Thursday, 27 October 2016

Wa-Baha’i kufanya sherehe kubwa

JUMUIYA wa Baha’i ya jijini Dar es Salaam itaungana na Wa-Baha’i wengine duniani, kuadhimisha kuzaliwa kwa waanzilishi wa imani yao ya Baha’i, Bab na Baha’u’llah, Novemba mosi na 2, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwakilishi wa Mawasiliano wa Baraza la Kiroho la Baha’i Dar es Salaam, Qudsiyeh Roy, maadhimisho ya kuzaliwa Bab ambaye ni Mtume Mtangulizi wa imani ya Baha’i, yatafanyika Novemba mosi na sherehe ya kuzaliwa kwa Baha’u’llah ambaye ni Mtume Mwanzilishi wa imani hiyo itafanyika Novemba 2.
Maadhimisho hayo yatafanyika ukumbi wa Baha’i Senta, Upanga Magharibi, jirani na makao makuu ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) saa 11.30 jioni kwa siku hizo.
“Usherehekeaji wa siku tatu za kuzaliwa kwao kwa mfuatano, kuna umuhimu wa kialama kwa sababu ujumbe wa Bab na Baha’u’llah, umeingiliana vivyo hivyo kwa namna nyingi. Siku ya kuzaliwa husherehekewa na waumini kwa shangwe kubwa na shukrani kwa Mungu,” alisema Roy.
Alieleza kuwa Bab na Baha’u’llah walizaliwa miaka 197 na 199 iliyopita kwa mfuatano na maisha yao yalikuwa ya kipekee katika nyanja ya historia ya kidini.
Imani ya Baha’i’ ni dini huru inayojitegemea, inayomwabudu Mungu mmoja. Inakubali mwanzo mtukufu na kusudi moja la dini zote kuu za dunia; na hufundisha kuwa Mungu amefunua ujumbe mpya katika zama hizi kwa lengo la kustawisha umoja wa jamii ya wanadamu.
Share:

Wachina mbaroni kwa kumteka mwenzao

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia raia wawili wa China kwa tuhuma za kumteka nyara Mchina mwenzao, Liu Hong (48) ambaye ni mfanyakazi wa Le Grande Cassino, wakidai kulipwa Dola za Marekani 19,000 (zaidi ya Sh milioni 38).
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi, Simon Sirro alisema walipokea taarifa kwamba raia huyo wa China alitekwa nyara na watu wasiofahamika.
Alisema taarifa hizo zilieleza kwamba Liu alitekwa nyara Oktoba 23, mwaka huu saa moja asubuhi na ndipo polisi wakaunda kikosi kazi kwa ajili ya ufuatiliaji wa taarifa hiyo na kubaini watekaji walikuwa wakidai Yen 100,000 (fedha za China) ambazo ni sawa na Dola za Marekani 19,000.
“Oktoba 24, mwaka huu saa 11 jioni kikosi kazi cha wizi wa makosa ya kimtandao cha Polisi Kanda Maalumu walibaini kuwa wateka nyara hao wapo katika Hoteli ya Palm Beach Upanga na walipofika hapo wakaanza kukagua chumba kimoja baada ya kingine,” alisema Kamanda Sirro.
Alisema polisi walipofika chumba namba tisa na kugonga wahusika waligoma kufungua mlango ndipo polisi waligundua wateka nyara hao kuwepo katika chumba hicho.
Alisema wakiwa wanajiandaa kuvunja mlango, mara mtuhumiwa mmoja Wang Young Jing (37) raia wa China aliamua kufungua mlango na kumkamata akiwa na Liu ambaye ni mtekwa nyara.
“Askari walipoingia ndani walimkuta aliyetekwa nyara akiwa hajitambui akiwa na majeraha usoni. Pia katika tukio hili, polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mwingine aitwaye Chen Chung Bao (35) raia wa China ambaye ndiye aliyekodi chumba hicho,” alieleza kamanda.
Alisema ndani ya chumba hicho kulikutwa vipande viwili vya taulo walivyotumia kumfunga mikono, kamba za plastiki na bomba la sindano. Alisema majeruhi alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu na watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa. Upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
Wakati huo huo, Polisi ilifanya operesheni katika maeneo ya katikati na pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam na kuwakamata watuhumiwa 57 kwa makosa mbalimbali ya uhalifu.
Kamanda Sirro alisema Mkoa wa Temeke walikamatwa watuhumiwa 21, Ilala watuhumiwa 19 na Kinondoni watuhumiwa 17.
“Baadhi ya watuhumiwa hao ni vikundi mbalimbali wanaojiita majina tofauti ikiwemo ‘Panya road’, ‘Black American’, Taifa jipya na Kumi ndani na kumi nje,” alieleza na kuongeza kuwa watuhumiwa walikamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Kivule, Mbagala, Buguruni, Kiluvya, Gongo la Mboto, Tandika, Ukonga, Banana, Kunduchi, Kawe na Keko.
Alisema watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuvunja nyumba usiku na kuiba, kuvuta na kuuza bangi, kuuza na kunywa gongo na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Katika tukio jingine, watu wawili wamekamatwa katika maeneo ya Karakata Relini kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa na gari lenye namba T 550 CWG Toyota Carina likiwa na viroba 11 vya bhangi, gongo lita 80, mitambo 10 ya kutengeneza pombe ya gongo, mirungi kilo mbili na vifaa vya kuvunjia na funguo za vitasa mbalimbali.
Share:

