Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu Waombaji wote
walioomba kudahiliwa katika kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada
(Diploma) na Umma kwa ujumla kuwa dirisha la maombi lilifungwa mnamo
tarehe 15 Oktoba 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya nne kwa waombaji
wa kozi hizo.
Uteuzi wa awamu ya nne kwa waombaji wa Astashahada na Stashahada unatarajiwa kutangazwa mnamo tarehe 2 Novemba 2016, hivyo basi waombaji wanaombwa kuwa na subira ili kutoa muda kwa Baraza kukamilisha taratibu za uteuzi huo.
Maombi mapya ya Udahili:
Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) utafunguliwa tena tarehe 2 Novemba 2016 hadi tarehe 6 Novemba 2016 ilikujaza nafasi za udahili zilizobaki wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya nne. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuweza kuomba hapo awali.Maombi ya Uhamisho:
Mwombaji aliyechaguliwa ataweza kuomba uhamisho kutoka chuo ama kozi moja kwenda nyingine kupitia kwenye ukurasa wake binafsi (profile) tu. Uhamisho huu utategemea nafasi zilizopo, ushindani na alama za chini za kujiunga na kozi (cut-off). Orodha ya Vyuo na Programu zenye nafasi inapatikana hapaHatua za kuomba uhamisho:
1. Ingia kwenye ukurasa wako binafsi (profile) kwa kutumia jina la mtumiaji (Username) na neno la siri (Password) ulivyopewa wakati wa usajili2. Bofya kitufe kilichoandikwa “Transfer Request/Kuomba Uhamisho”, na punde ukurasa utafunguka
3. Utafunguka ukurasa unaokuonesha chuo na kozi uliyochaguliwa awali
4. Chagua kada unayohitaji kuhamia
5. Chagua chuo unachohitaji kuhamia
6. Chagua kozi unayohitaji kuhamia
7. Mfumo utatathmini kama una sifa za kujiunga na kozi uliyochagua. Iwapo una sifa za kujiunga na kozi hiyo mfumo utakuomba ulipie Sh. 30,000/- kama ada ya maombi ya uhamisho. Kiasi hiki hakitarudishwa (non-refundable)
8. Bofya kitufe kilichoandikwa “Confirm Transfer Request/Kamilisha Maombi”.
9. Utapewa muhtasari wa maombi yako ya uhamisho pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye namba ya simu ya mkononi uliyoweka wakati wa usajili na barua pepe kukujulisha kwamba umekamilisha maombi.
Jinsi ya kulipia (Malipo ya tafanywa kwa M - pesa tu):
1. Piga *150*00#2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa
3. Chagua 4. Weka namba ya kampuni
4. Tafadhali weka namba ya kampuni (No. 607070)
5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (No. 1234)
6. Weka kiasi (e.g. 30,000/=)
7. Weka namba ya siri
8. Bonyeza 1 kuthibitisha.
Angalizo (Disclaimer):
1. Kuhama chuo na kozi si lazima.2. Uhamisho utafanyika kwa kozi zile tu zenye nafasi na kwa vyuo ambavyo bado havijafunguliwa na kuanza masomo.
3. Uhamisho ni kwa wale waombaji waliokwisha kuchaguliwa kupitia mfumo wa pamoja wa udahili tu.
4. Maombi ya uhamisho yanaweza kufanyika MARA MOJA na kwa kozi moja
5. Iwapo umefanikiwa kupata uhamisho, majibu yataonekana kwenye ukurasa wako binafsi (Profile). Majibu haya pia yatatumwa kwenye namba yako ya simu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupitia barua pepe baada ya tarehe ya mwisho ya maombi (6 Novemba 2016).
6. Uhamisho utategemea ufaulu wa waombaji na nafasi zilizopo. Hii inamaanisha kwamba wenye ufaulu wa juu ndio wenye uwezo mkubwa wa kukubaliwa kuhama.
7. Maombi yatakayotumwa kwa barua au barua pepe hayatoshughulikiwa.
8. Waombaji waliomba uhamisho na kukosa awamu iliyopita wataruhusiwa kuomba tena bila malipo mapya.
Imetolewana
Ofisiya Katibu Mtendaji
Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Tarehe: 1 Novemba, 2016