Kufuatia
uhamisho wa aliyekuwa mkurugenzi wa Idara ya habari-Maelezo Assah Mwambene
uliofanyika March 7 2016 kwenda wizara ya mambo ya nje ushirikiano wa kikanda
na kimataifa ulianza mchakato wa kumpata mkurugenzi mwingine.
Leo August 9
2016 Waziri wa Habari, Utamaduni sanaa na michezo, Nape Nnauye amemteua
Mkurugenzi wa idara ya Habari-Maelezo Hassan Abbas kuziba nafasi ikiyoachwa
wazi na Assah Mwambene Kabla ya uteuzi huo Hassan Abbas alikuwa ni meneja
Habari na Mawasiliano katika ofisi ya Rais inayosimamia utekelezaji wa program
ya matokeo makubwa sasa.
0 comments:
Post a Comment