Wednesday, 26 October 2016

Vyuo vikuu waanza kupata mikopo

AKAUNTI za wanafunzi wa vikuu nchini zitakuwa zimeanza kunona baada ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kusema kuanzia jana imeanza kuingiza fedha za wanafunzi wote wa elimu ya juu ambao wamekidhi vigezo vya kupatiwa mikopo.
Wanafunzi 20,183 kati ya wanafunzi 58,010 ambao wamedahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ndio ambao wamepangiwa kupata mikopo na bodi hiyo baada ya kutimiza vigezo vyote vilivyowekwa.
“Napenda kuwahakikishia waombaji kuwa boom limeanza kuingia leo, kwa kuwa fedha hizo zinapitia benki baadhi wanapata kesho na wengine siku zinazofuata, ila sisi tumeshatimiza wajibu wetu,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul Razaq Badru wakati akizungumza na gazeti hili jana.
Kwa idadi hiyo ya wanufaika wa mikopo iliyotangazwa na bodi, ni wazi kuwa wanafunzi wengine 37,827 hawatapatiwa mkopo kutokana na kukosa sifa ambao zimeainishwa na bodi hiyo.
Jumla ya wanafunzi 88,163 waliomba mikopo ya HESLB.
Badru alifafanua kuwa miongoni mwa waliokosa mikopo ni waombaji walioomba wakati wana umri wa zaidi ya miaka 30 na wengine wamekosa sifa za kukopeshwa kwa kuwa hawakuomba kabisa.
“Kuna wanafunzi kama 90 wamekosa mikopo kwa sababu ya umri wao kuwa mkubwa, sisi tunatoa mikopo kwa wanafunzi wanaotoka sekondari. Pia kuna wanafunzi wengine kama 6,561 hawakuomba kabisa mikopo licha ya kudahiliwa na TCU hao nao tunasema hawana sifa ya kukopeshwa,” alisema Badru.
Hata hivyo, kuna nafasi za wanafunzi 5,534 ambazo zimeachwa na bodi hiyo kwa ajili ya waombaji waliochelewa kupata udahili au kwa wale ambao wamekosa mikopo halafu wakakata rufaa na kushinda.
Katika ufafanuzi wa waliopata mikopo, Badru alisema kati ya wanafunzi hao yatima waliopata mkopo ni 873, wenye ulemavu wa viungo wako 118, wahitaji wenye mzazi mmoja 3,448, waliofadhiliwa na taasisi mbali mbali 87, wahitaji wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159 na Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine ni 9,867.
Badru pia alisema wanafunzi wengine 93,295 ambao wanaendelea na masomo yao, nao wameshaingiziwa fedha zao kwa utaratibu uliowekwa wakati wanapatiwa mikopo yao ya awali. Bajeti ya Serikali iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni Sh bilioni 483.
“Ila baada ya kuwapatia mikopo hiyo tutaendelea na uhakiki kubaini wale ambao walijaza taarifa ambazo sio sahihi na pia tunataka kuona anayepata mkopo ni mwanafunzi mwenye sifa tu,” alisema Badru.
Alifafanua kuwa baada ya hatua hiyo wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo.
Pia waombaji waliowasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao. Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso.
Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.
Juzi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifunga maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi inaendelea kufanya uhakiki wa taarifa za waombaji wa mikopo na akasema kufikia leo Alhamisi asilimia 90 ya waombaji waliotimiza masharti wawe wameshalipa fedha zao.
Aliwataka watumishi wa bodi ya mikopo kutimiza wajibu wao kuhakikisha kwamba kwa wale ambao uhakiki wao umekamilika wapatiwe mikopo hiyo kwa wakati.
Alisema kamwe serikali haitawavumilia watumishi ambao watachelewesha kwa makusudi mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Pia aliagiza kuwa kama kuna tatizo juu ya utoaji wa mikopo, taarifa itolewe ndani ya serikali haraka ili ifanyiwe kazi kuzuia mgogoro kati ya wanafunzi na serikali yao.
Share:

NSSF hatarini ‘kulizwa’ bil 270/-

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekiri mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa linaweza kupoteza kiasi cha Sh bilioni 270, zilizoingizwa kwenye mradi wa ubia baina yake na Kampuni ya Azimio Housing Estates (AHEL), kama shirika hilo lisipokuwa makini.
Pamoja na hayo, kamati hiyo baada ya kubaini madudu kadhaa katika hesabu za shirika hilo, imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalumu wa mikopo yote iliyotolewa na NSSF kwa vyama vya akiba na mikopo.
Akijibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mradi huo ambao ni ujenzi wa mji wa kisasa katika eneo la Dege Kigamboni jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema kwa sasa kinachoangaliwa kwenye mkataba huo ni athari za kupoteza fedha hizo.
Profesa Kahyarara alisema pamoja na shirika hilo kuwepo kwenye ubia huo, lakini limegundua ekari zilizopo kwenye mkataba si za uhalisia.
Alisema kwa mujibu wa mkataba zilitakiwa ziwe ekari 20,000 lakini kiuhalisia baada ya kufanya tathmini zipo ekari zaidi ya 3,500.
Aidha, alifafanua kuwa bei iliyothaminiwa kwenye ekari hizo pia ni tofauti kwani mwekezaji huyo alithaminisha ardhi hiyo kwa Sh milioni 800, lakini baada ya NSSF kufanya uchunguzi wake ikabaini kuwa ekari moja thamani yake ni Sh milioni 25.
Kwa mujibu wa taarifa za CAG zinaeleza kuwa NSSF iliingia ubia na kampuni hiyo na kuanzisha kampuni maalumu kwa jina la Hifadhi Builders Limited.
Katika mkataba huo, Azimio Housing Estates itatakiwa kuendeleza ekari 20,000 za ardhi zilizopo Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa mji mpya wa kisasa wa Kigamboni kupitia mradi uliopo eneo la Dege.
Hata hivyo, mradi huo umesimama utekelezaji wake tangu Februari, mwaka huu kutokana na mwekezaji kutokuwa na fedha huku NSSF tayari ikiwa imeshaingiza Sh bilioni 270.
Katika ubia huo, NSSF inamiliki asilimia 45 ya hisa wakati Azimio Housing Estates inamiliki asilimia 55 ya hisa na jumla ya gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 653.44.
Kwa mujibu wa utaratibu wa uchangiaji mtaji, NSSF itatoa fedha zenye thamani ya asilimia 45 ya gharama za mradi na Azimio itatoa fedha zenye thamani ya asilimia 35 ya gharama za mradi pamoja na ardhi ambayo itathaminishwa kuwa asilimia 20 ya gharama za mradi.
Kutokana na hali, Profesa Kahyarara alisema kwa sasa unafanyika ukaguzi maalumu kwenye miradi yote ya NSSF ikiwemo mradi huo.
“Mheshimiwa Mwenyekiti hatuwezi kwa sasa kutoka kwenye ubia huu tunaweza kupoteza fedha hizo, lazima tuwe makini ili kuhakikisha mwekezaji huyo Azimio anarejesha fedha hizo,” alisisitiza mkurugenzi huyo.
