na gharama za maisha kupanda, lakini kupitia ujenzi wa nyumba hizi wanaweza kupata nyumba hizo kwa gharama nafuu.
“Tumeona hapa kuna nyumba za kima cha chini cha shilingi milioni 38 unaweza ukajipanga ukakopa nyumba na kulipa taratibu hata pale utakapostaafu unakuwa na nyumba yako na familia yako na kuishi bila tabu,” alisema Makonda.
Share:

Tanzania yaipa somo ICC kukabili mpasuko

WAKATI nchi kadhaa za Afrika zikionesha dalili za kutaka kujiengua kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), Tanzania imeishauri mahakama hiyo kukaa meza moja na nchi wanachama wa Mkataba wa Roma, hasa za Afrika ili kutafuta suluhu ya changamoto na tofauti zilizopo kati ya mahakama hiyo na wanachama wake.
Imetoa mwito huo mwanzoni mwa wiki hii kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa (UN), Balozi Tuvako Manongi wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipopokea na kujadili taarifa ya utendaji wa ICC. Alisema uwepo au kuanzishwa kwa ICC kulitokana kwa kiasi kikubwa na uungwaji mkono kutoka nchi za Afrika.
Alisema uungwaji mkono huo ulisababishwa na namna nchi hizo za Afrika zilivyokatishwa tamaa na kuvunjika moyo baada ya kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.
“Baada ya kukatishwa tamaa na kuvunjwa moyo, mahakama hii, ilikuja kuwa chombo cha kutenda haki dhidi ya watu waliojihusisha na vitendo vya kikatili vikiwamo vya ukatili dhidi ya binadamu, uhalifu wa kivita na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu,” alisema Balozi Manongi.
Alisema kutokana na madhara makubwa yasiyoelezeka yaliyotokea Afrika yaliifanya mahakama hiyo kuwa chombo cha matumaini dhidi ya wale ambao hawakuweza kuguswa au walikuwa juu ya sheria.
“Tanzania inatambua kuwa uhusiano kati ya mahakama hii na Afrika ni ule wa misuguano, na ni uhusiano ambao umeleta hofu ya Afrika kujitoa,” alisema na kuongeza kuwa hofu hiyo ya kujitoa kwa Afrika katika mahakama hiyo, haipaswi kuwepo kutokana na mambo kadhaa ambayo Afrika imejipanga kuyatekeleza kwa manufaa ya bara hilo na watu wake.
Aliyataja mambo hayo kuwa ni utekelezaji wa ajenda ya Maendeleo ya Umoja wa Afrika maarufu kama agenda 2063 ambayo pamoja na mambo mengine inachagiza katika utawala bora, demokrasia, usawa wa jinsia, kuheshimu haki za binadamu, haki na utawala wa sheria.
“Viongozi wa wakuu wa nchi na serikali wa Afrika wameutangaza mwaka 2016 kuwa mwaka wa haki za binadamu huku mkazo ukielekezwa katika haki za wanawake. Na katika kutambua kuwa Amani na Haki ni vitu visivyoweza kutenganishwa, kwa sababu hizo, tunachotakiwa kuhimiza leo sana sana ni majadiliano,” alisisitiza.
Pamoja na hayo, Tanzania imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kutopeleka ICC rufaa zenye mlengo wa kisiasa, kwani kwa kufanya hivyo kunachangia kuharibu sifa ya ICC na kuifanya isiaminiwe na kuonekana inatumiwa na wakubwa kutimiza malengo yao.
Taarifa ya ICC iliwasilishwa na Rais wa mahakama hiyo, Jaji Silvia Fernandez de Gurmendi katika kipindi ambacho Jumuiya ya Kimataifa imekumbwa na taharuki baada ya wanachama wawili Afrika Kusini na Burundi kuwasilisha rasmi UN kusudio la kujiondoa huku Gambia nayo ikitangaza kutaka kujitoa ingawa haijawasilisha rasmi nia yake hiyo.
Share:

Shein ahimiza mikutano ya watendaji kutatua kero

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein ameeleza umuhimu wa viongozi katika Ofisi na Idara za Serikali kuwa na utaratibu wa kufanya mikutano mara kwa mara na watendaji wao ili kuzungumza na kujadili masuala yao ya kazi.
Dk Shein aliyasema kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kujua matatizo ya watendaji wao pamoja na kukaa kwa pamoja kwa lengo la kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizopo kwa haraka na hatimae kuweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Aliyasema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar katika kikao maalumu kati yake na uongozi wa Ofisi ya Rais, na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, wakati ilipowasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha Julai hadi Septemba katika Bajeti ya mwaka 2016-2017 ya ofisi hiyo.
Katika maelezo yake, alisema ni jukumu kwa kila mkuu wa Idara kuwa na utaratibu huo kwani utasaidia kwa kiasi kikubwa kupata maamuzi ya haraka sambamba na kuweza kufanya kazi kwa pamoja hatua ambayo pia, hupunguza mivutano na hujenga mafahamiano makubwa.
Aidha, alieleza kuwa kukaa pamoja kati ya kiongozi na watendaji wake kunasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia muwafaka katika kujadili masuala mbali mbali ya kiutendaji hali ambayo huzidisha mshikamano na kujenga udugu miongoni mwao.
Aidha, alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa uongozi na watendaji wote wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa utendaji wao wa kazi sambamba na kazi nzuri ya uwasilishaji na utekelezaji wa Mpango Kazi uliofanywa na Ofisi hiyo.
Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi Gavu akisoma taarifa ya Mpango Kazi wa Ofisi hiyo, na kusema kuwa Ofisi ya Rais imedhamiria kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar ili waishi kwa amani, mshikamano na upendo miongoni mwao.
Share:

Songwe wakamata mbegu feki za mahindi

POLISI katika Mkoa wa Songwe wamekamata kilogramu 455 za mbegu zinazoaminika kuwa feki za mahindi katika msako mkali unaoendelea kwa ushirikiano na Kampuni ya Mbegu ya Pana.
Kadhalika, watu watano wanashikiliwa na Polisi kutokana na kujihusisha na biashara hiyo ya kuuza mbegu hizo na uchunguzi dhidi yao unaendelea kufanyika.
Miongoni mwa maeneo ambayo msako umeendeshwa ni Mji Mdogo wa Mlowo wilayani Mbozi ambako ndiko zimekamatwa mbegu hizo za mahindi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Songwe, Mkuu wa mkoa huo, Chiku Galawa amebainisha hayo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana baada ya kukamatwa kwa mbegu hizo feki kuwa serikali mkoani hapa imejipanga kuhakikisha wauzaji pembejeo feki wote wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwaumiza wakulima.
Hata hivyo, Galawa aliwataka wananchi kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi la polisi ili kuwafichua watu wanaojihusisha na biashara hiyo ili wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwani wanachangia kudidimiza mapato ya mkulima kwa asilimia 80.
Share:

Uvuvi haramu ‘huyeyusha’ matumbawe

MAKAMU wa Rais mstaafu, Dk Mohammed Gharib Bilal ameonya kuwa uvuvi wa haramu unaofanywa na wavuvi katika maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi unatishia kutoweka kwa matumbawe, jambo ambalo lina madhara makubwa ya kimazingira kwa nchi.
Akitoa mhadhara katika kongamano la mazingira na mabadiliko ya tabianchi lililoandaliwa na kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Bilal alisema kitendo cha kuendesha uvuvi haramu kunaharibu matumbawe ambayo yana umuhimu makubwa katika fukwe na viumbe vingine vya baharini.
Dk Bilal alisema kama hatua za haraka hazitachukuliwa kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia baruti, janga kubwa la kimazingira litatokea na hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi na ustawi wa jamii, kwa vile matumbawe hivi sasa yana faida kubwa katika nyanja hizo.
Katika mhadhara wake, Dk Bilal alisema uchafuzi wa mazingira kwa sasa unatisha kutokana na watu wengi kutaka kutumia vyanzo vya mapato kwa kuharibu mazingira, hivyo akasema kuna haja ya wadau wote kuunganisha nguvu kukomesha athari za uhabirifu wa mazingira.
“Natoa mwito kwa wananchi wote, wawe wasikivu kwa ushauri unaotolewa na wataalamu wetu wa Mazingira, tusipochukua tahadhari ya kutunza mazingira vizazi vijavyo vitapata shida,” alisema Dk Bilal na kusisitiza kuwa uvuvi huo haramu unakimbiza samaki, lakini pia unaathiri maisha ya watu ambao uchumi wao unategemea rasilimali za baharini.
Katika hotuba yake, pia makamu huyo wa rais mstaafu alitaka kukomeshwa ukataji wa mikoko kwani kufanya hivyo kunatishia uhai wa miti hiyo ambayo huzuia kasi ya maji ya bahari kuvamia nchi kavu. Alisisitiza kuwa ukataji wa mikoko una athari kubwa kwa nchi kwani unasababisha mafuriko na mmonyoko wa udongo katika maeneo ya pwani ya bahari.
Kongamano hilo la siku tano linahusisha washiriki kutoka nchi mbalimbali ambao wanajadili namna ambavyo Afrika inaweza kupambana na athari za mabadiliko ya nchi. Kongamano hilo lilifunguliwa juzi na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ambaye alitaka wananchi wakomeshe vitendo vya uharibifu wa mazingira.
Share:

Mashali kuagwa Leaders leo

MWILI wa bondia wa ndondi za kulipwa nchini, Thomas Mashali aliyeuawa Kimara jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumatatu, utazikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni.
Baba mzazi wa marehemu, Malifedha Mashali alisema kuwa mwili wa mtoto wake huyo aliyeuawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana, utazikwa katika makaburi ya Kinondoni Mwembejini.
Alisema mipango mingine ya mahali utakapoagiwa mwili huo na utakapoombewa, bado ilikuwa inaendelea na alikuwa hajajua shughuli hizo zitafanyikia wapi.
Mzee Mashali alisema kuwa mwili wa mtoto wake utaagwa katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni kuanzia saa 4:30 asubuhi kabla ya kwenda kulazwa katika nyumba yake ya mileleni katika makaburi ya Kinondoni mapema mchana.
Mashali alikuwa akishikilia mikanda ya WBO na UBO kabla ya kifo chake, ambapo amekufa huku akiacha mataji kibao ya ngumi ya hapa nchini na yale ya kimataifa.
Wadau wengi wa michezo walitoa masikitiko yao kuhusu kifo hicho cha Mashali huku wengi wao wakisema kuwa bondia huyo alikuwa na kipaji cha aina yake katika ndondi.
Mashali alizaliwa Dar es Salaam mwaka 1989 na alianza kupigana ngumi za kulipwa Novemba 27, 2009 alipopigana na kumtwanga Hamadu Mwalimu katika pambano lililofanyika katika ukumbi wa Texas, Manzese
Share:

MNH wakusanya bil 4.6/- kwa mwezi

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imekuwa ikikusanya mapato ya Sh bilioni 4.6 kwa mwezi kuanzia Desemba mwaka jana hadi kufikia Oktoba mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 100.
Fedha ni zaidi ya wastani wa Sh bilioni 2.3 ilizokuwa ikizalishwa na hospitali hiyo kwa kipindi kama hicho kuanzia Dasemba 2014 hadi Oktoba 2015.
Sambamba na ongezeko hilo, pia huduma za vipimo vya MRI, CT –Scan, X-Ray na Ultra Sound zimeongezeka ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja sasa, jumla ya wagonjwa waliopimwa kwa kutumia vipimo hivyo wamefikia 55,073 ukilinganisha na kipindi kama mwaka uliopita ambapo wagonjwa waliopimwa walikuwa 23,989.
Akitoa taarifa ya mafanikio ya mwaka mmoja madarakani ya Serikali ya Awamu ya Tano jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma cha hospitali hiyo, Aminiel Eligaesha alisema hivi sasa mwelekeo wa mapato ya MNH kuanzia Julai 2016 hadi Oktoba 2016 unaonesha hospitali hiyo imezalisha Sh bilioni 4.6 kwa mwezi na kusema hayo ni mafanikio makubwa kuwahi kupatikana katika kipindi kifupi cha miezi miwili.
“Tumeona hospitali ina fursa ya kuzalisha kiasi kingi cha fedha na hivyo kuweza kujitosheleza kwa kiwango kikubwa katika uendeshaji wa shughuli zake kutokana na mwelekeo wa mapato yalivyo,” alisema Eligaesha.
Alisema mafanikio hayo yamechangiwa na uboreshwaji wa huduma hospitalini hapo pamoja na kazi ya usimamizi wa wafanyakazi na kupunguza kero za wafanyakazi hospitali hapo kwa sababu wameongeza morali ya kazi hasa baada ya kero na matatizo yao kupatiwa ufumbuzi.
Aliyataja maboresho hayo kuwa ni kuunganisha mashine za CT Scan, X-Ray na MRI katika mtandao wa Tehama katika kuhakikisha huduma zote zinazofanyika katika idara hiyo zinaonekana.
Aidha, pia kupata idadi ya wagonjwa waliofanya vipimo na kulinganisha kiasi cha mapato kilichokusanywa kama kinaendana na picha zilizofanyika kwenye mashine hizo.
Akizungumzia huduma za vipimo vya MRI, Eligaesha alisema Novemba 9, mwaka jana ikiwa ni siku nne baada ya Rais John Magufuli kuapishwa, alifanya ziara katika hospitali hiyo na kukutana na changamoto ikiwemo kuharibika kwa MRI na mashine nyingine za X-Ray na kutoa maagizo kwa uongozi wa hospitali kuhakikisha mashine hizo zinatengenezwa ndani ya siku 14.
Alisema maagizo hayo yalitekelezwa na hivi sasa mashine zote zinafanya kazi vizuri na kwa kipindi cha Desemba 2015 hadi Oktoba 25,mwaka huu jumla ya wagonjwa 17,951 wamepimwa kwa kutumia mashine ya MRI, ukilinganisha na wagonjwa 1,911 waliopima kwa kipindi cha Desemba 2014 hadi Oktoba 2015.
Akizungumzia huduma ya CTScan, Eligaesha alisema masheni hiyo ilitengenezwa na hivi sasa inaendelea kufanya kazi vizuri ambapo kwa kipindi cha Desemba 2015 hadi Oktoba 2016 wagonjwa 10,259 wamepimwa ukilinganisha na wagonjwa 3,319 waliopimwa Desemba 2014 hadi Oktoba 2015.
Kuhusu upatikanaji wa dawa, alisema wagonjwa wanapata dawa za zaidi ya asilimia 96 kutoka kwenye maduka ya dawa ya hospitalini na kuwa wameboresha mfumo wa Tehama kwenye utoaji na uagizaji dawa.
Share:

Serikali kutumia trilioni 32.9/- mwaka 2017/2018


SERIKALI imepanga kutumia Sh trilioni 32.946 katika bajeti yake ya mwaka 2017/2018, ikiwa imeongezeka kutoka Sh trilioni 29.5 ya mwaka 2016/2017 na kutaja maeneo ya kipaumbele kuwa ni pamoja na kuzingatia miradi ya kufufua kiwanda cha General Tyre cha Arusha na kuendeleza maeneo ya viwanda vidogo.
Sambamba na hilo, serikali imebainisha mikakati yake ya kudhibiti matumizi, ambapo sasa itahakikisha mikataba inayoingiwa na serikali na taasisi zake inakuwa katika shilingi za Tanzania, isipokuwa kwa mikataba inayohusisha biashara za kimataifa.
Kuhusu kuhamishia shughuli za makao makuu ya serikali Dodoma, mipango ya ujenzi wa majengo na miundombinu yote ya serikali iliyopangwa kujengwa Dar es Salaam, itahamishiwa Dodoma.
Akiwasilisha bungeni jana mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka 2017/2018, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema kati ya Sh trilioni 32.946, Sh trilioni 19.782 zitatengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
“Sh trilioni 7.206 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa serikali na taasisi za umma na Sh trilioni 9.723 ni kwa ajili ya kulipia deni la Taifa lililoiva. Matumizi ya maendeleo yatakuwa Sh trilioni 13.164 sawa na asilimia 40 ya bajeti yote ambapo fedha za ndani ni Sh 9.960 sawa na asilimia 76. Kiwango hiki ni ongezeko la Sh trilioni 1.343 ikilinganishwa na mwaka 2016/2017,” alifafanua.
Alisema mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Sh trilioni 20.872 sawa na asilimia 63 ya mahitaji yote.
Kati ya mapato hayo serikali inatarajia kukusanya mapato ya kodi ya Sh trilioni 18.097 sawa na asilimia 87 ya mapato ya ndani.
Hata hivyo, alisema kiasi hicho ni makisio ya awali ambapo makisio ya mwisho yatapatikana baada ya kukamilika kwa tathmini ya nusu mwaka 2016/2017 pamoja na taarifa ya kikosi kazi cha maboresho ya kodi, kinachojumuisha wadau mbalimbali wakiwemo sekta binafsi na washirika wa maendeleo.
Akizungumzia jinsi ya kudhibiti matumizi ya serikali, Dk Mpango alisema serikali itaendelea kupunguza gharama na matumizi yasiyokuwa ya lazima ikiwemo sherehe za kitaifa, posho za vikao, uchapishaji wa fulana, kofia, mikoba, safari za nje, mafunzo ya muda mfupi nje nchi na ununuzi wa samani kutoka nje.
Pia kutoa kipaumbele kwa taasisi za umma na zile ambazo serikali inamiliki hisa katika kununua huduma kama vile bima, huduma za fedha, usafirishaji wa barua, wavuti, simu, mizigo na vifurushi, matangazo na usafiri.
Waziri alitaja mikakati mingine ni kudhibiti utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Vyuo vikuu kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi waliokidhi vigezo pekee ndio wananufaika na mikopo hiyo na kudhibiti ulipaji mishahara kwa watumishi wanaostahili pekee.
Vilevile kutumia utaratibu wa ununuzi wa nyumba kwa utaratibu wa kulipia kwa awamu hususan kwa majengo ya balozi na wawakilishi walioko nje ya nchi, badala ya kupanga na kudhibiti safari za nje ya nchi na ukubwa wa misafara.
Katika kufanikisha ukusanyaji mapato, waziri huyo aliwataka maofisa masuuli wote nchini kuweka mazingira wezeshi katika kufanikisha hilo kwa kuingia mikataba na wazabuni na makandarasi na watoa huduma wanaotumia mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFDs) na kuimarisha ukaguzi na usimamizi wa vituo vya ukusanyaji mapato kama bandari, mipakani na viwanja vya ndege.
Dk Mpango alisema maofisa hao, pia wanaagizwa kufanya mapitio ya mikataba yote iliyopewa misamaha ya kodi ili kutathmini faida zake na kujipanga upya, ambapo pia kutoingia mikataba inayohusisha misamaha ya kodi bila idhini ya Waziri wa Fedha na Mipango.
Baadhi ya maeneo ya vipaumbele vya bajeti ya mwaka 2017/2018 alivyotaja Dk Mpango ni miradi ya kukuza viwanda na uchumi ikiwamo miradi ya magadi Soda kwenye bonde la Engaruka, kukifufua kiwanda cha General Tyre, uendelezaji wa eneo la viwanda vidogo(Sido) katika mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha.
Pia bandari kavu mkoani Pwani, bomba la mafuta kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga pamoja na mradi ya makaa ya mawe Mchuchuma, chuma cha Liganga na ujenzi wa Reli ya Kati kutoka Dar es Salaam –Tabora- Kigoma kwa standard gauge na matawi yake.
Share:

Vyuo vikuu 15 kitanzini

SERIKALI imetoa siku mbili kwa vyuo vikuu 15, kuwasilisha matokeo ya mitihani kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ya wanafunzi wanufaika na mikopo wanaoendelea na masomo ili kupangiwa mikopo kwa mwaka wa 2016/2017.
Vyuo hivyo vilivyokuwa viwasilishe matokeo hayo siku 30 kabla ya kufunguliwa, vimepewa siku hizo kuanzia jana, kabla serikali haijachukua hatua zozote.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Maimuna Tarishi alisema hayo jana, alipotembelea ofisi za Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Alisema serikali iko katika hatua za mwisho za upangaji na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo.
Tarishi alisema baadhi ya vyuo vimeshindwa kuwasilisha matokeo ya mitihani kwa wanafunzi wanaoendelea ili wapangiwe mikopo kwa mwaka unaoendelea, kwani utaratibu lazima vyuo kuwasilisha matokeo kuonesha wanafunzi wangapi wana sifa za kuendelea kupewa mikopo.
“Mikopo haiwezi kutolewa tu kwa kila mwanafunzi, hata kama ameamua kuacha masomo, hivyo vyuo vina wajibu wa kuthibitisha kuwa wanafunzi wanaowaleta bado ni wanafunzi sahihi na wanaendelea na masomo,” alisema Katibu Mkuu huyo.
Alivitaja vyuo ambavyo havijawasilisha matokeo hayo kuwa ni Vyuo vya Elimu ya Biashara (CBE) Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma, Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UOB), Chuo Kikuu cha St. John Kituo cha St Mark Dar es Salaam (SJUTDSM), Chuo cha St. John Tanzania (SJUT) na Chuo Kikuu cha Tumaini Mbeya (TUMAMBEYA).
Vingine ni Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI), Chuo cha United African University of Tanzania (UAUT), Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu Cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha Tiba ya Sayansi (STJCAHS), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Kituo cha Makambako na Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU).
Katibu Mkuu huyo pia alitaka vyuo hivyo kuimarisha mifumo yao ya kuandaa na kuwasilisha matokeo ya mitihani kwa wakati na kwa ukamilifu katika siku zijazo ili kuondoa usumbufu. Akizungumzia hatua watakazochukua wasipotimiza agizo hilo, alisema wanawaagiza kutekeleza maagizo hayo kwa siku walizopewa.
Alisema ana uhakika kauli hiyo inawatosha waungwana hao, kutimiza wajibu wao.
Awali vyuo vyote vya elimu ya juu, vilikumbushwa umuhimu wa kuwasilisha matokeo, kabla havijafunguliwa, ikiwemo serikali kufanya mkutano na Makamu Wakuu wa vyuo vyote vya elimu ya juu mkoani Dodoma na kusisitiza umuhimu wa vyuo kuwasilisha matokeo na nyaraka nyingine muhimu, kabla ya vyuo kufunguliwa.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano, imejipanga kikamilifu na imetenga fedha za kutosha na tayari imetoa Sh bilioni 80.89 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi, wanaonufaika na mikopo hiyo kwa robo ya kwanza ya mwaka.
Alisema kati ya kiasi hicho, tayari Sh bilioni 45.2 zimekwishalipwa na kiasi kilichosalia, kitalipwa kwa vyuo baada ya kupokea matokeo kikamilifu. Pia aliwatoa wasiwasi wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliokosa mikopo, kupeleka malalamiko katika dirisha maalum la malalamiko, lililofunguliwa na Bodi ya Mikopo kuanzia juzi na serikali ni sikivu, itafanyia kazi.
Katika siku za hivi karibuni, wanafunzi wa elimu ya juu katika vyuo mbalimbali wanaoendelea na masomo, wamekuwa wakilalamika kucheleweshwa kwa mikopo ya elimu ya juu ; huku wanaoanza mwaka wa kwanza, wakilalamikia kukosa mikopo hiyo.
Imeelezwa kuwa baada ya kufanyika uchambuzi, wanafunzi 20,183 wanaoanza mwaka wa kwanza katika vyuo mbalimbali wamepatiwa mikopo; huku wakitarajia kutoa mikopo kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama amesema serikali kwa sasa inaandaa taarifa kuhusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu; na ikishakamilika itawasilisha bungeni, kama walivyoomba wabunge.
Alitoa ufafanuzi huo baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga kujibu mwongozo uliotolewa na Mbunge wa Mwibara, Kange Lugola (CCM) kuomba mwongozo bungeni, akitaka leo serikali ilete taarifa kuhusu mikopo inayotolewa na Bodi ya Mikopo, kwa kile alichoeleza kuwa wanafunzi wengi walioomba mikopo wakiwa na vigezo, hawajapata. Jenista alisema kwa sasa serikali inaandaa taarifa hiyo na ikikamilika, italetwa bungeni kama wabunge walivyoomba.
Akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema Serikali itadhibiti utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi waliokidhi vigezo pekee, ndio wananufaika kwa mikopo hiyo.
Awali, Mhagama alisema serikali haifanyi kazi kwa miujiza, bali kwa kutumia mgangilio wa bajeti iliyowekwa na uthibitisho kwamba serikali inafanya kazi kwa mipango, imeweza kutekeleza kutoa elimu bure ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Mhagama alitoa kauli hiyo baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Free Mbowe (Chadema) kuuliza swali la nyongeza lililotokana na swali la msingi la Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele (CCM) kutaka kujua Serikali itaanza kutekeleza lini ahadi ya Sh milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa ili kutatua tatizo la ajira na mitaji kwa vijana na akina mama.
Akifafanua zaidi, alisema kamwe serikali haijiendeshi kwa miujiza bali kwa kutumia mipango iliyojiwekea katika bajeti zake.
“Kuthibitisha jambo hili linatekelezeka, Serikali ya CCM kupitia Ilani yake tumeweza kutoa elimu bure, kuwashangaza Watanzania miradi mikubwa mbalimbali imetekelezwa ikiwemo kununua ndege (mbili za Dash 8, Q400 zilizotengenezwa na Bombardier), Ilani inatekelezwa kwa mambo mengi mbalimbali,” alisema akimjibu swali la nyongeza Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) kuhusu Sh milioni 50 zilizoahidiwa kwa kila kijiji nchini.
Jenista alisema fedha zote zinazoahidiwa na serikali zikiwemo Sh milioni 50, zitatolewa na Watanzania watazipata.
Share:

Wapinzani wapinga takwimu ukuaji uchumi

LICHA ya takwimu za hivi karibuni kuonesha uchumi wa Taifa pamoja na Pato la Taifa vimekuwa vikikua kwa kasi na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zenye uchumi imara, kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imedai kuwa uchumi wa Tanzania umeyumba.
Kambi hiyo imetaja baadhi ya maeneo yanayothibitisha hilo kuwa ni mikopo inayotolewa na benki za biashara kwenye sekta binafsi kuwa imeshuka katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016.
Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Halima Mdee alisema mikopo hiyo imefikia Sh bilioni 1,167.2 ikilinganishwa na ongezeko la Sh bilioni 1,577.5 la mwaka 2015 katika kipindi kama hicho.
“Hii maana yake sekta binafsi imekosa Sh bilioni 410.3 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016. Hali hii imefanya mzunguko wa sarafu na noti mikononi mwa watu kushuka kutoka asilimia 188.8 Desemba 2015 na kufikia asilimia 6.7 Julai mwaka 2016,” alieleza.
Alisema kwa mujibu wa taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), amana za wateja katika benki zilipungua kutoka Sh trilioni 20.52 Desemba 2015 hadi kufikia Sh trilioni 20.24 Juni mwaka 2016.
Akichangia mapendekezo ya mpango huo wa maendeleo, Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda (CCM) alisema takwimu zinaonesha asilimia 53 ya viwanda vikubwa nchini vipo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Kagera na Arusha, uwiano ambao si mzuri na kutaka viwanda viwepo kwenye mikoa mingine pia.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), Dk Albina Chuwa, katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka huu, Pato la Taifa limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 7.9 ikilinganishwa na asilimia 5.8 ya robo ya pili ya mwaka jana.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu alisema ukuaji wa Pato la Taifa katika nusu ya kwanza ya mwaka ya Januari hadi Juni, umeongezeka na kufikia asilimia 6.7 kutoka asilimia 5.7 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2015.
Share:

Lowassa aongoza vigogo Chadema kuzuru bungeni


VIONGOZI wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwemo aliyekuwa mgombea wa urais wa chama hicho, Edward Lowassa jana walitembelea bungeni mjini hapa.
Lowassa ambaye pia amewahi kuwa Waziri Mkuu, alifika jana saa 2:40 katika viwanja vya Bunge na kutumia dakika kadhaa kusalimiana na baadhi ya wabunge nje ya ukumbi kabla hajaingia ndani.
Alipoulizwa na gazeti hili kuhusu ujio wake bungeni, Lowassa, aliyekuwa Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM kwa takribani miaka 20 hadi mwaka jana alipohamia Chadema, alisema yupo Dodoma kwa shughuli za chama chake. “Nimekuja kwa ziara, nikishatambulishwa huko ndani, nitaongea si sasa,” alisema Lowassa aliyepokewa na wabunge wa vyama mbalimbali, wakimsalimia na wengine wakimsindikiza katika lango la kuingilia katika ukumbi wa Bunge kufuatilia shughuli za Bunge la 11.
Baadhi ya wabunge aliozungumza nao ni pamoja na Mbunge wa Newala, George Mkuchika (CCM) ambaye alimsalimia na kumkaribisha bungeni, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema), wa Kilolo, Venance Mwamoto (CCM), wa Bukoba Mjini, Wilfred Rwakatare (Chadema).
Baada ya kuzungumza naye kwa muda mfupi, walionekana wakijumuika wote kumsindikiza katika lango kuu la Bunge kuingia bungeni.
Ndani ya Ukumbi wa Bunge, baada ya kipindi cha maswali na majibu, Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge, Najma Giga, akitambulisha wageni, alimtambulisha Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Lowassa kuwa ni wageni wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe.
Mbali na Lowassa na Sumaye, wageni wengine wa Mbowe walikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Profesa Abdallah Safari na Mjumbe mwingine wa Kamati Kuu, Arcado Ntagazwa.
Hata hivyo, baada ya Lowassa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, wabunge wengi walisalimiana naye bila kujali itikadi zao za vyama na wengine walionekana kuteta kwa muda mrefu.
Wageni wengine waliofika na kutambulishwa ni pamoja na Rais mstaafu wa Bunge la Afrika, Getrude Mongella ambaye wabunge wa CCM walimshangilia kwa nguvu zote huku wa upinzani nao wakimshangilia pamoja na Balozi wa Rwanda nchini.
Share:

Thursday 27 October 2016

UTOAJI WA MIKOPO KWA WANAFUNZI MWAKA 2016/2017

Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa  utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na:
 I. Vipaumbele vya  kitaifa vinavyoendana na Mpango  wa Maendeleo  wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya  Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji  ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;
• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa  Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
i. Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji  maalum kama vile ulemavu na uyatima
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o Wadahiliwa yatima waliopata mkopo                                                 873
o Wadahiliwa wenye ulemavu wa  viungo                                             118
o Wadahiliwa  wahitaji wenye  mzazi mmoja                                      3,448
o Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali                     87
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma  kozi  za kipaumbele                      6,159
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine                                  9,867
Jumla                                                                                             20,183
Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.
Hatua zinazofuata
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.
IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Share:

Majibu ya Meya Kinondoni kwa wanaohoji uwepo wa Dk. Tulia na Ndalichako

Share:

Baada ya Mchungaji Lwakatare kuwatoa wafungwa DSM, sasa ni zamu ya Dodoma


Ikiwa siku kadhaa zimepita tangu Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B, Dk. Getrude Lwakatare kutoa milioni 25 kwa ajili ya kuwalipia wafungwa 78 ambao walikosa fedha za kulipia faini na kufungwa jela mkoa wa Dar es salaam.  Sasa amejitolea kuwalipia faini wafungwa 50 walioko kwenye magereza mkoani DODOMA, wakiwemo wanaonyonyesha, wazee na watoto.
Akizungumza na Ayo Tv na millardayo.com, Lwakatare amesema …..>>>‘Siku ya ijumaa itakuwa kwa ajili ya Dodoma tumefanikiwa kuwalipia faini za watu wenye makosa madogo madogo ya elfu hamsini, ya laki na nusu kwa watu wapatao 50 na tulitoa kipaumbele kwa watu wanaonyonyesha watoto, wagonjwa, wazee vikongwe, wale watu ukiwalipia unapata thawabu kwa Mungu’
Share:

Mabadiliko ya Yanga na Simba yapigwa stop na serikali

Serikali imezipiga stop klabu za Yanga na Simba kuendelea na michakato yao ya kubadili umiliki wake hadi pale yatakapofanyika marekebisho ya katiba zao.
YangaSimba
Hayo yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni klabu hizo kongwe ziliazimia kuingia kwenye mabadiliko, Yanga ikikodishwa na mwenyekiti wake Yusuf Manji na Simba ikitaka kuuza hisa asilimia 51 kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’.
Kiganja alisema Serikali haikatai mabadiliko ya uendeshaji katika klabu hizo pamoja na nyingine za wanachama, ila inachotaka kwanza kufanyike marekebisho ya katiba zao kwani za sasa haziruhusu mabadiliko hayo.
Alisema kuwa BMT inapenda kuona wahusika wanafuata sheria na taratibu za nchi katika kufikia malengo yao, ambapo alisisitiza kuwa kuendelea na michakato hiyo kabla ya kurekebisha katiba zao ni kosa na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
“Hivi karibuni kumeibuka michakato ya watu wakitaka kubadilisha umiliki wa klabu za wanachama na kuzielekeza katika utaratibu wa hisa na ukodishwaji, vitendo vimesababisha migogoro mikubwa ambayo inaashiria uvunjifu wa amani…,” alisema.
Kiganja alisema tayari mezani kwake kuna barua nyingi za wanachama wa Yanga wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato huo wa kubadilisha umiliki.
Kwa mujibu wa katiba ya Yanga iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 Ibara ya 56 inaeleza kuhusu kampuni ya umma: Inaeleza kuwa kutakuwa na kampuni itakayojulikana kama Young African Sports Corporation Limited ambayo itasajiliwa chini ya sheria ya makampuni kama kampuni ya umma yenye hisa.
Sehemu ya pili ya ibara hiyo inasema wanachama wote katika klabu ambao katika tarehe ya marekebisho ya Katiba ya mwaka 2007 wako hai kwa nguvu ya uanachama wao watakuwa wanahisa katika kampuni kwa kiwango cha idadi ya hisa watakapopata kwa mujibu wa muafaka wa Yanga uliofikiwa na wana Yanga Juni 22, 2006.
Klabu itamiliki hisa zilizosawa na asilimia 51 ya hisa zote zilizomo katika klabu hiyo. Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utachagua wanachama wawili, ambao sio miongoni mwa viongozi wa klabu kuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni kwa ajili ya kuwakilisha maslahi ya klabu kwenye kampuni.
Tayari Yanga iko chini ya Kampuni ya Yanga Yetu ambayo ni mali ya mwenyekiti wa klabu hiyo Manji, ikiwa ni kinyume na katiba yao wenyewe.
Kiganja alisisitiza kuwa klabu zisitishe mipango ya kubadilisha uendeshaji na ziendelee kuwa mali ya wanachama. Wakati Yanga walikuwa tayari wameishaingia mkataba wa miaka 10 wa
kuikodisha klabu yao, wenzao wa Simba walijipa miezi sita kukamilisha taratibu za kuuza hisa.
Share:

Model anayedaiwa kutoka kimapenzi na Wema na kudai hamjui Idris Sultan anyoosha maelezo

Wiki moja iliyopita kupitia kipindi kimoja cha runinga, model huyo alisema hamjui Idris Sultan.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Calisah alisema ni kweli kwamba hamjui Idris Sultan na wala hakuongea kwa nia mbaya au kutafuta kiki.
“Mimi nashangaa kwanini watu wamepanic kisa kusema simjui Idris Sultan, kwani yeye ni nani kila mtu amjue?,” aliuliza Model huyo. “Wewe kuna wanamichezo wangapi wameshachukua tuzo kubwa duniani hawajui?. Kwahiyo mimi nadhani watu ambao wananishambulia katika mitandao hawajui nini wanafanya,”
Aliongeza,”Sikusema hivyo kuonyesha dharau, kwa sababu nipo karibu na Wema lakini hajawai kuniambia kuhusu mtu kama huyo na sijawahi kumuona naye, na kama ukiwa na mwanamke halafu akawa azungumzia mwanaume mwingine hizo ni dharau sana. Kwahiyo kiukweli mimi jamaa nimeanza kumjua baada ya watu kinitag picha zake katika mitandao ya kijamii,”
Pia model huyo alisema kwa sasa hawezi kuweka wazi kama ni kweli anatoka kimapenzi na Wema Sepetu huku akidai Wema ndiye atayekuwa na jibu sahihi juu yake.
Share:

Dayna Nyange: Lebo yoyote itakayokubali masharti yangu nitafanya nayo kazi

Hitmaker huyo wa ‘Komela’ amemuambia mtangazaji wa Maisha FM ya Dodoma, Silver Touchez “Kikubwa nachoangalia ni sababu, kabla sijajiunga na lebo yoyote lazima niwe na vitu vyangu ambavyo navitaka na wao wanavitu vyao wanavyotaka.”
“Record label ni studio tu ambao watu watakuwa wanasimamia kazi zangu ni kitu ambacho mimi mwenyewe ninaweza nikaenda sehemu yoyote nikafanya kazi zangu. Kuna vitu vingi sana kabla hujaingia kwenye lebo yoyote kama kuna makubaliano mazuri yatakuwepo basi tutafanya kazi,” ameongeza.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amekanusha kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Idris Sultan zaidi ya kuwa marafiki tu.
Share:

Man Utd kukutana na West Ham robo fainali EFL Cup

Mechi za robo fainali EFL Cup ratiba imetoka baada ya kumuondoa Guardiola, Mourinho sasa atacheza na Bilic.
Mechi hizi zitachezwa katika wiki inayoanza Tarehe 28,Novemba.
Hii ndo ratiba kamili ya Michuano ya EFL Cup.
Share:

‘Magufuli ameletea msiba Dodoma’

WAKATI serikali ya awamu ya tano ikiendelea na hekaheka za kuhamishia makao makuu yake mkoani Dodoma, baadhi ya wakazi wa mkoa huo wamelaani hatua hiyo ya serikali na kusema inawasababishia matatizo makubwa,

Wakizungumza na mtandao huu, wakazi wa Ndachi kata ya Miyuji, Manispaa ya Dodoma, wamesema baada ya serikali kutangaza kuhamishia makao makuu yake Dodoma, tayari wameanza kuporwa ardhi yao.
Wameenda mbali zaidi na kutishia kuwakata kwa mapanga na kuwajeruhi kwa mishale watu wanaovamia maeneo yao kwa madai kuwa wana hatimiliki kutoka Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) pamoja na halmashauri.
“Sisi tunafahamu kuwa eneo hili halijapimwa na watu tuliopo hapa ni wazawa hivyo tunashangazwa na watu kuja na kudai wana hatimiliki za maeneo haya.
“Tunajutia uamuzi wa Rais Magufuli kuhamishia rasmi makao makuu ya nchi Dodoma, tumeanza kupata matatizo makubwa, watu wenye hati wanadai kuwa wameuziwa maeneo yetu,” amesema Nicholaus Lupimo, Mkazi wa Ndachi.
Ameongeza kuwa, wamekuwa wakipigwa na askari walioagizwa kuondoa wazawa, ambao wanaitwa wavamizi katika eneo hilo licha ya kuishi hapo kwa zaidi ya miaka hamsini sasa.
John Masala, aliyezaliwa mwaka 1954 katika eneo la Ndachi amesema Babu na Baba yake wamekuwa wakazi wa eneo hilo tangu mwaka 1915 na kwamba hata yeye alizaliwa katika eneo hilo ambalo ameishi mpaka sasa.
“Sisi hatujatoka Rwanda wala Burundi, kama wanatuona sisi ni wakimbizi au wavamizi basi waturudishe tulipotoka,” amesema.
Kwa upande wake Jackson Mpilimi, ameeleza kuwa alizaliwa katika eneo hilo mwaka 1968, na hawajawahi kuhama wala kuona maeneo hayo yanapimwa katika kipindi chote hicho.
“Baada ya tangazo la Serikali kuhamia rasmi Dodoma, watu wameingia katika eneo hili wakiwa na hati tunazoamini kuwa ni ‘feki’ wanadai kuwa walishauziwa maeneo haya. Tunafukuzwa na polisi na kupigwa mabomu,” amesema.
Wananchi hao waliamua kuitisha mkutano wa hadhara baina yao na Godwine Kunambi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma siku ya leo ambapo alifika katika eneo hilo ili kusikiliza madai yao.
Amewaomba wananchi hao kumpa siku saba ili aweze kufuatilia kwa kina na kujua kama eneo hilo kama lipo chini CDA au manispaa.
“Nawaomba muwe watulivu nitashughulikia jambo hili ndani ya siku saba na kuwapatia majibu ya kina. Hakuna haki ya mtu yeyote itakayopotea, kama kuna watendaji au mamlaka imehusika katika kupoteza haki za wananchi basi tutatoa taarifa sehemu husika na hatua zitachukuliwa,” amesema.
Share:

RC MWANZA APOKEA UJUMBE WA WAWEKEZAJI KUTOKA KOREA.

