TANZANIA jana ilianza vibaya Michezo ya 31 ya Olimpiki baada ya
mchezaji wake wa judo, Andrew Thomas Mlugu kudundwa na Jake Bensted wa
Austria katika mchezo wa kilo 73.
Tanzania katika michezo hiyo iliyoanza Agosti 5, imepeleka wachezaji
saba, judo akiwa mchezaji mmoja, wawili wa kuogelea, ambao ni Magdalena
Moshi na Hilal Hilal na wale wa riadha, ambao bado hawajaenda Rio
kutokana na ratiba yao kuwa mwishoni.
Mchezaji huyo wa judo alishiriki mashindano hayo kupitia tiketi ya upendeleo baada ya kushindwa kufuzu kwa njia ya kawaida.
0 comments:
Post a Comment