Akihoji kuhusu utata uliojitokezakwenye ripoti ya CAG kuhusu mradi huo, mbunge wa Msalala Ezekiel Maige, alibainisha kuwa mradi huo umegubikwa na uchafu.
“Tukubaliane tu mradi huu umegubikwa na madudu, kwa nini usivunjwe na una uhakika gani utakuwa safi NSSF ikiendelea kuwa kwenye huo mkataba tena? Alihoji Maige.
Naye Mbunge wa Magomeni, Jamal Kassim Ali alisema kwa taarifa zilizopo kampuni hiyo ya Azimio ilitaka kukopa NSSF wakati ina tayari ina deni katika shirika hilo, huku ikiwa haijaingiza fedha zozote katika mradi huo wa ubia.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Aeshi Hilaly alitahadharisha kuwa kwa sasa mkandarasi wa mradi huo yupo eneo la mradi, hivyo kuna uwezekano wa kupoteza fedha nyingi zaidi endapo fedha zilizowekezwa tayari na NSSF hazitorejeshwa.
Kwa upande wake, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba alihoji ni kwa nini Azimio imeingia ubia tena katika kutekeleza mradi wa Mji wa Kisasa wa Arumeru na kupewa kazi nyingine ya kuwa mhandisi mshauri wakati utekelezaji wake ni mbovu.
Alihoji NSSF ina mkakati gani wa kurejesha kiasi cha Sh bilioni 43.9 zilizolipwa kwa kampuni hiyo ya Azimio kwa kazi ya ushauri ambayo lengo lake halijatimia.
Kuhusu suala la mikopo, PAC imeagiza ufanyike ukaguzi maalumu wa mikopo yote iliyotolewa na shirika hilo kwenye Saccos, baada ya kubainika kuwa Saccos ya Bumbuli ilipatiwa mkopo wa Sh bilioni 2.4 ndani ya mwaka mmoja.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka alitoa agizo hilo kwa CAG na kusisitiza kuwa kitendo cha Saccos ya Bumbuli kupatiwa fedha hizo ndani ya mwaka mmoja kimewashtua wajumbe wa kamati hiyo. Kaboyoka alisema maelekezo mengine kuhusu suala hilo yatatolewa bungeni kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge 117(10).
Awali wakichangia wajumbe wa kamati hiyo akiwemo Mbunge wa Kilindi, Omar Kigua alihoji vigezo vilivyotumika mpaka Saccos moja kupewa mkopo mara tatu. Alifafanua kuwa kwa mujibu wa ripoti ya CAG, NSSF imetoa mikopo kwa SACCOS tisa kiwango kinachozidi asilimia 50 ya thamani ya mali za Saccos husika kinyume cha Sera ya kukopesha ya shirika hilo.
Katika ripoti ya CAG mbali na Bumbuli pia Saccos zingine zilizopatiwa fedha nyingi ni Korongo Amcos Saccos, UMMA Saccos, SBC Saccos Ltd, Hekima Saccos, Ukombozi Saccos Ltd, Uzinza Saccos Ltd, Harbour Saccos, na Umoja Saccos.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Profesa Samwel Wangwe alisema kwa sasa bodi imesimamisha mikopo kwa Saccos zote hadi uchunguzi ukamilike na utawekwa utaratibu mpya wa utoaji mikopo.
Share:

U HEARD: Alichoongea H Baba kuhusu nyumba walizopost Alikiba na Diamond

Jana October 25, 2016 kwenye mtandao wa Instagram kulikuwa na majibizano ya mashabiki wa mastaa wakubwa wa muziki wa Bongo Flava Tanzania nawazungumzia Diamond Platinumz na Alikiba hukua akiwepo mtu wa kati H Baba ambaye pia aliwahi kutofautiana na Diamond Platinumz siku za nyuma na sababu ikitajwa na kuwa waliibiana nyimbo studio.
Kupitia account ya Instagram ya Diamond Platinumz jana alipost picha akiwa kwenye nyumba yake anayodai kuwa ameinunua nchini Afrika Kusini na kwa mujibu wake alikua amefika hapo kwa mara ya kwanza tangu alipoinunua nyumba hiyo. Na baada ya muda mfupi pia kuna picha zilianza kusambaa zikimuonesha Star single ya Aje, Alikiba akiwa kwenye nyumba iliyodaiwa ni yake pia. 
Sasa msanii H Baba naye aliamua kupost maneno kwamba kama kweli nyumba hizo ni zao basi wangepost documents za kuonesha wakizinunua na sio picha tu.
“Siku zote mimi ninachojua mtu anayependa kuwatangazia watu ni mstaarabu sana na kitu cha kwanza mtu anaponunua nyumba lazima apewe mkataba then angepiga picha akiwa anasaini sio wanatupostia picha tu. Anapost picha kwasababu Alikiba amepost nyumba na yeye ndio apost? Unatakiwa kumpongeza tu muziki ni ushindani sio kujibizana kwa picha”:- H Baba
Share:

Kiwango cha Pesa utatakiwa kulipa Ili upate Collabo na msanii Akothee

Kama ilivyo ahadi yangu kwako, ni kuhakikisha haipitwi na story yoyote mtu wangu na leo nimeipata hii kutoka kwa msanii wa muziki kutoka Kenya, Akothee. Inawezekana wengi wetu tunafahamu tu kwamba ni msanii na labda kwasababu ana historia ya kuwa na pesa nyingi basi hata muziki anaufanya tu kama starehe. 
Kwa mujibu wa Citizen, taarifa hii ikufikie kama ni msanii na unahitaji kufanya collabo na Akothee basi unatakiwa kuandaa mfuko wako kisawasawa. Akothee ametangaza kiwango cha Pesa ambacho utatakiwa kumlipa ili uweze kuingia naye studio kuwa ni Shilingi Milioni 1 za Kenya ambazo ni zaidi ya shilingi Milioni 21 za Tanzania.
“Ukiwa msanii, hautakiwi kukimbilia kusaini deal za record labels, uanweza kutengeneza pesa zako kuoitia social media. Usijikalishe na kusubiri pesa zije. Sasa kwa upande wangu wala usijisumbue kunipigia simu kama hauna shilingi Milioni 1 za kufanya collabo,” – Akothee
Akothee amesema anatafikiria kusaini deal na lebel za Marekani endapo tu zitakuwa na maslahi ya kueleweka. 
Star huyo wa single ya ‘Yuko Moyoni’ hivi karibuni amefanikiwa kushinda tuzo mbili za best East African female artist zilizotolewa na waandaaji wa jarida la African Muzik Magazine (AFRIMMA) pamoja na African Entertainment Awards USA (AEAUSA).


Share:

China imeshikilia rekodi hii ya dunia kwenye biashara ya Smartphone!!

