KOCHA wa Mtibwa Sugar Salum Mayanga amesema ushindi walioupata katika
mchezo dhidi ya Majimaji umetokana na juhudi za kuboresha kikosi chake
mara kwa mara pindi wanapobaini mapungufu.
Mtibwa Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Majimaji,Songea.
Ushindi huo unaifanya Mtibwa Sugar kufikisha pointi sita baada ya kushinda michezo miwili dhidi ya Ndanda FC mabao 2-1 na Majimaji mabao 2-1 na kufungwa mmoja dhidi ya Ruvu Shooting.
Akizungumza na gazeti hili, Mayanga alisema kikosi chake kilifanikiwa kupata ushindi huo baada ya kutumia nafasi walizopata na kwamba wanategemea kuendelea na harakati zao za kupata matokeo ya ndani na nje ya uwanja wao.
“Tunashukuru kwa kupata pointi tatu ugenini, unajua tulivyopoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting, tulijaribu kuangalia mapungufu yetu na hatimaye tukafanyia kazi na kupata ushindi huu,” alisema.
Alisema wanajipanga kwa mchezo ujao kuhakikisha wanapambana na kupata matokeo mazuri.

0 comments:
Post a Comment