Wednesday, 26 October 2016

Agizo la Waziri Hamad Masauni kwa Askari na Madereva endapo ajali itatokea

Ajali za Barabarani zimekuwa zikipoteza maisha ya wananchi wengi kila siku huku wengine kupata ulemavu wa kudumu.  Leo October 25, 2016 Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Eng. Hamad Masaudi imetoa mkakati ili kupunguza ajali hizo.
Naibu Waziri Eng. Hamad Masauni amesema kuwa mkakati huo utahusikana na kuchukua hatua kali kwa askari ambao watahusika na masuala ya ukaguzi  wa vyombo vya usafiri, madereva pamoja na wamiliki wa magari yatakayohusika kwenye ajali.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri Masauni amezitaja wilaya za Ilala na Kinondoni kuwa zinaongoza kwa ajali nchi Tanzania.
Ayo TV inakuletea taarifa kamili ya Naibu Waziri Hamad Masauni wakati akizungumzia mikakati ya Serikali juu ya ajali za Barabarani.
Share:

PICHA 7: Jinsi Star Davido anavyomuhudumia mtoto wake

Moja kati ya vitu ambavyo hufanywa siri sana na mastaa wengi duniani ni kuonesha jinsi wanavyoishi na familia zao kuanzia maisha ya mahusiano ya kimapenzi au malezi ya watoto. Lakini kwa baadhi yao huwa tofauti sana linapokuja suala la malezi ya watoto na hili limedhihirishwa mara kadhaa na mastaa wakubwa kama Chris Brown, Mwana FA, Diamond Platnumz na wengine wengi ambao wamefanikiwa kupata watoto.
Leo nimezipata picha 7 alizozipost Snapchat star wa hit single ya How Long aliyompa collabo female singer Tinashe kutoka Marekani. Davido ameonekana akiwa na mtoto wake wa kike.




Share:

PICHA 12: Watoto wanavyoshuka na kupanda mita 800 za mlima huko China ili kwenda shule

Katika milima ya jimbo la Sichuan kusini magharibi mwa China, kundi la watoto ambalo lilikuwa likishuka mita 800 kwenye mlima ili kufika shule huku wakitumia njia za asili ambazo ni ngazi za miti ambayo ni hatari sasa wanajengewa ngazi za chuma.
Ngazi hiyo ya chuma inayojengwa na wanakijiji itakuwa na mabomba 1,500 ya chuma na inatarajiwa kukamilika mwezi November mwaka huu, ujenzi wa ngazi hizo zenye gharama ya dola za marekani 150,000 ambazo ni karibu Tsh za kitanzania milioni 327, ilianza kujengwa na wanakijiji mwezi August mwaka huu. 
Ngazi hiyo inatarajiwa kuwa na muundo imara zaidi pia inatarajiwa itakuwa yenye usalama zaidi kwa hata wanakijiji wa kijiji hicho ambao watakuwa wanaitumia kupanda na kushuka kila wiki kununua bidhaa mbalimbali na kufanya biashara zao katika soko ambalo liko mbali na wanakoishi. Siku za nyuma wanakijiji walikuwa wakitumia miti ya mizabibu ambayo ilikuwa mibovu.









Share:

Gambia kujiondoa katika mahakama ya uhalifu ICC

Serikali ya Gambia imesema kuwa itajiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC mara moja.
Hatua hiyo imekuja kutokana na madai kuwa ICC hushughulika na Waafrika pekee.
Maamuzi ya kujitoa katika mahakama hiyo yanafuatia baada ya Burundi na Afrika ya Kusini kutangaza kujiondoa
Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh amekua madarakani tangu mapinduzi nchini humo mwaka 1994.
Uchaguzi ujao unatarajiwa kufanyika desemba lakini mapema mwaka huu viongozi nane wa upinzani walikamatwa na kuhumiwa miaka mitatu jela kwa kuhusika katika maandamano ambayo hayakua na kibali.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty limesema kuwa maamuzi hayo ni sehemu ya muendelezo wa ukandamizaji wa haki za binadamu nchini Gambia.
Share:

al Hussein:chuki za makabila ni hatari Sudan Kusini

Kamishina wa juu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa Prince Zeid Ra'ad al Hussein ameonya kuwa kuzuka kwa kauli za chuki na uchochezi wa ghasia za kikabila nchini Sudan kunaweza kusababisha mauaji ya halaiki.
Hofu baina ya makabila makubwa Dinka, na yale ya kutoka ukanda wa ikweta imeongezeka kwa kasi katika wiki za hivi karibuni, baada ya shambulio la basi huko Dinka na kusababisha vifo vya watu kadhaa waliokuwa wakisafiri.
Umoja wa mataifa unasema kuwa una wasiwasi juu ya mashambulio hayo na kuhusu barua za kuogofya watu kutoka ukanda wa Ikweta inaonekana kuwa ni kulipiza kisasi.
Pia amesema kuwa ametilia maanani kauli iliyotolewa na Rais wa nchi hiyo Salva Kiir ambayo imetafsiriwa na wengi kama ina msukumo wa kikabila. Rais Kiir alisema yeye mwenyewe ataendesha operasheni ya kijeshi dhidi ya makundi ya waasi kuwajibika kwa mauaji katika eneo hilo.
Share:

Volkswagen kulipa faini kwa wamiliki

Hakimu wa mahakama kuu nchini Marekani ameidhinisha faini ya karibu dola bilioni kumi na tano kwa ajili ya madai dhidi ya kampuni ya kutengeneza magari Volkswagen ya Ujerumani juu ya kashfa ya uzalishaji wake wa dizeli.
Wamiliki Karibu nusu milioni wa Volkswagen wataweza kurudisha magari yao au kufanyiwa marekebisho, Pia watapokea fidia ya hadi dola elfu kumi.
Volkswagen ilikiri mwaka jana kuwa ilifanya udanganyifu juu ya majaribio ya uzalishaji wa dizeli ili kufanya magari yake kuonekana safi.
Hukumu hiyo ni rekodi kwa ajili ya sekta ya magari nchini Marekani, lakini Volkswagen inakabiliwa na gharama zaidi, kwa faini na kesi za kisheria kutoka majimbo kumi na sita nchini Marekani na katika nchi nyingine.
Share:

Korea Kaskazini 'haiko tayari kuziacha' silaha za nyuklia

Sera ya Marekani kuishawishi Korea kaskazini kuachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia huenda 'haina ufanisi' , mkurugenzi wa shirika la kitaifa la ujasusi Marekani amesema.
James Clapper amesema Marekani jambo ambalo Marekani inaweza kutumainia ni kuzuia uwezo wa taifa hilo, katika hotuba New York.
Ni nadra kwa Marekanikukiri kuwa lengo lake kuu la kuwa na dunia isiyokuwana matumizi ya nyuklia huedna isifanikiwe.
Hatahivyo, wizara ya mambo ya nje Marekani inasema sera yake hiyo haijabadilika.
Korea kaskazini inadai kupiga hatua katika mradi wake wa kutengeneza silaha za nyuklia licha ya upinzani wa kimataifa na vikwazo vikali.
Mnamo Septemba, ilifanya jaribio lake la tano na kubwa la silaha zake za nyuklia, jambo lililozusha shtuma kote duniani.
Akizunguma katika baraza kuhusu uhusiano wa nchi za nje siku ya Jumanne, Clapper ameitaja serikali ya KOrea kaskazini kama iliyo na 'uoga' na kusema inaona silaha za nyuklia kama 'tikiti yao ya kuendelea kuwepo'.
Amependekeza, kutoa vikwazo vya kiuchumi kwa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un kupunguza silaha zake za nyuklia huenda ndio sera bora zaidi.
Akijibu kauli ya Bwana Clapper, wizara ya mambo ya nje imesema bado inanuia kufanya majadiliano ya mataifa sita, ambayo Korea kaskazini ilijitoa mnamo 2009.
Marekani inatarajia kutuma mfumo wake wa ulinzi wa anga za juu Korea kusini (THAAD) hivi karibuni, licha ya upinzani kutoka China na Korea kaskazini.
Washington na Seoul zinasisitiza ni kwa lengo la kuimarisha ulinzi tu dhidi ya tishio kutoka kwa Korea kaskazini.
Share:

Usimbague mteja, mhusishe kuboresha biashara yako

JUMATANO iliyopita niliahidi kuendelea kutoa majibu ya swali lililoulizwa na mfanyabiashara Harrieth Mwakitwange, anayeishi na kuendesha biashara mbalimbali, ikiwemo ya saluni katika eneo la Mabatini mkoani Mbeya.
Swali hilo lilikuwa na vipengele a na b ambapo kipengele a kilijibiwa na wataalamu kutoka katika mtandao wa majibu www.answers.com, na kipengele b ndio kinajibiwa na wataalamu hao leo katika safu hii. Hata hivyo, kabla ya kutoa majibu ya kipengele b, ninaona kuwa ni vyema tukajikumbusha swali hilo na vipengele vyake vyote, ili hata msomaji mpya aweze kuelewa kilichoulizwa.
(a) Biashara ni yangu, mteja anahusikaje kunipangia jinsi ya kuiboresha? (b) Hasara ya kumtafuta ili anieleze hili na lile nani atailipa? Mwakitwange aliomba majibu yaegemee zaidi katika biashara ya saluni.
Aidha, kwa kuwa majibu yalikwishatolewa wiki iliyopita, nimeona vyema kuyarudia kwa ufupi ili waliopitwa Jumatano iliyopita wapate mwanga wa nini kiliendelea kwenye safu hii, ndipo niwape na majibu ya kiengele (b).
Kuhusu swali katika kipengele (a), wataalamu wawili tofauti kutoka www.answers.com, wanasema kila mmoja kwa aina yake ya maneno kuwa, biashara nyingi za saluni hasa za mitaji ya kati hufa kutokana na uelewa finyu wa wanaoziendesha kuhusu umuhimu wa kusikiliza mteja anataka nini. Mtaalamu wa kwanza anasema,
“Wapo wahudumu wa saluni wenye tabia ya kulazimisha wateja watumie aina fulani ya dawa bila kusubiri kuwasikiliza ikiwa wana lolote la kuzungumza kuhusu dawa wanayolazimishwa kuitumia”.
“…Wengine wamesababisha wateja wao kukosa nywele zenye afya na wapo waliosababishiwa udumavu nywele au upara vichwani kwa wateja wao”.
Mtaalamu huyo wa masuala ya urembo wa kichwa na muonekano wa uso anasema, mteja mwingine mwenye woga au asiyejiamini hukubali lolote analoambiwa na mhudumu wa saluni anayeshughulika kutengeneza nywele zake, hata kama anajua wazi kuwa dawa anayotakiwa kuitumia ndio iliyompa matokeo mabaya awali.
Anasema, lakini, ikiwa mteja huyo atahusishwa katika mazungumzo ya nini anadhani kinafaa ili kuifanya biashara hiyo ya saluni iwe bora zaidi, anaweza kueleza kilichomsibu hivyo kuchangia kubadili tabia ya wahudumu katika saluni husika kutoka kuhudumia wateja kwa kuzingatia matakwa ya saluni hadi kuanza kusikiliza mapendekezo ya wateja na mwisho kujikuta wakitoa huduma bora kwa kila mteja.
Katika hili, Mwakitwange na wasomaji wengine mtaona kuwa si wakati wote wateja wanapewa nafasi ya kuchagua wahudumiweje na hili linadhihirishwa na mtaalamu wa pili kutoka www.answers.com, anayeeleza kuwa, wahudumu wengine wa saluni ‘husukuma’ dawa zao kwenye vichwa vya wateja au kucha mpya za bandia kwenye vidole vya wateja, ilimradi ziishe, bila kujali afya ya nywele au kucha za mteja husika.
Neno ‘husukuma’ nimelichukua na kulitafsiri kama ilivyopasa kutokana na uzio wake.
Mtaalamu amemaanisha kulazimisha matumizi ya dawa fulani kwenye nywele za mteja fulani au kucha za bandia, bila kujali endapo dawa inakubaliana na nywele hizo, kucha kufaa vidoleni au la.
Kwa maana nyingine, mhudumu aliamua kutoa huduma ilimradi (bora liende) na kusahau kwamba matokeo mabaya yatasababisha biashara yake ionekane kuwa ina walakini. Uhusika wa mteja kuboresha Www.aswers.com inasema, mteja anahusika kwa kuwa ndiye mtumiaji wa huduma.
Mtandao huo unasema si vibaya wakafikiwa watena wane au watano na kuulizwa aina ya dawa za nywele au kucha za bandia wanazopenda kuzitumia, ili mwenye saluni ajue anaweka dawa na kucha za aina gani saluni kwake.
Inaelezwa katika mtandao huo kuwa kuwepo kwa vifaa vinavyopendwa na wateja kunawajengea imani kuwa saluni husika inawapa huduma watakayo.
Kuhusu swali katika kipengele (b), ambapo Mwakitwange anahoji ni nani atalipa gharama za kumtafuta mteja huyo ili aeleze hili na lile, kwa ajili ya kuboresha biashara hiyo ya saluni, mtandao wa majibu, www.answers.com unasema hakuna sababu ya kueafuata mbali wateja ili kuondoa gharama gharama zisizo lazima.
Mtandao huo unaeleza kuwa, mfanyabiashara wa saluni anaweza kuandaa utaratibu mzuri wa kuwahoji wateja wake maswali ya msingi kuhusu biashara hiyo, pindi wanapokuja kupata huduma katika saluni yake.
Kwa maelezo ya mtandao huo, bila kuwaeleza au kwa kuwaeleza kuwa anakusudia kufanya nini, mfanyabiashara ya saluni anaweza kupata majibu yatakayompa mwongozo wa nini afanye ili kuifanya biashara yake iwe bora zaidi.
Unasema si lazima jambo hilo lifanyike kwa siku moja, inayoweza kutompa matokeo au majibu yasiyomsaidia, bali kwa kipindi maalumu kitakachomuwezesha mwenye saluni kupata idadi ya wateja watakaoyafanya majibu kuwa na uzito.
“Itakuwa vyema ikiwa katika kila siku ya mahojiano atakayepewa maswali atakuwa ni mteja anayehojiwa kwa mara ya kwanza, ili kuepuka kurudia swali moja kwa wateja hao hao na kupoteza maana ya kuhusisha wateja kuboresha biashara,” www.answers.com, inasema.
Mtandao huo unaongeza kuwa, kwa biashara ya saluni, hata kama jambo litalalamikiwa na mteja moja tena kwa mfano dhahiri, kama vile kuharibiwa nywele kutokana na matumizi ya dawa isiyofaa kwa kukosa ubora au kwa kumalizika muda wa matumizi, mhudumu au mwenye biashara anapaswa arekebishe kasoro hiyo mara moja kwa kueleta dawa zilizo ndani ya muda wa matumizi.
Share:

Tazara kurejesha nyumba zake ‘kimtindo’

MAMLAKA ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) ina mpango wa kurejesha nyumba 71 zilizouzwa kwa wafanyakazi bila kufuata utaratibu.
Aidha Taasisi hiyo imetoa siku 60 kwa wafanyakazi 457 ambao hawakulipa au wamefanya malipo kidogo kukamilisha malipo, kinyume chake watanyang’anywa nyumba zao.
Meneja Mkuu wa Tazara (Tanzania), Fuad Abdallah alitoa maagizo hayo jana alipotembelea baadhi ya nyumba zilizouzwa katika vituo vya Vigama na Kifuru.
Alisema hatua ya kurejesha nyumba hizo imelenga kunusuru nyumba 71 ambazo ziliuzwa baada ya muda wa mwisho uliowekwa wa mwaka 2008 huku nyumba nyingine 19 ambazo uuzwaji wake ulikuwa na utata jambo ambalo limefanya shirika hilo kufungua kesi mahakamani.
Alisema baada ya kufanya ukaguzi, Mamlaka imebaini kuwa baadhi ya nyumba zinazomilikiwa na ama wafanyakazi au wastaafu, baadhi ya watu walioorodheshwa kama wamiliki walikana kumiliki au kununua nyumba hizo.
Meneja huyo alisema nyumba zilizo sambamba na reli ya Tazara kuanzia Dar es Salaam hadi Tunduma, ni nyumba 831 zilizouzwa kihalali na nyumba 774 zimebaki kwenye taasisi ambazo zinatumika na wafanyakazi katika vituo mbalimbali.
Alisema kazi ya uuzaji wa nyumba hizo ulifanyika kati ya mwaka 2002 hadi 2008 baada ya Bodi ya Wakurugenzi kutoa kibali cha uuzaji mwaka 1999 lengo likiwa ni kupunguza gharama za uendeshaji na matengenezo ya nyumba hizo.
Kwa mujibu wa Abdallah, wamiliki wa nyumba 201 hawajalipa malipo yoyote ambapo Mamlaka ilitarajia kukusanya Sh milioni 178 huku wamiliki wengine 256 wamelipa kidogo na wanatarajia kukusanya Sh milioni 192 watakapomalizia madeni yao.
Share:

Magufuli ni yule yule tuliyemchagua

"NYOTA yake kisiasa ilianza kung’aa mapema zaidi katika viunga vya Tanzania akianzia na utumishi wa umma hadi kufikia ngazi ya uwaziri. Umri wake umeingia katika utu uzima na kuanza kugusa uzuri wa nywele zake, lakini katika mwili wake bado nguvu ya ujana ipo."
Sentensi hiyo ilikuwa kwenye makala iliyowahi kuchapishwa katika gazeti hili, ambapo mchambuzi kutoka Zanzibar, Juma Mohammed, alitabiri mengi ambayo Magufuli anayafanya sasa akiwa Ikulu.
Juma alidokeza kwamba ushiriki wake katika shida za watu na uchapakazi akiwa waziri katika wizara mbalimbali na mbunge wa Jimbo la Chato, ni hali aliyoanza kumtofautisha na wagombea wengine, iwe ni wa vyama vya upinzani au wa chama chake, Chama Cha Mapinduzi.
Katika kipindi cha uwaziri wake na ubunge, Dk John Magufuli alikaa kwa wema, hisani na adabu na wananchi wenzake na ndio maana haikustajaabisha kuona Watanzania wengi, wa kike, kiume, vijana kwa wazee wakamuunga mkono kumpigia kura Oktoba 25 mwaka jana na hata sasa wanaendelea kumuunga mkono kwani ndio tegemeo lao.
Tuliokuwa tukifuatilia hotuba zake wakati akiwa Mgombea Urais wa CCM, Dk Magufuli, kwa hakika maneno yake yalipenya vyema kwenye masikio, yakaakisi shauku ya mabadiliko ya kweli na siyo ya 'kuzungusha mikono'.
Kuna waliodhani ni porojo zilizozoelekwa kwa wanasiasa na ambazo tulizisikia pia kwenye majukwaa ya wagombea wa upinzani lakini wanaomjua vyema Magufuli hawakuwa na mashaka na ahadi zake na kwa hakika wananchi walianza kushuhudia ukweli wa ahadi zake mara tu alipoanza kazi ya kuongoza nchi hii baada ya kuapishwa.
Kutokana na hulka yake tangu akiwa Waziri, Dk Magufuli hakuwa mtu wa porojo, ubabaishaji na usanii na ndio maana alipoibuka na kaulimbiu ya 'Hapa Kazi tu' wakati wa kampeni, watanzania walimwelewa na wakampa kura zao kwa wingi Oktoba 25 na kwa hakika sasa wanaona kazi inafanyika. Juma katika andiko lake anasema:
"Watu wenye busara na waadilifu mara nyingi wanawatendea wema binadamu wenzao katika nchi na kwa hakika maisha yanakwisha kwa mtu huyo kukumbukwa na jamii kwa wema wake, lakini wapo pia ambao hukumbukwa kwa maovu na ubaya wao, ufisadi na kuifisidi nchi".
Hakuna ubishi kwamba Dk Magufuli ni miongoni mwa watu wema na yale ambayo ameyafanya Ikulu katika kipindi kifupi yanadhihirisha kwamba Dk Magufuli ni yuleyule aliyekuwa makini na imara akiwa waziri na sasa akiwa mkuu wa nchi.
Ni kwa muktadha huo, kama alivyotabiri Juma katika uchambuzi wake, Dk Magufuli ataingia katika orodha ya watakaoacha simulizi ya uchapakazi, uadilifu, upendo, umoja na mshikamano kwa jamii ya Tanzania kwa ujumla wake.
Ndio maana, Profesa Patrick Lumumba wa Kenya, hasiti kueleza hadharani namna anavyomkubali rais wetu akisema kwa sasa ndiye rais pekee wa Afrika ambaye anaonekana amekwenda Ikulu kuwatumikia wananchi na si kutafuta mambo mengine.
Wakati akiwa na miezi michache tu ofisini, Profesa Lumumba aliwahi kusema katika mahojiano kwamba Magufuli ni "real deal", akimaanisha kwamba anayofanya si nguvu ya soda bali ndivyo alivyo kwa maana ya utumishi wa umma uliotukuka.
Kwa mwenendo wake ambao unaonesha haukwazwi na madaraka makubwa aliyo nayo sasa, bila shaka rais huyu wa awamu ya Tano ataendelea kuwa nguzo na hazina ya utawala uliotukuka kwa bara la Afrika, lakini pia atakuwa chachu ya mabadiliko ya kweli yanayotegemewa na wananchi waliowengi.
Bila shaka katika kipindi kifupi, wapo Watanzania ambao wameshaona madhara ya kuwaunga mkono wagombea mafisadi maana ubaya wake, kama alivyoonya Juma katika andiko lake unazidi ule wa chuma kuliwa na kutu maana sumu ya maendeleo ni ufisadi.
Dk Magufuli ameipatia tunu ya neema Tanzania na faida ya kumchagua inaonekana katika kila pembe ya nchi, Afrika na sehemu nyingine ya dunia na sasa Watanzania duniani kote wanatembea kifua mbele wakijivunia kuwa na rais jembe. Hakika waliomuita tingatinga hawakukosea.
Alipoanza kuahidi kutumbua majipu, wengi hawakuamini kwamba atatakeleza kauli hiyo nzito kwa vitendo, kwani hakuna shaka kwamba baadhi ya majipu ni watu waliomfanyia kampeni, kumpigia kura au kuwa naye katika chama chake.
Magufuli ametekeleza utumbuaji majipu kwa vitendo na hivyo kuleta nidhamu katika utumishi wa umma uliokuwa umegubikwa na shombo kubwa ya utovu wa maadili, watu wakijifanyia mambo wanavyotaka, wakiendekeza ubinafsi wao.
Kwa hatua hiyo, sasa Tanzania inaendelea kupata watu wenye wito wa kuutumikia umma wa Watanzania na siyo matumbo yao. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipata kusema kwamba Ikulu ni mahala patakatifu na kwamba anayeingia mahala hapo anapaswa kuwafanya hata marafiki zake wajue kwamba hakwenda pale kupageuza kuwa pango la walanguzi, na bila shaka Magufuli hilo ameliweza.
Kwamba uteuzi ambao amekuwa akiufanya hauangalii sura ya mtu bali uwezo wa wale anaowateua na wateule wake wanapokwenda kinyume cha maadili hasiti kutengua uteuzi wake muda uleule.
Mwalimu Nyerere pia alipata kusema kwamba Ikulu ni mzigo na mtu mkweli kabisa kabisa hapakimbilii kwa kuwa matatizo ya wananchi ni mzigo wa huyo aliyeko Ikulu.
Kwa matendo yake na jinsi anavyopigana kuhakikisha wanyonge wa nchi hii nao wanafaidi keki ya mafanikio, hakuna ubishi kwamba Rais Magufuli analijua hilo na kulifanyia kazi.
Anajua matatizo yetu ni mzigo wake na ndio maana anahangaika kuhakikisha kwamba mapato ya nchi yanafika kunakostahili na yanatumika kwa faida ya Watanzania wote na si genge la watu wachache wenye roho za kinyang'au.
Akiwa anatimiza mwaka mmoja ofisini, hakika Magufuli amedhihirisha kwamba ni yuleyule ambaye wakati akiwa waziri tulitamani awe waziri wa wizara zote kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka.
Shime wananchi, tumuombee kwa Mwenyezi Mungu azidi kumpa siha na moyo wa kututumikia na pia tumuunge mkono kwa kuchapa kazi na kulipa kodi.
Share:

Ukawa wampinga kortini Meya Kinondoni

VIONGOZI wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamekwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa umeya na naibu meya wa Manispaa ya Kinondoni katika Jiji la Dar es Salaam uliompa ushindi Diwani wa Msasani, Benjamin Sitta wa CCM.
Ukawa kupitia kwa Wakili wao, John Mallya wamewasilisha kesi hiyo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 23 mwaka huu, kwa kuwa ulikuwa batili na ulikiuka taratibu za kisheria.
Mallya alisema kesi hiyo ambayo walalamikaji ni aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Jumanne Mbunju na aliyekuwa mgombea wa umeya, Diwani wa Kata ya Kinondoni, Mustafa Muro, imepokelewa lakini haijafunguliwa.
Mbali na Sitta, walalamikiwa wengine katika kesi hiyo ni Naibu Meya, Manyama Mangaru, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli na Ofisa Tawala wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza baada ya kesi hiyo kupokelewa, Wakili Mallya alisema wamefungua kesi hiyo kupinga kile wanachoita uchaguzi ambao CCM walikaa wenyewe na kupigiana kura.
Alisema: “Katika kesi hiyo tunaiomba Mahakama itengue uamuzi uliomchagua meya huyo, iamuru manispaa iitishe uchaguzi wa umeya mara moja pia imuamuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa na wasimamizi wa uchaguzi wafuate taratibu za kisheria.”
Katibu wa Chadema mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo alisema wamefika mahakamani kutafuta haki kwa sababu wanaamini wamenyang’anywa haki yao.
Alisema kilichosababisha uchaguzi wa Ubungo kuahirishwa ni kukiukwa kwa taratibu hivyo Mkurugenzi na Ofisa Tawala wa Ubungo walipoona taratibu zimekiukwa Kinondoni, waliamua kuahirisha uchaguzi.
“Kilichofanyika siku ile ilikuwa ni kuchagua Mwenyekiti wa CCM, lakini siyo uchaguzi wa kumchagua meya wa Kinondoni kwa sababu hata kisheria, uchaguzi unatakiwa kuwa robo tatu ya wajumbe ambao walitakiwa kuwa 23, lakini walikuwa 18, ndiyo maana hata matokeo yalikuwa kura 18,” alisema.
Alidai madiwani wao walinyimwa fursa ya kuingia manispaa na kuwasilisha malalamiko yao hivyo hawamtambui Meya wa Kinondoni na kwa sasa hakuna Meya wa Manispaa hiyo.
Share:

Mbunge-Nimepania kuwainua akinamama, vijana

“NIKIWA mwanamke nimeguswa na kundi la akina mama, kwani naamini sehemu yoyote mwanamke ndiye anayezalisha mali, iwe sekta za viwandani au kilimo. Sisemi kuwa wanaume hawazalishi hapana ila kuna utofauti kwenye namna ya kuzalisha mali.
“Bado naweza kusema kuwa mwanamke ndiye anaweza kukomboa familia hasa kwa kuwa anaweza kufanya kazi yoyote ile na kwa muda wowote,” hiyo ni kauli ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe.
“Hebu tumuangalie mwanamke anaamka mapema katika nyumba na kuelekea kwenye kilimo, wakati huo atatumia nafasi hiyo pia kuchanja kuni na baadaye kuteka maji hivyo nalazimika kusema bado tunaweza kutamka ni nguvu kazi ya taifa na familia," anasema.
Munde ananukuu maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyewahi kusema kwamba eneo lolote ama taifa lenye maendeleo basi mwanamke aliwezeshwa na anamiliki uchumi. Tambwe anasema kauli hiyo ya Mwalimu Nyerere ndiyo iliyomsukuma, akaamua kuanza kuwapa mafunzo ya semina akina mama wajasiriamali wa jimbo la Tabora Mjini.
Anasema licha ya kuanza kuwasaidia nakina mama kwa mafunzo ya semina Tabora Mjini, amekuwa akiwawezesha akina mama wajasiriamali na vijana mkoa mzima tangu mwaka 2010.
Anasema amekuwa akifanya hivyo kwa kuungana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo mkoani Tabora (SIDO) kwa kujali zaidi wajasiriamali wadogo wadogo, kwani hali hiyo itakomboa kundi hili kwa kasi kikubwa.
Anasema tangu mwaka 2010 vipo vikundi ambavyo alivipa mafunzo na mitaji na sasa vikundi hivyo vimesimama imara na vina mitaji mikubwa na vingine ambavyo havikuzingatia maelekezo na mafunzo vilikufa. Anasema anaendesha semina ya mafunzo katika kata zote 29 za jimbo la Tabora Mjini na kila kata alikuwa akichukua takribani wajasiriamali 250 hadi 300.
Anafafanua kwamba alikuwa akitafuta walimu wenye ujuzi ili kufundisha vijana na akina mama wajasiriamali lakini kwa sasa ameamua kwanza kuanza na kina mama.
Munde anaeleza kipato kidogo cha akina mama na vijana ndiyo sababu hasa ilimsukuma ili mafunzo atakayowapatia anaamini atawavusha kutoka walipo na kuondokana na umasikini.
Aidha anasema anaamini makundi haya ndiyo nguvu kazi ya taifa na kwamba wakiwezeshwa kwenye mafunzo na kupatiwa mitaji watafika mbali kimaisha na kutoa mchango wa kiuchumi kwa taifa.
Anasema akina mama wengi kiuchumi ni wanyonge na hivyo anaungana na Rais John Magufuli kutetea wanyonge kwa vitendo kwa kuwawezesha ili waweze kuchangia uchumi wa taifa na kukuza mitaji na kusaidia familia zao kufikia mkakati wa Tanzania ya viwanda.
Anasema mafunzo aliyoendesha katika kata 29 yalilenga kuwapatia ujuzi akina mama ambapo jumla ya waliopewa mafunzo hayo ni 8,700 kwa mujibu wa mahudhurio na kwamba yalimgharimu Sh milioni 23. Munde anabainisha aina ya mafunzo kwa vitendo waliyopata akina mama hao ni utengenezaji wa batiki, utengenezaji mishumaaa, utengenezaji sabuni ngumu na za maji, utengenezaji shampoo, usindikaji mazao na utengenezaji mafuta.
Mafunzo mengine waliyopata ni ufumaji mashuka, ufumaji vitambaa, utengenezaji achali, tomato sauce (nyana za mezani), chili (pilipili), vitafunwa vitokanavyo na zao la muhogo, utunzaji wa vitabu vya hesabu, namna ya kusajili vikundi na namna ya kuweka na kukopa.
Kuhusu kundi la vijana anasema kwa kuwa wameshapatiwa mafunzo sasa anakuja kuwawezesha kifedha ili waweze kutunisha mitaji ama kazi za uzalishaji watakazoanzisha.
Ili kutekeleza azma yake, mbunge huyo alikabidhi fedha taslimu kwa wajasiliamali akina mama kwa kata zote 29 sh milioni 14.5 ambapo kila kikundi kilipokea sh 500,000 taslimu kama mtaji watakaoanzia.
Tambwe anasema pamoja na msaada huo bado anajipanga kwa kuanza mchakato wa kuunganisha vikundi anavyoviwezesha hatkmaye viweze kuunganishwa na Baraza la Taifa la Uwekezaji nchini kuelekea Tanzania ya viwanda.
Anasema baraza hilo litasaidia vikundi hivi kusaidiwa kwenye maeneo kadhaa ili viweze kuyafikia malengo yao na kujikwamua kiuchumi na kwamba ana imani vikundi vitaleta mageuzi ya kweli.
Anatoa mwito kwa vikundi vote vilivyopata mafunzo na mitaji kutumia mafunzo na mitaji hiyo ili kufikia malengo waliyojiwekea hususani kujikwamua kiuchumi.
Zinduna Abdallah, mkazi wa Tambuka Reli anasema yeye ni mmoja wa wanufaika na hivyo anatoa wito kwa wajasiriamali mkoani Tabora kuweka nia ya dhati ya kujiendeleza kiuchumi kwa fedha hizo na mafunzo waliopata. Aziza Bakari Said wa kata ya Ikomwa anasema kikundi chao cha Tupendane walipokea Sh 500,000 kama mtaji na wamejipanga kuzitumia ipasavyo ili kuondokana na umasikini.
Share:

RC kuzindua klabu ya Jogging Moshi

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa klabu mpya ya michezo ya Rhino Sports Talents utakaofanyika Jumamosi Oktoba 29.
Mbali na uzinduzi huo pia kutakuwa na mbio za pole au jogging zitakazofanyika siku hiyo mjini hapa na kufuatiwa na usafi wa mazingira kama ilivyokawaida ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Mratibu wa Jogging hiyo, Nelson Mrashan alisema kuwa Said Mecky Sadiki anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa klabu hiyo ya michezo.
Mrashan alisema kuwa, Jogging hiyo itashirikisha watu wa rika mbalimbali wakiwemo wazee, vijana na hata watoto pamoja na walemavu ili kujenga miili na kuepukana na magonjwa mbalimbali. Alisema kuwa mbali na watu wa kawaida pamoja na viongozi wa serikali ya mkoa wa Kilimanjaro na wale wa taasisi mbalimbali, pia kutakuwa na viongozi wa Polisi na Magereza.
Mbio hizo za pole zitakuwa zikifanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi sambamba na kuitikia wito wa Rais John Magufuli ya kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Mrashan alisema kuwa mbio hizo zitaanzia katika mzunguko wa Moshi-Arusha kwenda hadi katika tangi la maji kupitia barabara ya Sekotoure na kurudi katika mzunguko huo wa Moshi-Arusha.
Alisema kuwa anawaomba watu kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uzinduzi huo na baadaye katika jogging ili kuweka fiti miili na kuiepusha na maradhi mbalimbali, kwani michezo ni furaha, afya na ajira.
Share:

nunua vitabu vya watoto kuanzia chekechekea mpaka darasa la saba

nunua vitabu vya watoto kuanzia chekechekea mpaka darasa la saba