Biashara ya Simu za kisasa maarufu kama Smartphone au Simu Janja imeendelea kukua na kuongeza ushindani wa makampuni ya utengenezaji wa bidhaa hizo duniani kote. Leo October 26, 2016 mtu wangu nimeipata hii kuhusu nchi iliyofanya vizuri kwenye biashara ya Smartphone duniani.
Ripoti iliyotolewa na kampuni ya GFK ya Ujerumani inaonesha kuwa, mpaka kufikia robo ya tatu ya mwaka huu, China imeongoza katika soko la simu za smartphone na kuendelea kukua zaidi, huku ikiongeza msukumo mkubwa wa ukuaji wa soko la simu hizo duniani.
 Ripoti hiyo inasema simu milioni 353 aina ya smartphone zimeshauzwa katika robo ya tatu ya mwaka huu duniani kote, na idadi hiyo imetajwa kuongezeka kwa asilimia 7.5 kuliko mwaka 2015 kwa wakati kama huo, huku simu milioni 113 kati ya hizo zikiuzwa katika soko la China pekee.

Share:

Agizo la Waziri Hamad Masauni kwa Askari na Madereva endapo ajali itatokea

Ajali za Barabarani zimekuwa zikipoteza maisha ya wananchi wengi kila siku huku wengine kupata ulemavu wa kudumu.  Leo October 25, 2016 Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Eng. Hamad Masaudi imetoa mkakati ili kupunguza ajali hizo.
Naibu Waziri Eng. Hamad Masauni amesema kuwa mkakati huo utahusikana na kuchukua hatua kali kwa askari ambao watahusika na masuala ya ukaguzi  wa vyombo vya usafiri, madereva pamoja na wamiliki wa magari yatakayohusika kwenye ajali.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri Masauni amezitaja wilaya za Ilala na Kinondoni kuwa zinaongoza kwa ajali nchi Tanzania.
Ayo TV inakuletea taarifa kamili ya Naibu Waziri Hamad Masauni wakati akizungumzia mikakati ya Serikali juu ya ajali za Barabarani.
Share:

PICHA 7: Jinsi Star Davido anavyomuhudumia mtoto wake

Moja kati ya vitu ambavyo hufanywa siri sana na mastaa wengi duniani ni kuonesha jinsi wanavyoishi na familia zao kuanzia maisha ya mahusiano ya kimapenzi au malezi ya watoto. Lakini kwa baadhi yao huwa tofauti sana linapokuja suala la malezi ya watoto na hili limedhihirishwa mara kadhaa na mastaa wakubwa kama Chris Brown, Mwana FA, Diamond Platnumz na wengine wengi ambao wamefanikiwa kupata watoto.
Leo nimezipata picha 7 alizozipost Snapchat star wa hit single ya How Long aliyompa collabo female singer Tinashe kutoka Marekani. Davido ameonekana akiwa na mtoto wake wa kike.




Share:

PICHA 12: Watoto wanavyoshuka na kupanda mita 800 za mlima huko China ili kwenda shule

Katika milima ya jimbo la Sichuan kusini magharibi mwa China, kundi la watoto ambalo lilikuwa likishuka mita 800 kwenye mlima ili kufika shule huku wakitumia njia za asili ambazo ni ngazi za miti ambayo ni hatari sasa wanajengewa ngazi za chuma.
Ngazi hiyo ya chuma inayojengwa na wanakijiji itakuwa na mabomba 1,500 ya chuma na inatarajiwa kukamilika mwezi November mwaka huu, ujenzi wa ngazi hizo zenye gharama ya dola za marekani 150,000 ambazo ni karibu Tsh za kitanzania milioni 327, ilianza kujengwa na wanakijiji mwezi August mwaka huu. 
Ngazi hiyo inatarajiwa kuwa na muundo imara zaidi pia inatarajiwa itakuwa yenye usalama zaidi kwa hata wanakijiji wa kijiji hicho ambao watakuwa wanaitumia kupanda na kushuka kila wiki kununua bidhaa mbalimbali na kufanya biashara zao katika soko ambalo liko mbali na wanakoishi. Siku za nyuma wanakijiji walikuwa wakitumia miti ya mizabibu ambayo ilikuwa mibovu.









Share:

nunua vitabu vya watoto kuanzia chekechekea mpaka darasa la saba

nunua vitabu vya watoto kuanzia chekechekea mpaka darasa la saba