  • Awaahidi ushirikiano.
  • Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amepokea ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini, wenye niya yakuwekeza katika mkoa wa Mwanza ukiwa na ujumbe wa watu kumi na watano nakufanya nao mazungumzo mapema katika Ofisi yake kabla yakuendelea na ziara yao katika Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
    Katika mazungumzo yao yaliyodumu saa 1:33, Mkuu wa Mkoa amewahakikishia utayari wa mkoa wa Mwanza kuwapokea wawekezaji kutoka nchini humo lakini pia kuwabainishia maeneo mbali mbali katika sekta ya uchumi ambayo watu wa Korea kusini wanaweza kuwekeza.
    Alianza kwakuwashukuru sana kwakutambua urafiki wa nchi hizi mbili ambao umeanza miaka ya 1960’s, na kuwaambia kuwa Mwanza ni mkoa ambao una fursa nyingi za uwekezaji katika Nyanja mbali mbali ikiwapo: Viwanda, Biashara, Kilimo, uvuvi, Mifugo, kwakutaja baadhi.
    Mkuu huyo wa mkoa ameuwambia ujumbe huo wa watu wa jamhuri ya Korea kusini, uliokuwa unaomngozwa na Bw. Son Yang Soo, kuwa Mwanza ndio sehemu pekeee katika nchi za eneo la maziwa makuu inayo liunganisha soko la Afrika Mashariki kwa nchi za South Sudan, Rwanda, Burudi, Jamhuri ya Congo na hata Kenya na Uganda
    Mkuu wa mkoa amesema kutoka na uchumi wa Mkoa wa Mwanza kufikia Tril. 8.45 kwa mwaka katika uzalishaji lakini pia Mwanza ndio mkoa unaochangia pato la Taifa ukishika nafasi ya pili ambapo mchango wake ni asilimia 9.4 katika pato la taifa ukitanguliwa na Dar es Salaam unaochangia kwa asilimia 17 kwa mwaka, hivyo kwa watu wanaotaka kuwekeza Mwanza wamewaza vyema kama jinsi ujumbe huu wa Korea Kusini ulivyo fanya.
    Naye kiongozi wa msafara huo, Song Young Soo, alianza kwakuwapa Watanzania pole kufuatia tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10, Septemba na kuathiri zaidi Mkoa wa Kagera na mara baada ya hapo, akasema wamefurahishwa na jitihada zinazo chukuliwa na mamlaka ya serikali katika kuahakikisha wawekezaji wanapata fursa yakuwekeza, Song amesema katika Nchi ya Korea Kusini uwekezaji umejikita katika nyanja za Teknolojia ya habari na mawasiliano, Afya na Viwanda kwa ujumla, aidha amesema kufuatia ziara iliyofanywa na mbunge wa Ilemela na Ujumbe wake mapema Mwaka huu, hiyo sasa imeibua chachu na muendelezo wa ushirikiano wanachi wanchi hizi mbili ambazo zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu sasa.
    Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makaazi Dkt. Angeline Mabula (MB), amewataka wana watanzania na wana Mwanza kwa ujumla wao , kuonesha utayari na kuwapokea wageni wanao kuja kwa nia njema yakuwekeza katika Mkoa wa Mwanza “ Niwa ombe tuu wananchi wa Tanzania, kuonesha utayari wakupokea wawekezaji, tunaimba viwanda, viwanda vikiwapo watakao ajiriwa ni watanzania wenye sifa husika, hivyo nilazima tunapopata wawekezaji tuwe na utayari na ukarimu kwa wageni wetu hasa wawekezaji wema na kuwapa ushirikiano kwenye maeneo yetu,” alisema Mabula.
    Ujumbe huo wa Korea Kusini ulikuwa ukiongozwa na Song Yaung Soo, wajumbe wengine ni Shing Jong Sam, Cho Yoop Gon, Kim Gi Geob, Doewak Kim, KTM Kyu il, wengine ni Rark in Nwan, Kim Il Hyun, Kim Ji Mi, Lee Suk Hoom, Kim Chan Kyu, Byun Kyumg Ho, Lee Joom Hwa na Kim Lim Gon na Mkalimani wao aliyekuwa anaitwa Alex Gang.
    Ujumbe huo wa Korea pamoja na mambo mengine utatembelea eneo la Nyamongholo kisha utapata fursa yakujionea Matayarisho ya Mpango Kamambe ya urasimishaji wa Makaazi ya Jiji la Mwanza na mpangilio wake.
    Share:

    RC MWANZA ATOA SOMO KWA WAREMBO MISS TANZANIA. 2016

    MKUU wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewaasa warembo wanaoshiriki shindano la Mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania-2016), kutambua wana jukumu zito mbele yao la kuzisaidia jamii zao katika majukumu mbali mbali ya kijamii.
    Mongella alitoa kauli hiyo muda mfupi mara baada ya warembo 30 wanaoshiriki shindano hilo kumtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha.
    Mongella aliwataka warembo hao kufanyakazi kwa bidii na kujituma kwani ndio njia pekee itakayowawezesha kuondokana na umasikini.
    “Jijengeeni tabia yakufanyakazi kwa bidii na maarifa tena bila kuchoka, hii awamu ya tano ni awamu ya hapa kazi tuu, hivyo kama warembo mnalo jukumu zito la kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais katika kufanya kazi na hasa katika kazi za kijamii, lakini haya yote yatawezekana mkiwa wadilifu na wachapa kazi, sasa hivi mpo kwenye U miss wewe pambana na jenga tabia yakufanya kazi masuala ya nani atakuwa mshindi waachie majaji, alisema Mongella.
    Katika hatua nyingine Mongella amewashauri warembo hao kuto ionea haya Lugha ya Taifa ya Kiswahili, k wakuwa fikra sahihi huja kwa lugha sahihi, amewataka kuinze Lugha hiyo wakati wa mashindano hasa pale wanapotakiwa kujieleza ili kuweza kufikisha ujumbe kwa jamii kwa wepesi.
    Akizungumza kabla yakumkaribisha mkuu wa mkoa wa Mwanza, mmoja wa waratibu wa Mashindano hayo Bibi Pamella Irengo, amesema, wamefurahi sana kama mkoa wa Mwanza kuyapokea mashindano hayo, kwani hii ni mara ya kwanza mashindano hayo yatafanyika nje ya mkoa wa Dar es salaam.
    “Mhe. Mkuu wa Mkoa mashindano haya kwa miaka 21, yamekuwa yakifanyika Mkoa wa Dar es salaam, hivyo kuyaleta Mwanza sisi kwetu ni fursa ya kipekee katika kuutangaza mkoa wetu lakini tunashukuru sana uongozi wa mkoa kwakutuunga mkono nakutupokea kwa moyo mkunjufu.
    Mashindano ya kumsaka Mrembo wa Tanzania yatafanyika Oktoba, 29, 2016 katika Ukumbi wa Rock City Mall, ambapo warembo wapatao thelasini (30), watachuana kumsaka mrembo mmoja atakaye peperusha Bendera ya Taifa katika mashindano ya Dunia na Kauli mbiu ya mashindano hayo kwa Mwaka huu ni
    “Mrembo na Mazingira safi”.
    Share:

    Ofisa usalama feki atupwa jela miaka 2

    MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemhukumu Seleman Manoti, kifungo cha miaka miwili jela kwa kupatikana na hatia ya kujifanya usalama wa Taifa.
    Hata hivyo, mahakama imetoa hukumu hiyo bila mshitakiwa kuwepo mahakamani kutokana na kuruka dhamana kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa.
    Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Flora Haule alisema kuwa upande wa mashitaka, ulileta mashahidi wanne kwa ajili ya kuthibitisha tuhuma hizo.
    Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa, mahakama imeridhishwa na ushahidi huo na kwamba mahakama inamtia hatiani mshitakiwa licha ya yeye kutokuwepo.
    “Hati ya kumkamata mshitakiwa itolewe na adhabu hii itaanza kutumika pindi mshitakiwa atakapokamatwa kwani alitoroka akiwa na haki ya kusikilizwa,” alisema Hakimu Haule.
    Wakili wa Serikali, Ester Kyara aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa iwe fundisho kwa wengine.
    Inadaiwa kuwa Novemba 19, 2014 maeneo ya Kariakoo Msimbazi wilayani Ilala, mshitakiwa alijitambulisha kwa Issaya Odelo na Charles Odinga kuwa Ofisa Usalama wa Taifa, kitu ambacho alijua si kweli. Katika hatua nyingine, kondakta Ally Salum (23), mkazi wa Mwananyamala, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kuiba daladala.
    Mbali na mshitakiwa huyo, Exavery Kaunga (44) ambaye ni mlinzi na mkazi wa Kiwalani, Minazi Mirefu, aliachiwa baada ya ushahidi dhidi yake kuwa na shaka.
    Akitoa hukumu hiyo jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan, alisema kuwa upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanne kuthibitisha kosa hilo.
    “Nimeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, nakutia hatiani mshitakiwa kama ulivyoshitakiwa kwa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela,” alisema Hakimu Hassan.
    Kabla ya kutolewa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Grace Mwanga aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine. Hata hivyo, mshitakiwa alipoulizwa ni kwa nini asipewe adhabu kali, hakujibu chochote na mahakama kutoa adhabu hiyo.
    Washitakiwa hao walishitakiwa kwa makosa mawili ya kula njama kutenda kosa ambapo inadaiwa kati ya Julai 5, mwaka jana, washitakiwa walikula njama kutenda kosa.
    Pia inadaiwa Julai 5,2015 pembezoni mwa barabara ya Nyerere katika Kituo cha Mafuta cha Victoria, washitakiwa waliiba gari lenye namba za usajili T 624 CSH aina ya Eicher mali ya Kampuni ya White Swan.
    Share:

    TFS yanasa lori lenye shehena ya mbao

    WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wamekamata lori lililokuwa likisafirisha mbao zilizovunwa kinyume cha sheria baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria.
    Lori hilo lenye namba za usajili T 676ANQ aina ya Scania lililokuwa likitoka Kigoma kwenda jijini Dar es Salaam, lilikutwa limetelekezwa katika maegesho ya mkazi wa Dar es Salaam, eneo la Amana katika Manispaa ya Ilala na dereva wa lori hilo kutokomea kusikojulikana.
    Hata hivyo, haikuwa rahisi kuzibaini mbao hizo kutokana na kufunikwa kwa miche ya sabuni, viroba vya dawa za kuku pamoja na chupa tupu zilizokuwa zimeshatumika.
    Kaimu Ofisa Habari ambaye pia ni Ofisa Misitu Mkuu wa Wakala hao, Nurdin Chamuya alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria kuwa kuna lori limebeba mbao zilizovunwa kiharamu, walishirikiana na kikosi maalumu dhidi ya ujangili wa wanyama pori na kubaini lori hilo likiwa limetelekezwa katika eneo hilo.
    Alisema wanamtafuta dereva wa lori hilo pamoja na mmiliki wake ili sheria ichukue mkondo wake huku akitoa mwito kwa wananchi kufuata taratibu na sheria za uvunaji wa miti ya mbao ikiwa ni pamoja na kuwa na vibali halali vinginevyo atakayebainika atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya nchi.
    Share:

    Kiini cha nauli juu Dar-Zanzibar chaelezwa

    TATIZO la uhaba wa vyombo vya usafiri kati ya Zanzibar na Tanzania Bara ikiwemo boti zinazokwenda kwa kasi, kwa kiasi kikubwa kumechangia kuwepo kwa tatizo la ulanguzi wa tiketi kwa abiria na kusababisha usumbufu mkubwa.
    Ulanguzi wa tiketi hizo umeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi, Mohammed Ahmada wakati alipofanya ziara katika eneo la bandari ya Malindi.
    Tiketi moja ya boti zinazokwenda kwa kasi zinazomilikiwa na Kampuni ya Azam Marine inayouzwa Sh 20,000 hupanda bei na kufikia Sh 30,000 hadi 40,000.
    Ahmada, akizungumza jana alionesha kukerwa na tatizo hilo na kuahidi kulifanyia kazi kwa sababu linaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi, wakiwemo kinamama na wazee.
    Alisema ingawa tatizo hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa vyombo vingi vinavyofanya safari kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, lakini isiwe sababu ya kupandisha bei kwa kiwango hicho na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wenye kipato cha chini.
    Meneja wa Usafiri wa Kampuni ya Azam Marine, Ali Mohamed Abeid alikiri kuwepo kwa tatizo la tiketi za magendo ambalo wamekuwa wakipambana nalo kwa kiwango kikubwa.
    Share:

    Serikali yazindua mpango maalumu kuboresha afya

    SERIKALI imezindua mpango maalumu kitaifa wa kuboresha afya ujulikanao kama Mkoba wa siku 1,000 utakaotumika kutekeleza afua mbalimbali za lishe nchini kwa lengo la kupunguza udumavu kwa watoto na upungufu wa damu kwa wajawazito na wanyonyeshao.
    Mkoba wa siku 1,000 ni nyenzo ya uwezeshaji unaotumia njia mbalimbali za mawasiliano yenye lengo la kushawishi mabadiliko ya tabia na mitazamo kuhusu lishe katika jamii, ukihamasisha wajibu wa kijinsia wa wazazi na walezi walio ndani ya siku 1,000 za mwanzo wa maisha ya mwanadamu ambazo zinahesabiwa tangu mimba inapokuwa imetungwa hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili.
    Akizindua mpango huo jana jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk Zainab Chaula alisema Mkoba wa siku 1,000 utaasiliwa na serikali kama Mkoba Maalumu wa Kitaifa.
    Alisema mpango uliotengenezwa na mradi wa lishe wa Mwanzo Bora kwa kushirikiana na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) ulifanya kazi katika mikoa sita nchini ambao umesaidia pia kupunguza tatizo la udumavu.
    Kuhusu udumavu, Dk Chaula alisema ni jambo lililopo lisiloonekana ingawaje ni hatari likiwa tishio kijamii, kiuchumi na likihitaji kufanyiwa kazi na kupatikana kwa suluhu.
    Alisema serikali imejipanga kuratibu juhudi zilizofanywa na wadau katika kupambana na aina yoyote ya udumavu nchini.
    Alisema Mkoba wa siku 1,000 utatumiwa na wadau mbalimbali kama maofisa lishe wa wilaya na mikoa, wahudumu wa afya katika jamii ili kuchochea tabia chanya zinazolenga kupunguza tatizo la upungufu wa damu kwa wajawazito na wanaonyonyesha na udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka miwili.
    Alisema msisitizo umewekwa katika kuboresha matendo na majukumu katika jamii ambayo ni muhimu sana katika kupunguza matatizo ya lishe kwa akina mama na watoto.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dk Joyceline Kaganda alisema Mkoba wa siku 1,000 una vyumba sita kila kimoja kikiwa na alama maalumu ya utambulisho, kila chumba kimehifadhiwa machapisho mbalimbali yenye jumbe zinazohamasisha matendo na tabia chanya za lishe katika kila hatua ya maendeleo ya ukuaji wa mtoto.
    Share:

    Wanaosomea fani za kipaumbele wapewe mikataba

    TAARIFA kwamba serikali inakusudia kuweka utaratibu wa kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo katika fani za kipaumbele, kutumikia utumishi wa umma kwa muda fulani, haina budi kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo ya kweli.
    Fani ambazo serikali kwa makusudi imezipa kipaumbele kwa lengo la kupata wataalamu wa kutosha katika maeneo husika, ambayo kwa sasa yana wataalamu wachache ni pamoja na fani za sayansi ya tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta, gesi asilia, sayansi asilia, mabadiliko ya tabia nchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na miundombinu.
    Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya alidokeza juu ya kusudio hilo la serikali, alipokuwa anazungumzia hivi karibuni juu ya utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
    Alisema serikali inafikiria kuchukua hatua hizo, kutokana na kubaini kuwepo kwa wanafunzi wanaosomea fani hizo kwa lengo la kupata mikopo, lakini wakishahitimu hukimbilia kufanya kazi nyingine; au kwenda kufanya kazi nje ya nchi, hivyo kuzorotesha lengo la kupata wataalamu waliotarajiwa katika fani husika.
    Ni wazi kwamba kwa mtindo huo, lengo la serikali la kutoa kipaumbele kwa fani hizo, litaendelea kukwamishwa na wanafunzi wenye azma ya kupata mikopo zaidi kuliko kukuza fani husika kwa kuongeza idadi ya wataalamu wake.
    Sisi tunaunga mkono pendekezo la serikali kwamba wanafunzi wanaotaka kuingia katika fani hizo na kupewa kipaumbele katika mikopo, waingie mkataba na serikali kwa muda maalumu wa kutumikia umma ili kuhakikisha dhamira ya serikali ya kuwapa kipaumbele inatimia.
    Tungependa kukumbushana tu kwamba jambo hilo siyo geni hapa nchini kwetu, kwani miaka ya nyuma taasisi na mashirika ya umma, yaliweza kuwasomesha wafanyakazi wao kwa kuwalipia gharama zote za masomo na malazi katika vyuo mbalimbali ndani na hata nje ya nchi.
    Lakini hiyo ilikuwa inafanyika kwa utaratibu maalumu, ambapo mfanyakazi alikuwa akiingia makubaliano ya kisheria kwamba atakapohitimu, atalazimika kulitumikia shirika husika, siyo chini ya miaka miwili au mitatu, kabla ya kuamua kuondoka na kwenda kufanya kazi nje ya shirika husika.
    Wengi walisomeshwa kwa utaratibu huo; na walioondoka baada ya kuhitimu, walichukuliwa hatua kali kwa mujibu wa makubaliano waliyoyafikia hapo awali na waajiri.
    Wakati umefika sasa kwa vijana wetu, ambao serikali imeamua kuwapa kipaumbele katika kupata mikopo kusomea fani hizo ili kupunguza pengo la wataalamu, nao wakaingia katika mkataba maalumu na serikali kuutumikia umma baada ya kuhitimu masomo yao kwa muda fulani.
    Mkataba huo maalumu utawafanya vijana hao, wawajibike kama tunavyotarajia, badala ya kutumia mkopo na kisha kujiondokea pasipo utaratibu. Hali hii ni sawa na matumizi mabaya ya rasilimali ya umma, jambo ambalo asilani lisifumbiwe macho.
    Share:

    Polisi yawashikilia wanne mtandao wizi wa magari

    POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu wanne kwa tuhuma za wizi wa magari kwa kununua nyaraka za magari yaliyopata ajali na kulipwa na bima.
    Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi, Simon Sirro alisema jana Dar es Salaam kuwa askari waliwakamata watuhumiwa hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
    “Watuhumiwa hawa wanajihusisha na wizi wa magari kwa mbinu ya kununua nyaraka za magari yaliyopata ajali na kulipwa na bima, pamoja na kukata vibali vya namba ya ‘chassis’ ya magari hayo kisha kuweka kwenye magari waliyoyaiba,” alisema Kamanda Sirro.
    Alisema baada ya askari kupata taarifa hizo, walifanya ufuatiliaji eneo la Tandale na kukamata mtuhumiwa Dennis Gasper (25), mfanyabiashara wa Manzese Uzuri akiwa na mabaki ya gari namba T 290 DDM Toyota ALPHAD.
    Alisema katika mahojiano mtuhumiwa alitaja watuhumiwa wengine na kuwaongoza askari hadi Magomeni Mikumi maeneo ya kituo cha daladala na kuwakamata watuhumiwa wengine watatu ambao ni Alfred Ditrick (33), mkazi wa Sinza, Venance Bureta (24) wa Mbezi na Dickson Valentino (23) mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na mkazi wa Kimara, wote katika Jiji la Dar es Salaam.
    Kamanda Sirro alisema watuhumiwa hao walikutwa na gari la wizi namba T 368 CES Toyota Passo na walipohojiwa walikiri kufanya matukio mbalimbali ya wizi wa magari katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuyauza nje ya mkoa huo.
    Katika tukio lingine, askari wamekamata magari mengine matatu ya wizi yaliyoibwa mkoani Dar es Salaam na kupelekwa mafichoni Arusha yakiwemo Toyota Vitz T 262 CTF, Suzuki Carry lenye namba za usajili T 935 CPC, Toyota Passo lenye namba za usajili T 368 CES na Toyota Landcruiser Prado lenye namba za usajili T 735 BLZ.
    Alisema watuhumiwa wa mtandao huo wanashikiliwa mkoani Arusha na juhudi za kuwafuata zinafanyika ili kuja kuwaleta Dar es Salaam kujibu mashitaka yanayowakabili.
    Share:

    Pluijm aziita timu zinazomtaka

    KOCHA Hans van Pluijm amesema milango iko wazi kwa timu yoyote inayomhitaji.
    Kocha huyo Mholanzi alitangaza kujiuzulu juzi baada ya waajiri wake Yanga kuingia mkataba na kocha wa Zesco ya Zambia, George Lwandamina bila kumshirikisha.
    Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm alikiri timu kadhaa kumwania lakini akasema ni mapema kuzitaja na kusisitiza amefungua milango kwa yeyote inayomtaka kumfuata kwa mazungumzo.
    “Muhimu siwezi kukaa bila kufundisha kwa sababu ndio kazi yangu na nimeizoea hivyo kweli nahitaji timu ya kufanya nayo kazi,” alisema.
    Licha ya kujiuzulu, taarifa za Yanga zilisema kuwa Pluijm alitakiwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi na nafasi yake ya ukocha angepewa Lwandamina, jambo ambalo Pluijm alilikataa.
    “Nahitaji kuendelea kufundisha timu yoyote itakayonihitaji, ni mapema kuzungumzia ni wapi, lakini nawashukuru Yanga na wachezaji wote kwa kipindi chote ambacho tulifanya kazi pamoja, pia mashabiki waendelee kuiunga mkono timu yao wasikate tamaa,” alisema.
    Pluijm amekuwa akihusishwa na kujiunga na Azam FC, jambo ambalo amelikanusha kuwa halina ukweli.
    Alisema sio vyema kuzungumzia timu ambayo tayari ina makocha wake, kitaalamu haipendezi. Kwa upande wa Azam FC walisema kwa sasa hawana mpango wa kumbadilisha kocha, kwani aliyepo bado ana mkataba, na kwamba wanaamini wachezaji watamuelewa taratibu falsafa yake na mambo yatakwenda vizuri.
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba alisema jana kuwa Pluijm ni kocha mzuri na anasikitika kuondolewa kwake katikati ya ligi na kwamba anamheshimu isipokuwa hawana mpango wa kumchukua.
    “Tunaamini kocha tuliye naye ( Mhispania Zeben Hernandez) anatosha, naamini wachezaji wakimuelewa watabadilika na kufanya vizuri, kama itatokea kumbadilisha kocha basi tutaangalia sehemu nyingine na sio nyumbani,”alisema.
    Share:

    Serikali yazipiga stop Yanga, Simba

    SERIKALI imezipiga stop klabu za Yanga na Simba kuendelea na michakato yao ya kubadili umiliki wake hadi pale yatakapofanyika marekebisho ya katiba zao.
    Hayo yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
    Hivi karibuni klabu hizo kongwe ziliazimia kuingia kwenye mabadiliko, Yanga ikikodishwa na mwenyekiti wake Yusuf Manji na Simba ikitaka kuuza hisa asilimia 51 kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’.
    Kiganja alisema Serikali haikatai mabadiliko ya uendeshaji katika klabu hizo pamoja na nyingine za wanachama, ila inachotaka kwanza kufanyike marekebisho ya katiba zao kwani za sasa haziruhusu mabadiliko hayo.
    Alisema kuwa BMT inapenda kuona wahusika wanafuata sheria na taratibu za nchi katika kufikia malengo yao, ambapo alisisitiza kuwa kuendelea na michakato hiyo kabla ya kurekebisha katiba zao ni kosa na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
    “Hivi karibuni kumeibuka michakato ya watu wakitaka kubadilisha umiliki wa klabu za wanachama na kuzielekeza katika utaratibu wa hisa na ukodishwaji, vitendo vimesababisha migogoro mikubwa ambayo inaashiria uvunjifu wa amani…,” alisema.
    Kiganja alisema tayari mezani kwake kuna barua nyingi za wanachama wa Yanga wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato huo wa kubadilisha umiliki.
    Kwa mujibu wa katiba ya Yanga iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 Ibara ya 56 inaeleza kuhusu kampuni ya umma: Inaeleza kuwa kutakuwa na kampuni itakayojulikana kama Young African Sports Corporation Limited ambayo itasajiliwa chini ya sheria ya makampuni kama kampuni ya umma yenye hisa.
    Sehemu ya pili ya ibara hiyo inasema wanachama wote katika klabu ambao katika tarehe ya marekebisho ya Katiba ya mwaka 2007 wako hai kwa nguvu ya uanachama wao watakuwa wanahisa katika kampuni kwa kiwango cha idadi ya hisa watakapopata kwa mujibu wa muafaka wa Yanga uliofikiwa na wana Yanga Juni 22, 2006.
    Klabu itamiliki hisa zilizosawa na asilimia 51 ya hisa zote zilizomo katika klabu hiyo. Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utachagua wanachama wawili, ambao sio miongoni mwa viongozi wa klabu kuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni kwa ajili ya kuwakilisha maslahi ya klabu kwenye kampuni.
    Tayari Yanga iko chini ya Kampuni ya Yanga Yetu ambayo ni mali ya mwenyekiti wa klabu hiyo Manji, ikiwa ni kinyume na katiba yao wenyewe.
    Kiganja alisisitiza kuwa klabu zisitishe mipango ya kubadilisha uendeshaji na ziendelee kuwa mali ya wanachama. Wakati Yanga walikuwa tayari wameishaingia mkataba wa miaka 10 wa
    kuikodisha klabu yao, wenzao wa Simba walijipa miezi sita kukamilisha taratibu za kuuza hiza.
    Share:

    Mbarawa awataka Posta kukusanya mapato

    WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania kusimamia mapato kwa kukusanya fedha kinyume cha hapo atachomoa mmoja mmoja na kuweka wengine kwa nusu saa tu.
    Aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo jijini Dar es Salaam.
    Katika uzinduzi huo, alisema kwa kuwa serikali inahitaji fedha, kama waziri hahitaji kuambiwa maneno mengi, kwani tofauti na hapo ataendelea kuwachomoa wajumbe hao mpaka apate kile anachokihitaji.
    “Nahitaji pesa kwenye shirika. Ukiniambia maneno mengi mimi sijali, mimi nataka pesa, serikali inataka pesa, sitaki kitu kingine. Ni lazima msimamie mapato mkishindwa nachomoa mmoja mmoja. Naweza kufanya hivyo nusu saa tu. Nitaendelea kufanya hivyo mpaka nihakikishe Napata kile ninachokihitaji,” alisema Profesa Mbarawa.
    Share:

    Historia MOI upasuaji kwa wenye kibiongo

    KIBIONGO ni tatizo la kupinda kwa mgongo upande moja hasa wa kulia, hali inayomfanya mtu aliye na hali hiyo kutembea akiwa ama ameinama au kujikunja. Tatizo hilo mtu huweza kuzaliwa nalo au kutokea baadaye mtoto anapokuwa amefikisha umri wa miaka mitatu na kuendelea.
    Kwa kuwa hapa nchini kulikuwa hakuna upasuaji kwa tatizo hilo, watu waliokuwa na shida hiyo walikuwa wakikua nalo hivyo hivyo isipokuwa wenye uwezo wa kifedha na kuwa na taarifa sahihi walipelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji. Hivi sasa ufumbuzi umepatikana nchini.
    Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa kwa mafanikio wa kunyoosha mfupa wa mgogo wa mtoto uliopinda (kibiongo). Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Othman Kiloloma anasema upasuaji huo umefanyika kwa kutumia teknolojia ijulikanayo kama ‘posterior instrumentation and fusion’.
    Inahusisha uwekaji wa vyuma maalumu kwenye mfupa wa mgongo katika sehemu ya juu na chini ya mfupa wa mgongo na kuufanya unyooke kama inavyotakiwa.
    Dk Othman anasema taasisi hiyo imefanikiwa kufanya upasuaji huo kupitia madaktari bingwa walioko kwenye mafunzo ya ubobezi wa juu katika upasuaji wa mifupa na mgongo kwa watoto kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Marekani.
    “Uanzishwaji wa upasuaji huu umetokana na kuanzisha ushirikiano wa kimafunzo kati ya Taasisi ya MOI na Chuo cha Madaktari bingwa wa upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini (COSECSA) na madaktari bingwa kutoka Marekani,” anasema.
    Anasisitiza kuwa uanzishwaji huu wa kunyoosha migongo ya watoto iliyopinda unatarajiwa kuisaidia serikali kupunguza rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi ambazo ni za gharama kubwa.
    Kutokana na hatua hiyo, uongozi wa MOI unatoa mwito kwa madaktari wote nchini kwenda kupata mafunzo hayo kwenye taasisi hiyo. Pia wazazi wenye watoto wenye matatizo hayo wawapeleke hospitalini wafanyiwe uchunguzi na upasuaji.
    Awali watoto waliokuwa wakienda India na sehemu nyingine kutibiwa iliwagharimu dola 6,000 (Sh milioni 13 na zaidi).
    “Sasa hivi upasuaji huo unafanyika hapa nchini, mgongo unanyooka na mgonjwa anarudi katika hali ya kawaida kwa gharama ya dola 2,000 tu (takribani Sh 4,400,000),” anasema.
    Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mifupa na Viungo, Bryson Mcharo anasema huo ni upasuaji mpya, na ni mara ya kwanza kufanyika MOI lakini umekuwa ukifanyika nchi nyingine.
    Anasema ukubwa wa kupinda kwa mgongo huo hutegemeana na umri wa mtoto. Anasema wataalamu hawajabaini sababu ya tatizo hilo. Mcharo anasema hii ni mara yake ya kwanza kushiriki katika upasuaji huo, na hivi sasa yupo kwenye mafunzo ya upasuaji wa mifupa ya watoto.
    Katika upasuaji uliofanyika nchini, anasema walifanikiwa kunyoosha mgongo wa mtoto mwenye umri wa miaka 13 anayesoma kidato cha kwanza. Anasema kwa sasa Moi wana vifaa vinavyowawezesha kuwawekea wagonjwa 30 baada ya kufanyiwa upasuaji.
    Inaelezwa kwamba baada ya mtu kufanyiwa upasuaji huo na kuwekewa kifaa maalumu mgongoni, kuna baadhi ya vitu hataweza kuvifanya tena kama awali.
    Hupewa masharti ya kutoinama endapo anataka kuokota kitu ama kupinda kama wengine wanavyoweza na pia huelekezwa namna ya kuishi na kifaa hicho mwilini. Mama mzazi wa mtoto huyo ambaye ni mkazi wa Yombo, Temeke, Dar es Salaam, Itika Mwankenja anasema mtoto wake hakuzaliwa na tatizo hilo na kwamba lilimpata akiwa na umri wa miaka 11.
    “Kama wazazi tuligundua hali hiyo ya mabadiliko kwa mtoto wetu kwa kuwa ni kitu ambacho hatukuwahi kukiona kwake,” anasema.
    Mzazi huyo anamshukuru Mungu kwa kumwezesha mtoto wake kufanyiwa upasuaji mkubwa wa mafanikio. Kwa mujibu wa mama huyo hivi sasa kuna tofauti kubwa kabla ya upasuaji na baada ya mtoto kufanyiwa upasuaji huo.
    Anasema mtoto wake huyo anaendelea vizuri na mazoezi anayoyafanya baada ya upasuaji huo. Mtoto huyo anayesoma kidato cha kwanza anasema baada ya kupatwa hali hiyo, alikuwa akichoka anapokaa kwa muda mrefu hasa akiwa darasani.
    “Ilibidi niwe najikaza ili muda wa kurudi nyumbani ufike na nilikuwa ninaandika kwa shida lakini kwa sasa baada ya upasuaji naweza kukaa muda mrefu,” anasema.
    Ni dhahiri kwamba, MOI imeandika historia mwaka huu ya kufanya upasuaji mkubwa wenye mafanikio, hatua inayotajwa kuwa ni ukombozi kwa jamii ya Tanzania na majirani zetu.
    Share:

    Mfumo wa PReM utakavyodhibiti wanafunzi hewa

    TANGU serikali iliporuhusu mazingira ya soko huria katika sekta ya elimu, kumekuwapo na shule binafsi nyingi. Katika shule hizo binafsi, suala la kuhamisha wanafunzi limekuwa halizingatiwi kama ilivyokuwa miaka ya nyumba ambapo ilikuwa ni lazima taarifa za mwanafunzi za kuhama zipate baraka na mamlaka za elimu katika ngazi za kata, wilaya na mkoa na taarifa kubaki katika ngazi hizo.
    Kukatika kwa mnyororo huo ulifanywa uhamishaji na taarifa za mwanafunzi kutokuwepo katika ngazi husika zaidi ya shule ambayo mwanafunzi husika anatoka na kuhamia. Badala yake shule ambayo imepokea mwanafunzi ilikuwa ikiandika barua Necta ya kuainisha wanafunzi waliohamia na shule walizotoka.
    Ili kuwa na mfumo unaoeleweka, Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limeunda mfumo wa kutunza taarifa za wanafunzi wa Shule za Msingi (PReM) ambao utasaidia katika uandikishaji wa wanafunzi wote wa shule za msingi na wanafunzi hao kupewa namba maalumu itakayomtambulisha mwanafunzi katika ngazi mbalimbali za mafunzo zinazosimamiwa na baraza.
    Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi anasema mbali na mfumo huo kumtambulisha mwanafunzi, pia utasaidia katika uhamisho wa mwanafunzi kutoka shule moja hadi nyingine ndani na nje ya mkoa katika shule za umma na zile binafsi.
    “Ni mfumo ambao utarahisisha utaratibu unaotumika sasa wa kuhamisha mwanafunzi kutoka shule moja hadi nyingine ili kuondoa tatizo la wanafunzi hewa,” anasema. Anasema Mfumo wa PReM utasaidia katika uandaaji na utoaji wa takwimu za wanafunzi katika ngazi ya shule, wilaya, mkoa hadi ngazi ya kitaifa.
    Aidha, Nchimbi anasema mfumo huo pia utasaidia katika ufuatiliaji wa taarifa za matokeo ya kila mwanafunzi kuhakikisha wadau mbalimbali wa elimu wanapata ufahamu wa kutosha kuhusu ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi ya shule.
    Baraza limefanya majaribio ya mfumo huu katika mikoa miwili ya Mwanza na Ruvuma na ifikapo Desemba mwaka huu, utaimarishwa ili Januari hadi Mei 2017, utumiwe na mikoa yote kusajili wanafunzi wa shule za msingi.
    “Mfumo huu wa PReM utasimikwa Baraza la Mitihani Tanzania na kutumiwa na wadau mbalimbali wa Elimu. Baraza la Mitihani la Tanzania litahakikisha mfumo huu unapatikana katika ngazi za wilaya ili wadau wote waweze kupata taarifa mbalimbali za elimu,” anasema.
    Anasema NECTA ina wajibu wa kutoa mafunzo ya uendeshaji wa mfumo wa ngazi ya mkoa, kuandaa na kusimamia taratibu za uandikishaji na utunzaji wa taarifa za mwanafunzi katika ngazi ya wilaya na mkoa, na kuchukua taarifa za usajili za wanafunzi wa darasa la nne na la saba.
    “Necta pia ina wajibu wa kuweka matokeo ya mitihani ya kitaifa, kutatua changamoto za mfumo wa PReM katika ngazi ya mkoa, kuhakikisha usalama wa taarifa zilizohifadhiwa katika mfumo na kusimamia uendeshaji wa mfumo katika ngazi zote.
    Aidha, Nchimbi anasema ili kufikia malengo mahususi ya mfumo wa PReM, kila mdau wa elimu atatakiwa kutimiza wajibu wake. Wadau hao ni mwalimu mkuu, mratibu wa elimu kata, ofisa elimu wilaya, mkoa na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
    Anasema kwa ofisi ya mwalimu mkuu, inawajibu wa kuandaa orodha ya wanafunzi kwa ajili ya kuandikishwa kwenye mfumo wa kupeleka wilayani, kupeleka taarifa za uhamisho na matokeo ya kila mwaka kwa wanafunzi wote wilayani na kupokea ripoti za uandikishwaji na uhamisho wilayani.
    Nchimbi anasema kwa upande wa ofisi ya mratibu wa elimu kata, ina wajibu wa kutoa ripoti za takwimu za shule katika kata husika, na kusimamia uingizaji wa taaria za wanafunzi ngazi ya shule na kata.
    “Ofisi ya Ofisa Elimu wilaya yenyewe ina wajibu wa kusimamia uingizaji wa taarifa ya uandikishwaji, uhamisho na matokeo kwenye mfumo, kuthibitisha uhamisho wa mwanafunzi kwenye mfumo na kutoa ripoti za takwimu za shule zote wilayani.
    Nchimbi anasema ofisi ya elimu mkoa, wanawajibu wa kutekeleza mfumo wa PReM kwa kusimamia uandikishwaji wa wanafunzi wa shule zote katika mkoa husika, kuthibitisha uhamisho wa mwanafunzi katika shule zote za mkoa husika na kutoa ripoti za takwimu za shule za mkoa husika.
    Anasema kwa upande wa Ofisi ya Rais, Tamisemi inawajibika kuhakikisha kila mkoa unaingiza taarifa za wanafunzi wa ngazi zote katika shule za msingi na kutoa ripoti mbalimbali za takwimu na matokeo kulingana na mahitaji yao.
    Nchimbi anasema wanawajibika pia kupokea na kuingiza taarifa za uandikishaji kutoka shule za wilaya na kuingiza taarifa za matokeo na uhamisho kwenye mfumo na kutoa ripoti za uandikishaji na uhamisho za kila shule katika wilaya husika.
    Share:

    Yanga siku 5 bao kumi

    ANGA siku tano bao 10! ndivyo ilivyotokea jana baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu kushinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu na hivyo kuwa na mabao 10 ndani ya siku tano baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 6-2 Jumamosi iliyopita.
    Ushindi huo uliopatikana kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam umeifanya Yanga kuendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 24, tofauti ya pointi tano na vinara wa ligi hiyo, Simba. Katika mechi hiyo ya kiporo, Yanga ilitawala katika vipindi vyote vya mchezo.
    Obrey Chirwa nyota yake iliendelea kung’ara jana baada ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya tano ya mchezo huo.
    Alifunga bao hilo kwa shuti baada ya kuunganisha mpira wa Simon Msuva. Mshambuliaji huyo sasa amefikisha mabao matano. Amisi Tambwe aliifungia Yanga bao la pili katika dakika ya 63.
    Alifunga bao hilo baada ya kuukokota mpira nje ya 18 huku mabeki ya Ruvu wakimsindikiza kabla ya kuachia fataki lililojaa wavuni. Dakika ya 82, Msuva alifunga bao la tatu kwa kazi nzuri ya Tambwe aliyempigia pande murua.
    Tambwe aliibua tena shangwe kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kufunga bao la nne katika dakika ya 90 baada ya kumzidi ujanja mlinzi wa Ruvu, Michael Aidan aliyekuwa akirudisha mpira kwa kipa wake na Tambwe kuuwahi na kuujaza wavuni.
    Share:

    Kagera yatumia mil. 800/- ukarabati miundombinu

    UKARABATI wa miundombinu iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera umeanza, na tayari Sh milioni 800 zimetumika kati ya Sh bilioni tano zilizotolewa na wadau mbalimbali katika kuwachangia waathirika wa tetemeko hilo lililotokea Sept 10, mwaka huu na kusababisha vifo, uharibifu wa majengo na miundombinu mbalimbali.
    Aidha, imeelezwa kuwa, inahitaji miaka miwili au mitatu kwa mkoa huo kurejea katika hali ya kawaida kutokana na maeneo mengi kuathirika vibaya.
    Hayo yalibainishwa mjini Dodoma jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohammed Mchengerwa alipokuwa anazungumzia taarifa ya serikali ya maafa ya tetemeko yaliyotokea mkoani Kagera.
    Taarifa hiyo iliwasilishwa mbele ya kamati hiyo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. Alisisitiza kuwa, serikali imeihakikishia kamati hiyo kuwa inaendelea na jitihada za kusaidia waathirika hao.
    Aidha, alisema kwa mujibu wa taarifa ya waziri huyo kwa sasa wanafunzi wa shule ya sekondari Ihungo wamehamishwa kupelekwa shule ya Mwani ili kuendelea na masomo.
    “Hadi sasa wagonjwa 440 waliokuwa hospitali wameendelea kupatiwa matibabu na kati ya wagonjwa hao sita wamefariki dunia,” alisema Mchengerwa.
    Alisema kutokana na taarifa hiyo, kwa sasa idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko hilo imeongezeka kutoka watu 17 na kufikia 23.
    Alisema taarifa hiyo pia imebainisha kuwa wananchi walioathirika na janga hilo, kwa sasa wanaendelea kupata huduma mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa miundombinu yao ambapo askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) takribani 96 wapo mkoani humo wakiendelea kulinda na kusaidia masuala ya usalama.
    Akizungumzia mapendekezo ya kamati hiyo kwa serikali, Mchengerwa alisema imeitaka serikali kusimamia masuala ya afya na usalama kwa wananchi waliopatwa na tetemeko.
    Aidha, alisema kamati hiyo imeishauri serikali iendelee kuratibu kwa kushirikiana na wahisani na kuhakikisha wanawatumia wataalamu wa ndani katika kufanya utafiti katika maeneo yenye bonde la ufa kabla ya maafa kutokea.
    Pia kamati imeiomba serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya tetemeko na kujenga nyumba imara zinazostahimili mtikisiko, kuboresha kitengo cha maafa na kuanzisha vituo vya kitaifa vyenye vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majanga.
    Akizungumzia serikali kuhamia Dodoma, alisema kamati hiyo imeishauri itungwe sheria maalumu itakayosisitizia jambo hilo na kuongeza nguvu katika kuisimamia Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) inayolalamikiwa kwa kuwa na urasimu mkubwa katika upangishaji wa ardhi.
    Share:

    nunua vitabu vya watoto kuanzia chekechekea mpaka darasa la saba

    nunua vitabu vya watoto kuanzia chekechekea mpaka darasa la saba

    Arquivo do blog