WATUMISHI wa umma wameshauriwa kuchangamkia fursa ya kununua nyumba
zilizojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) kabla ya muda wa kustaafu
ili kujitengenezea maisha mazuri baada ya kustaafu.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati alipotembelea nyumba za watumishi zilizojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) zilizopo eneo la Bunju na nyumba za wananchi Magomeni Kota.
Makonda alisema watumishi wengi amekuwa wakiishi maisha ya tabu baada ya kustaafu kutokana na kutojipanga kabla ya kustaafu na gharama za maisha kupanda, lakini kupitia ujenzi wa nyumba hizi wanaweza kupata nyumba hizo kwa gharama nafuu.
“Tumeona hapa kuna nyumba za kima cha chini cha shilingi milioni 38 unaweza ukajipanga ukakopa nyumba na kulipa taratibu hata pale utakapostaafu unakuwa na nyumba yako na familia yako na kuishi bila tabu,” alisema Makonda.

0 comments:
Post a Comment